settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana kifungu Filioque?

Jibu


Kifungu cha Filioque kilikuwa, na bado ni cha utata katika kanisa kuhusiana na Roho Mtakatifu. Swali ni, " Ni kutoka kwa nani Roho Mtakatifu hutoka, ni Baba, au Baba na Mwana? " Neno Filioque lina maana ya "na mwana" katika Kilatini. Linajulikana kwetu kama " kifungu Filioque" kwa sababu maneno "mwana" kiliongezwa kwa kile kifungu cha imani cha Nicene, kikionyesha kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba "na mwana." Kulikuwa na ubishi sana juu ya suala hili kwamba hatimaye ilisababisha mgawanyiko kati ya makanisa ya Katoliki na Mashariki Orthodox katika mwaka wa AD 1054. Ni Makanisa mawili tu bado yanakubaliana juu ya kifungu cha Filioque .

Yohana 14:26 inatuambia, "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu ..." Yohana 15:26 inatuambia, "Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi." Angalia pia Yohana 14:16 na Wafilipi 1:19. Maandiko haya yanaonekana kuonyesha kuwa Roho anaonekana kutumwa na Baba na Mwana. Jambo muhimu katika kifungu Filioque ni shauku ili kuulinda uungu wa Roho Mtakatifu. Biblia inafundisha wazi kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu (Matendo 5:3-4). Wale wanaopinga kifungu cha Filioque hupinga kwa sababu wanaamini Roho Mtakatifu hutoka kwa Baba na Mwana hufanya Roho Mtakatifu "kuwa tiivu" kwa Baba na Mwana. Wale ambao hutekeleza kifungu cha Filioque huamini kwamba Roho Mtakatifu hutoka kwa Baba na Mwana haina athari kwa Roho kuwa sawa kwa wote Mungu Baba na Mwana.

Utata wa kifungu cha Filioque hasa uhusisha nyanja ya mtu wa Mungu kwamba sisi kamwe hatuwezi kufahamu kikamilifu. Mungu, ambaye asiye na mipaka, hatimaye hawezi fikirika katika akili zetu binadamu silizo na mwisho. Roho Mtakatifu ni Mungu, na Yeye alitumwa na Mungu kama "badala ya" Yesu Kristo hapa duniani. Swali kuwa Roho Mtakatifu alitumwa na Baba, au kwa Baba na Mwana, hakiwezi amuliwa, wala hakina haja kabisa ya kuwaamuliwa. Kifungu cha Filioque labda kitabaki kuwa cha utata.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana kifungu Filioque?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries