Swali
Je! Ni nini maana ya kauli mbiu ”imani inayotafuta ufahamu”?
Jibu
Usemi “imani inayotafuta fahamu” inachukuliwa kuwa mojawapo ya fafanusi kuhusu utamaduni na elimu ya Wayunani na Warumi wa zamani. Kauli hii ilitafsiriwa kutoka Kilatini Imani inayotafuta hekima (fides quaerens intellectum). “Imani inayotafuta ufahamu” inamaanisha kwamba imani katika Mungu iliyofunuliwa katika Kristo huibua swali la kutaka kujua ufahamu wa kina zaidi.
Kifungu kamili “imani inayotafuta ufahamu” kilianzishwa na Anselm wa Canterbury mnamo mwaka wa (1033-1109), mtawa, mwanatheolojia, na Askofu Mkuu wa Canterbury, katika kitabu chake Proslogium.
Kabla ya Anselm, Augustine wa Hippo (AD 354-430) alibuni kishazi sawia cha Kilatini: Crede ut intelligas, “amini ndio uweze kuelewa.” Augustine aliamini kwamba ufahamu kumuhusu Mungu huja kabla ya imani katika Yeye, walakini imani katika Mungu huleta hamu ya kudumu ya kutaka kumfahamu zaidi. Ili kuliweka kwa urahisi, Wakristo kwa bidi wanataka kuelewa kile wanachoamini.
Anselm alikubaliana na Augustine kwa hilo. Aliamini kwamba imani inahitajika katika kufahamu, lakini pia akili ni muhimu katika kuelewa. Kulingana na Anselm, imani ya Kikristo huanzisha jitihada ya kumjua na kumuelewa Mungu na kile tunachoamini Kumhusu.
Imani, kulingana na Anselm, inawafanya waumini kutafuta ufahamu kwa furaha ya kumjua Mungu na kumpenda Yeye. Katika kitabu chake Faith Seeking Understanding: An Introduction to Christian Theology, Daniel L. Migliore anaeleza, “Kwa Anselm, imani hutafuta ufahamu, na ufahamu huleta furaha.” Anselm mwenyewe aliandika katika proslogium, “Nakuomba, Ee Mungu, nijulishe nikujue na kukupenda ili nipate kushangilia ndani yako.”
Biblia inakuza wazo la imani inayotafuta ufahamu. Yesu alifunza kwamba amri kuu inatusihi tumpende Bwana na akili zetu zote (Mathayo 22:37). Akizungumza na wanafunzi wake katika mojawapo ya mwonekano baada ya ufufuo, Yesu “akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko” (Luka 24:45). Imani ndiyo inayoushinda ulimwengu (1 Yohana 5:4), lakini imani hiyo inaambatanishwa na kumfahamu Mungu: “Nasi pia twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi ufahamu ili tupate kumjua yeye aliye Kweli” (aya ya 20).
Katika kujadili usemi wa Anselm, kitabu cha Falsafa cha Stanford (Stanford Encyclopedia of Philosophy) kinarekebisha masuala mawili potofu. Wengi wamechukulia “Imani inayotafuta ufahamu” kumaanisha kwamba Anselm alitarajia imani nafasi ya ufahamu, lakini hii iko mbali na ukweli. Kwa Anselm, imani ni upendo kwa Mungu ulio hai katika kutafuta ufahamu wa kina kumhusu Mungu.
Pili, wanafalsafa wengi wamefikiri “imani inayotafuta ufahamu” inahusisa waumini tu pekee kwa sababu huanza na imani. Lakini Anselm aliamini kwamba akili pekee ilitosha kumsadikisha hata mtu mwenye akili ya kadri juu ya kuwepo kwa Mungu. Kitabu cha Anselm Monologion kinaanza kwa maneno haya: “Ikiwa mtu yeyote hajui, ama kwa sababu hajasikia au kwa sababu haamini kwamba kuna asili moja, ambayo ni kuu kati ya vitu vyote vilivyomo, ambaye inajitoleshelesha pekee yake katika furaha yake ya milele, ambaye kupitia kwa wema wake wenye kudura ambao unatupa na kuleta vitu vingine vyote kuwepo na kustawi kwa aina yoyote, na mambo mengine mengi sana ambayo ni lazima tuamini kuhusu Mungu au uumbaji wake, nadhani angeweza angalau kujisadikisha mengi ya haya kwa akili pekee, ikiwa yeye ni wa akili kiasi.”
Usemi wa Anselm wa “imani inayotafuta ufahamu” uliunda msingi wa mfumo wa kitheolojia na falsafa wa zama za kati (medieval) ujulikanao kama falsafa ya uwanazuoni (enzi za kati), ambayo ilitafuta kuunganisha imani na akili kuwa mfumo mmoja unaoambatana.
English
Je! Ni nini maana ya kauli mbiu ”imani inayotafuta ufahamu”?