settings icon
share icon
Swali

Je, nawezaje kujua bila shaka kuwa nitafika Mbinguni pale nitakapo fariki?

Jibu


Je, utajuaje kwa uhakika kama una uzima wa milele na kwamba utafika Mbinguni pale utakapofariki? Mungu anataka uwe na uhakika! Bibilia yasema: “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la mwana wa Mungu” (1 Yohana 5:13, TMP). Kwa mfano; ikatokea umesimama mbele za Mungu saa hii na akuulize, ‘Kwanini nikuruhusu uingie Mbinguni?’ Je, ungemjibu nini? Unaweza usijue utajibu nini. Unachohitaji kujua ni kwamba Mungu anatupenda na ameshaweka njia inayotuwezesha kujua kwa uhakika mahali tutakapoishi milele. Bibilia inasema hivi “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16, TMP).

Lakini kabla ya hilo, ni sharti tuelewe shida ambayo inatupinga kufika Mbinguni. Nayo ni hii – asili yetu ya dhambi inatupinga kuwa na uhusiano na Mungu. Sisi ni wenye dhambi kwa asili na kwa kuchagua. “Kwasababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23, TMP). Hatuwezi kujiokoa sisi wenyewe. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu awaye yote asije akajisifu.” (Waefeso 2:8-9, KCV). Tunastahili mauti na jehanamu. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23, TMP).

Mungu ni mtakatifu na mwenye haki hivyo ni lazima aadhibu dhambi, lakini pia, Ye atupenda na ameweka njia ili tupate msamaha wa dhambi zetu. Yesu alisema: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi’’ (Yohana 14:6, TMP). Yesu alitufia pale msalabani “Kwa maana Kristo naye alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu’’ (1 Petro 3:18, TMP). Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu nakufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki” (Warumi 4:25, TMP).

Sasa turudi kwenye swali letu – “Nawezaje kujua bila shaka kuwa nitafika Mbinguni pale nitakapo fariki?’’ Jawabu ni hili – ‘Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka’ (Matendo 16:31, TMP). Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12, TMP). Unaweza kupokea uzima wa milele kama ZAWADI ya bure. “zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu’’ (Warumi 6:23b, BHN). Unaweza kuishi maisha yenye ukamilifu na yenye maana kuanzia sasa. Yesu alisema: “mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10, TMP). Wewe pia waweza kuishi milele na Yesu Mbinguni, kwani alisha ahidi: “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” (Yohana 14:3, TMP).

Ukiwa unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na upokee msamaha wa dhambi toka kwa Mungu, hapa kunalo ombi unaweza kuomba. kusema ombi hili au ombi lingine lolote lile halitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kupeana kwa ajili ya msamaha wako. “Mungu, najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo ameichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu, na msamaha - zawadi ya uzima wa milele! Amina!"

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nawezaje kujua bila shaka kuwa nitafika Mbinguni pale nitakapo fariki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries