Swali
Jinsi ya kufika mbinguni-Je! kuna maoni gani kutoka kwa dini tofauti?
Jibu
Inaonekana kuwa na ina tano kuu kuhusu jinsi ya kufika mbinguni katika dini za ulimwengu. Wengi wanaamini kwamba kufanya kazi kwa bidii na hekima kutaongoza kwenye utimizo wa mwisho, iwe huo ni umoja na mungu (Uhindu, Ubudha, na Baha’i) au uhuru na kujitegemea (Sayansi, Ujaini). Wengine, kama imani ya Waunitariani na Wicca hufundisha maisha ya baada ya kifo kuwa chochote unachotaka kiwe, na wokovu sio suala kwa sababu asili ya dhambi haipo. Wachache wanaamini kuwa maisha ya baada ya kifo haipo au haijulikani kiwa ya kufirika
Vyanzo vya ibada ya Mungu wa Kikristo-Uyahudi kwa ujumla hushikilia kwamba imani katika Mungu na/au Yesu na kutimizwa kwa matendo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ubatizo au uinjilisti wa nyumba hadi nyumba, kutahakikisha muumini ataenda mbinguni. Ukristo pekee ndio unaofundisha kwamba wokovu ni zawadi ya bure ya Mungu kupitia imani katika Kristo (Waefeso 2:8-9), na hakuna kiasi cha kazi au juhudi zinazohitajika au zinawezesha kufika mbinguni.
Ukanaji Mungu (Atheism): Watu wengi wasioamini kuwa kuna Mungu wanaamini kwamba hukuna mbinguni-hakuna maisha ya baaada ya kifo hata kidogo. Baada ya kifo, watu huacha kuishi. Wengine hujaribu kufafanua maisha ya baada ya kifo kwa kutumia mbinu ya kukadiria kiasi na mbinu zingine za kisayansi.
Baha’i: Kama dini nyingine nyingi, Baha’I haifundishi kwamba mwanadamu alizaliwa na asili ya dhambi au kwamba manadamu anahitaji kuokolewa kutokana na uovu. Mwanadamu anahitaji tu kuokoa kutokana na imani zake potofu za jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi anavyopasw akuingiliana na ulimwengu. Mungu alituma wajumbe kuwaelezea watu jinsi kufikia ufahamu huu. Abraham, Krishna, Zoroaster, Moses, Budha, Yesu, Muhammad, na Baha’u’llah. Manabii hawa kwa hatua walifunua asili ya Mungu kwa ulimwengu. Baada ya kifo, roho ya mtu inaendelea safari yake ya kiroho, labda kupitia majimbo yanayojulikana kama mbingu na kuzimu, mpaka inakuja hatua ya mwisho ya kupumzika, umoja na mungu.
Ubudha: Ubudha pia unaamini kwamba mbingu, au “nirvana,” inapaswa kuunganishwa tena kwa roho na mungu. Kufikia Nirvana, hali ya kupendeza, ya furaha, ya kiroho, inahitaji kufuata Njia ya Nane. Hii ni pamoja na kuelewa ulimwengu, na kutenda, kuzungumza, na kuishi kwa njia sahihi na kwa nia sahihi. Kujua njia hizi na nyingine ya njia nane itarudisha roho ya mwabudu kwa mungu.
Dini ya Kichina: Dini ya kichina sio kanisa lililopangwa, lakini ujumuishaji wa dini na imani tofauti ikiwa ni pamoja na Taoism na Ubudha. Baada ya kifo, waabudu wanahukumiwa. Wema hutumwa paradiso ya Buddah au mahali pa makao ya Tao. Na wabaya hutumwa kuzimu kwa kipindi cha muda na kisha kuzaliwa tena.
Ukristo: Ukristo ndio dini pekee ambayo inafundisha mwanadamu hawezi kufanya chochote ili kupata au kujilipia kuingia mbinguni. Mwanadamu, mtumwa wa asili ya dhambi aliyezaliwa naye, lazima kutegemea kabisa neema ya Mungu katika kutumia dhabihu ya Yesu Kristo kwa dhambi za muumini. Watu wameokolewa kwa imani katika kifo na ufufuo wa Kristo. Baada ya kifo, roho za Wakristo huenda mbinguni, huku roho za wasioamini huenda kwenye mahalipa muda paitwayo kuzimu. Katika hukumu ya mwisho, wasioamini wanatengwa na Mungu milele katika ziwa la moto.
Dini ya Confucius: Dini ya Confucius hukazia tabia ifaayo maishani, si mbingu ya wakati ujao. Maisha ya baada ya kifo hayajulikani, kwa hiyo jitihada zote zinapaswa kufanywa ili kufanya maisha haya kuwa bora zaidi, kuheshimu mababu, na kuheshimu wazee.
Othodoksi ya Mashariki: Othodoksi ni toleo la Ukristo-Uyahudi ambalo hufasiri upya vifungu muhimu vya Maandiko kwa nji ambayo inafanya matendo kuwa muhimu kufika mbinguni. Othodoksi inafundisha kwamba imani katika Yesu ni muhimu kwa wokovu, lakini ambapo Ukristo unafundisha kwamba kuwa zaidi kama Kristo ni matokeo ya ushawishi wa Kristo katika maisha ya muumini, Othodoksi inafundisha kwamba ni sehemu ya mchakato wa wokovu. Ikiwa mchakato huo (ni ule wa kufanyika kuwa Mungu) haufanyiki ipasavyo, mwabudu anaweza kupoteza wokovu wake. Baada ya kifo, wacha Mungu wanaishi katika hali ya kati ambapo hali ya kufanyika Mungu inaweza kukamilika. Wale ambao wana imani lakini hawakutimiza maendeleo ya kutosha katika kufanyika kama Mungu wanapelekwa kwenye “hali mbaya” ya muda na wataenda kuzimu isipokuwa wacha Mungu walio hai waombe na kukamilisha matendo ya rehema kwa niaba yao. Baada ya hukumu ya mwisho, wacha Mungu wanatumwa mbinguni na wengine kuzimu. Mbinguni na kuzimu si mahali, bali ni miitikio ya kuwa katika uwepo wa Mungu, kwani hakuna mahali popote ambapo Yeye hayupo. Kwa wafuasi wa Kristo, uwepo wa Mungu ni paradiso, lakini kwa wale ambao hawajaokolewa, kuwa na Mungu ni mateso ya milele.
Uhindu: Uhindu ni sawa na Ubuddha kwa kiwango fulani. Wokovu (au moksha) hufikiwa wakati mwabudu anapowekwa huru kutokana na mzunguko wa kuzaliwa upya katika umbo jingine, na roho yake inakuwa moja na Mungu. Mtu huwa huru kwa kujiondolea karma mbaya-athari ya kitendo kiovu au nia mbaya. Hili linaweza kufanywa kwa njia tatu tofauti: kwa kujitolea bila ubinafsi na kumtumikia mungu fulani, kupitia kuelewa asili ya ulimwengu, au kwa kufahamu vitendo vinavyohitajika ili kuridhisha miungu kikamilifu.
Katika Uhindu, wenye zaidi ya miungu milioni moja tofauti, kuna maoni tofauti kuhusu asili ya wokovu. Shule ya Advaita inafundisha wokovu hutokea wakati mtu anaweza kuvua nafsi ya uwongo na kuifanya nafsi isiyotofautishwa na ile ya mungu. Mwenye uwili anasisitiza kwamba nafsi ya mtu daima huhifadhi utambulisho wake hata kama inavyounganishwa na mungu.
Uislamu: Uislamu ni kupaa kwa Mungu wa Kikristo/Uyahudi. Waislamu wanaamini wokovu huja kwa wale wanaomtii Mwenyezi Mungu vya kutosha kwamba matendo mema ni makubwa kuliko mabaya. Waislamu wanatumai kwamba kurudia yale aliyofanya na kusema Muhammad itatosha kufika mbinguni, lakini pia wanasoma sala za ziada, kufunga, kwenda kuhiji, na kufanya kazi nzuri kwa matumaini ya kupunguza uzito. Kuuawa kishahidi katika kumtumikia Mwenyezi Mungu ndiyo kazi pekee iliyohakikishwa ya kumpeleka mwabudu peponi.
Ujaini: Ujaini ulitokea kule India karibu wakati uleule na Uhindu na unafanana sana. Mtu lazima ashike imani sahihi, awe na maarifa sahihi, na atende kwa njia sahihi. Ni hapo tu ndio roho inaweza kusafishwa kutoka kwa karma. Lakini katika Ujaini hakuna muumba. Hakuna mungu wa juu zaidi wa kufikia au kukopesha misaada. Wokovu ni mwanadamu kama mtawala wa hatima yake mwenyewe, aliyekombolewa na mkamilifu, aliyejawa na utambuzi usio na kikomo, ujuzi, raha, na nguvu.
Mashahidi wa Yehova: Mafundisho ya Jumuiya ya Mnara wa Mlinzi yanatuongoza kuainisha Mashahidi wa Yehova kama dhehebu la Ukristo ambalo hutafsiri vibaya kitabu cha Ufunuo. Sawa na wa Wamomoni, Mashahidi wa Yehova hufundisha viwango tofauti vya mbinguni. Watiwa-mafuta ni 144,000 wanaopokea wokovu kwa damu ya Kristo na watatawala pamoja Naye katika paradiso. Wao ni bibi-arusi wa Kristo. Kwa wengine wote, dhabihu ya Yesu iliwaweka huru tu kutoka kwa laana ya Adamu ya dhambi ya asili, na “imani” ni fursa tu ya kupata njia yao ya kwenda mbinguni. Ni lazima wajifunze juu ya historia ya Ufalme, washike sheria za Yehova, na wawe washikamanifu kwa “serikali ya Mungu” -wale viongozi 144,000, ambao 9,000 kati yao wako duniani sasa. Ni lazima pia waeneze habari za Ufalme, kutia ndani kugeuza imani nyumba kwa nyumba. Baada ya kifo, watafufuliwa wakati wa ufalme wa milenia ambapo lazima waendelee na maisha ya utauwa. Ni baada tu yah apo ndipo wanapewa fursa ya kumkubali Kristo rasmi na kuishi milele chini ya utawala wa wale 144,000.
Uyahudi: Wayahudi wanaamini kwamba, mtu binafsi au kama taifa, wanaweza kupatanishwa na Mungu. Ijapokuwa dhambi (za mtu binafsi au taifa) wanaweza kupoteza wokovu wao, lakini vile vile wanaweza kuupata kupitia toba, matendo mema, na maisha ya kujitolea.
Umomoni: Wamomoni wanaamini kuwa dini yao imetokana na Uyahudi/Ukristo, lakini kutegemea kwao kazi za ziada kunapinga hili. Pia wana mtazamo tofauti wa mbinguni. Ili kufika mbingu ya pili chini ya “wokovu wa jumla,” mtu lazima amkubali Kristo (ama katika maisha haya au yajayo) na abatizwe au abatizwe kwa wakala kupitia jamaa aliye hai. Ili kufikia mbingu ya juu kabisa, ni lazima mtu aamini katika Mungu na Yesu, atubu dhambi, abatizwe kanisani, awe mshiriki wa kanisa la LDS, apokee Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono, kutii Momoni “Neno la Hekima.” Na amri zote za Mungu, na kukamilisha taratibu fulani za hekalu ikiwa ni pamoja na ndoa. Na “wokovu huu wa mtu binafsi” huongoza kwa mwabudu na mwenzi wake kuwa miungu na kuzaa watoto wa kiroho ambao hurudi Duniani wakiwa nafsi za walio hai.
Ukatoliki wa Kirumu: wakatoliki wa Kirumi hapo awali waliamini kuwa wale pekee walio katika Kanisa la Kitoliki la Kirumi ndio wangeweza kuokolewa. Kujiunga na kanisa ilikuwa mchakato mrefu wa madarasa, matambiko, na ubatizo. Watu ambao tayari walikuwa wamebatizwa lakini hawakuwa washiriki wa Kanisa Katoliki la Rumi walikuwa na matakwa tofauti na huenda hata tayari walionekana kuwa Wakristo. Ubatizo unahitajika “kawaida” kwa wokovu, lakini hii inaweza kujumuisha “ubatizo wa nia” (kutaka kubatizwa kwa vyovyote vile). Kutokana na mwongozo (katekisimu): “Wale wanaoifia imani, wakatekumeni, na wale wote ambao, pasipo kujua juu ya Kanisa, bali wanatenda chini ya maongozi ya neema, wanamtafuta Mungu kwa uaminifu na kujitahidi kutimiza mapenzi yake, wanaokolewa hata kama hawajabatizwa.” Licha ya mabadiliko katika miaka mingi, ubatizo (au tamaa ya ubatizo) bado huitajika kwa wokovu.
Kulingana na Ukatoliki, baada ya kifo, roho za wale waliomkataa Kristo hupelekwa kuzimu. Roho za wale waliomkubali Kristo na kufanya matendo ya kutosha ili kutakaswa dhambi huenda mbinguni. Wale waliokufa kwa imani lakini hawakukamilisha hatua za kutakaswa wanapelekwa toharani ambako wanapitia adhabu ya muda, yenye uchungu hadi roho zao zisafishwe. Utakaso kwa mateso unaweza kupunguzwa kwa kuteseka maishani na matoleo na sala za wengine kwa niaba ya mwenye dhambi. Baada ya utakaso kukamilika, roho inazweza kwenda mbinguni.
Usayansi: Usayansi ni sawa na dini za Mashariki kwa kuwa wokovu hupatikana kupitia ujuzi wa nafsi na ulimwengu. “thetan” (jibu la kisayansi kwa nafsi) husafiri kupitia maisha kadhaa tofauti, akijaribu kufukuza picha zenye uchungu na za kutisha ambazo husababisha mtu kutenda kwa hofu na bila hekima. Mara baada ya Mwanasayansi “kuondolewa” kwa picha hizi hatari na kuwa “thetan ya uendeshaji,” unaweza kudhibiti mawazo, maisha, suala, nishati, nafsi na wakati.
Shinto: Maisha ya baada ya kifo katika Shinto hapo awali yalikuwa ulimwengu wa kutisha, unaofanana na Kuzimu. Mambo ya maisha ya baadaye sasa yamehamishiwa kwenye Dini ya Buddha. Wokovu huu unategemea toba na kuepuka uchafu au uchafuzi wa nafsi. Kisha nafsi ya mtu inaweza kujiunga na wale mababu zake.
Kalasinga (Sikhism): Kalasinga iliundwa kwa kuguswa na mzozo kati ya Uhindu na Uislamu, na inaendeleza mvuto mwingi wa Uhindu-ingawa Masingasinga wanaamini Mungu mmoja. “Uovu” ni ubinafsi wa kibinadamu pekee. Wokovu unapatikana kwa kuishi maisha ya uaminifu na kumtafakari mungu. Ikiwa matendo mema yanafanywa vya kutosha, mwabudu anaachiliwa kutoka kwa mzunguko wa kuzaliwa upya na kuwa pamona na mungu.
Utao: Sawa na dini nyingine nyingi za Mashariki (Shinto dini za watu wa Kichina, Sihkism), Dini ya Tao ilikubali kanuni zake nyingi za maisha ya baada ya kifo kutoka kwa Ubuddha. Hapo awali, Watao hawakujishughulisha na wasiwasi wa maisha ya baada ya kifo na badala yake, walijikita katika kuunda jamii ya ndoto. Wokovu ulifikiwa kwa kupatana na ulimwengu na kupokea usaidizi kutoka kwa watu wasioweza kufa wa kimbinguni ambao waliishi milimani, visiwa na maeneo mengine duniani. Tokeo likawa kutokufa. Hatimaye, Watao waliacha jitihada ya kutoweza kufa na kuchukua mafundisho ya baada ya kifo ya Dini ya Buddha.
Ungamano-watu wote (Unitarian-Universalism: Wayuniteria wanaruhusiwa na kutiwa moyo kuamini chochote wanachopenda kuhusu maisha ya baada ya kifo na jinsi ya kufika huko. Ingawa, kwa jumla, wanaamini kwamba watu wanapaswa kutafuta nuru katika maisha haya na wasiwe na wasiwasi sana kuhusu maisha ya baadaye.
Wicca: Waumini wa Wicca wanaamini mambo mengi tofauti kuhusu maisha y baada ya kifo, lakini wengi wanaonekana kukubaliana kwamba hakuna haja ya wokovu. Watu huishi kupatana na mungu wa kike kwa kutunza udhihirisho wake wa kimwili-duniani-au hawafanyi hivyo, na karma yao mbaya inarudishwa kwao mara tatu. Wengine huamini kwamba nafsi huzaliwa upya hadi wajifunze masomo yao yote ya maisha na kuwa kitu kimoja na mungu huyo wa kike. Wengine wamejitolea sana kufuata njia ya mtu binafsi hizi kwamba wanaamini watu binafsi huamua kitakachotokea watakapokufa; ikiwa waabudu wanafikiri kuwa watazaliwa upya au watapelekwa kuzimu au kuunganishwa na mungu wa kike ambaye watakuwa. Wengine wanakataa kabisa kutafakari maisha ya baada ya kifo. Kwa vyovyote vile, hawaamini katika dhambi au kitu chochote wanachohitaji kuokolewa nacho.
Uzorotalia (Zoroastrianism): Uzorotalia unaweza kuwa dini ya kwanza ambayo ilisema kwamba maisha ya baada ya kifo yanategemea matendo ya mtu maishani. Hakuna kuzaliwa upya, hukumu rahisi siku nne baada ya kifo. Baada ya muda wa kutosha kuzimuni, hata hivyo wale ambao walihukumiwa wanaweza kwenda mbinguni. Ili kuhukumiwa kwa haki, mtu anaweza kutumia ujuzi au kujitolea, lakini njia yenye ufanisi zaidi ni kupitia matendo.
Unataka kujifunza kweli kuhusu jinsi ya kufika mbinguni? Angalia Makala yetu “Kwenda Mbinguni-Ninawezaje kujiahakikishia hatima ya milele?
English
Jinsi ya kufika mbinguni-Je! kuna maoni gani kutoka kwa dini tofauti?