settings icon
share icon
Swali

Je! Bibilia ina kasoro, au kujipinga au kujichanganyisha?

Jibu


Ikiwa tutaisoma Bibilia kwa nia nzuri bila ya dhana ya kutafuta ukasoro wowote wa Bibilia, basi tutapata kuwa Bibilia ni kitabu kinachoweza kueleweka, na maudhui yake yanafuatana. Naam, kuna kurasa gumu kuelewa. Naam, kuna aya zinazoonekana kujichanganya. Lazima tukumbuke kwamba Bibilia iliandikwa na takribani watu 40 takribani kwa kibindi cha miaka 1500. Kila mwandishi ako na njia yake ya uandishi tofauti, kutoka kwa mtazamo tofauti, akiandikia kikundi tofauti, kwa lengo tofauti. Lazima tutarajie tofauti kidogo sana. Ingawa tofauti si mgongano. Itakuwa kasoro tu pekee kama hakuna njia yoyote aya au ukurasa zaweza kuletwa pamoja. Ingawa jibu halipatikani sasa hivi, hiyo haimanishi kuwa hakuna jibu kabisa. Wengi wamepata kasoro ya kudhania katika Bibilia inayo husu historia au chiografia, baadaye wapata kuwa iko sawa, wakati sehumu/vipande vinapopatikana, kwa mfano yale mawe ya kuchonga amri kumi ziliandikwa thibitisho la ukweli la patikana.

Kila mara twapokea maswali yanakaribiana na “Eleza/fafanua vilie hizi aya hazigongani” au “Angalia hapa kuna kasoro ya Bibilia” kwa kukubali baadhi ya mambo haya watu wayawazilisha ni magumu kuyajibu. Ingawa, ni amini yetu kuwa kuna majibu ya kuaminika kwa maswali yoyote ya aya za Bibilia kuihitilafiana au kasoro yoyte. Kuna vitabu na mitandao ambayo imeratibisha chini “zile kasoro ziko kwa Bibilia.” Watu wengi wanapata silaha zao (vilipuaji) kutoka sehemu hizi; hawawezi kupata kasoro yoyote wao wenyewe. Pia vitabu na mitandao amabayo inapinga au mtu yeyote mwenye aliye na kasoro yoyote kuhusu Bibilia. Cha kushangaza ni kwamba watu wanayoipinga Bibilia si kwamba wako na nia ya kutafuta jibu. Wengi “wapinga Bibilia” wanajua majibu vizuri sana, ni ile tu wanaendeleza pingamishi hafivu za zamani kuipinga Bibilia tena.

Tunastahili kufanya nini wakati mtu anapotujia na dhana kuwa Bibilia ina kasoro? 1) Kwa kuomba na kusali isome Bibilia na uone kama kuna suluhisho lolote. 2) Fanya utafiti ukitumia vitabu vinavyo elezea mengi kuhusu Bibilia (Commentaries) vitabu vinavyoitetea Bibilia, na mitandao ya Kibibilia. 3) Muuliize mchungaji/kiongozi yeyote wa kanisa lako uone kama wanaweza kuwa na suluhisho. 4) Kama hakuna jibu la kuridhisha baada ya hatua ya 1, 2 na 3 zimefuatwa, tunamwamini Mungu kuwa neno lake ni kweli na kuna suluhisho ambalo bado halijagunduliwa (2 Timotheo 2:15, 3:16-17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Bibilia ina kasoro, au kujipinga au kujichanganyisha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries