settings icon
share icon
Swali

Mafundisho kuhusu neema ni yapi?

Jibu


Kifungu “mafundisho kuhusu neema” kinatumika kama neno mbadala kwa neno “Ukalvini,” ili kuondoa tahadhari kutoka kwa John Calvin na badala yake kuzingatia jinsi hoja hizo maalum zinavyofaa kibiblia na kitheolojia. Kifungu “kanuni kuhusu neema” kinaelezea mafundisho yanahusiana na wokovu ambayo ni ya kipekee katika theolojia ya Mageuzi, ambayo ni ya Kalvin. Kanuni hizi zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo: Upotovu kamili, Uchaguzi Usio na Masharti, Upatanisho Kiwango, Neema Isiyozuuilika, na Ustahimilivu wa Watakatifu.

Wakristo waliobadilishwa wanaamini kwamba mafundisho yote matano ya neema yametolwea moja kwa moja kutoka kwa Maandiko Matakatifu na kwamba yanaeleza kwa usahihi kanuni ya Biblia kuhusu wokovu-kanuni ya wokovu. Yafuatayo ni maelezo mafupi ya kila moja yao.

Upotovu kamili- Matokeo ya kuanguka kwa Adamu, kizazi chote cha mwanadamu kiliathiriwa; uzao wote wa Adamu umekufa kiroho katika makosa na dhambi zao (Waefeso 2:1,5). Wafuasi wa Calvini kwa uepesi wanasema kuwa hii haimanishi kwamba watu ni waovu jinsi wanavyoweza kuwa. Badala yake, kanuni inasema kwamba, kwa ajili ya matokeo kuanguka kwa mwanadamu katika Adamu, watu wote wa wameharika kutoka ndani na kuharibika kwao kunaadhiri kila sehemu ya maisha yao.

Uchaguzi usio na masharti- Kwa sababu mwanadamu amekufa katika dhambi, hawezi (kwa ukaidi na kutokuwa tayari) kuanzisha itikio la wokovu kwa Mungu. Kwa mjibu wa hili, Mungu tangia kale ya milele, kwa huruma aliwachagua baadhi ya watu kwa wokovu (Waefeso 1:4-6). Watu hawa ni pamoja na wanaume na wanawake kutoka kila kabila, lugha, jamii, na taifa (Ufunuo 5:9). Uchaguzi na kuamuliwa kabla havina masharti; havitegemei mwitikio wa mwanadamu kwa neema ya Mungu (Warumi 8:29-30; Waefeso 1:11-12) kwa sababu mwanadamu, katika hali yake ya kuanguka, hawezi na hayuko tayari kuitikia ipasavyo toleo la Kristo la wokovu.

Upatanisho wa kikomo- Kusudi la kifo cha upatanisho cha Kristo halikuwa tu kuwafanya wanadamu waweze kuokolewa na hivyo kuacha wokovu wa wanadamu ukitegema mwitikio wa mwanadamu kwa neema ya Mungu. Badala yake, kusudi la upatanisho lilikuwa kupata ukombozi wa watu fulani (Waefeso 1:4-6; Yohana 17:9). Wote ambao Mungu amewachagua na Kristo aliwakufia wataokolewa (Yohana 6:37-40, 44). Wakristo wengi wa mageuzi wanapendelea neno “ukombozi mahususi” wanapohisi kuwa kifungu hiki kinaangazia kwa usahihi zaidi kiini cha fundisho hili. Sio kwamba upatanisho wa Kristo una mipaka kama vile ulivyo ule wa maalum, uliyokusudiwa watu maalum-wateule wa Mungu pekee.

Neema isiyozuilika- Mungu amewachagua watu fulani kuwa wapokeaji wa kazi ya upatanisho ya Kristo. Watu hawa wanavutwa kwa Kristo kwa neema isiyozuilika. Mungu anapoita, mwanadamu huitikia (Yohana 6:37, 44; 10:16). Fundisho hili halimaanishi kwamba Mungu anawaokoa wanadamu kinyume na mapenzi yao. Badala yake, Mungu hubadilisha moyo wa muumini mwasi ili apate nia ya kutubu na kuokolewa. Wateule wa Mungu watavutwa kwake, na neema inayowavuta kwake kwa kweli haizuiliki. Mungu huondoa moyo wa jiwe na kuweka ule moyo wa nyama (Ezekieli 36:26). Katika thoelojia ya Mageuzi, kuzaliwa upya huja kabla ya imani.

Uvumilivu wa Watakatifu- watu mahususi ambao Mungu amewachagua na kuwavuta kwake kupitia Roho Mtakatifu watadumu katika imani. Hakuna hata mmoja wa wale ambao Mungu amewachagua atakayepotea; wako salama milele ndani Yake (Yohana 10:27-29; Warumi 8:29-30; Waefeso 1:3-14). Baadhiya wanatheolojia ya Mageuzi hupenda kutumia neno “Kuhifadhiwa kwa Watakatifu” kwa kuwa wanaamini kwamba chaguo hili la maneno linaelezea kwa usahihi zaidi jinsi Mungu anavyowajibika moja kwa moja katika kuwahifadhi wateule wake. Ni wazi katika Maandiko kwamba Kristo anaendelea kuwaombea watu wake (Warumi 8:34; Waebrania 7:25). Hii inaendelea kuwapa waumini uhakikisho kwamba wale walio wa Kristo ni Wake milele.

Mafundisho haya matano kwa pamoja yanaunda mafundisho ya neema, yanaitwa hivyo kwa sababu yanafupisha tukio la wokovu kama tokeo la neema ya Mungu, ambaye anatenda bila mapenzi ya mwanadamu. Hakuna juhudi au tendo la mwanadamu linaloweza kuongeza neema ya Mungu katika kuleta ukombozi wa nafsi. Kwa maana ni kweli “mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mafundisho kuhusu neema ni yapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries