settings icon
share icon

Kitabu cha Mwanzo

Mwandishi: Mwandishi wa Kitabu cha Mwanzo hatambuliki.Kitamaduni, mwandishi anakisiwa kuwa Musa. Hakuna sababu adilifu ya kukana uandishi wa Musa kitabu cha Mwanzo kisheria.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha Mwanzo hakitaji wakati kilipoandikwa. Tarehe ya uandishi inawezekana kuwa kati ya 1440 na 1400 KK, kati ya wakati Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri na kifo chake.

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Mwanzo mara nyingine kimeitwa "mbegu-njama" ya Biblia nzima. Mafundisho mengi makuu katika Biblia yameazishwa kwa utaratibu wa "mbegu" katika kitabu cha Mwanzo. Pamoja na kuanguka kwa mwanadamu, ahadi ya Mungu ya wokovu au ukombozi umenakiliwa (Mwanzo 3:15). Mafundisho ya uumbaji, kushutumiwa kwa dhambi, kuhesabiwa haki, upatanisho, upotovu, ghadhabu, neema, uhuru, uwajibikaji, na mengine mengi yote yamezungumziwa katika hiki kitabu cha asili kiitwacho Mwanzo.

Maswali mengi mazito kuhusu maisha yamejibiwa katika Mwanzo. (1) Mimi nilitoka wapi? (Mungu alituumba sisi - Mwanzo 1: 1) (2) Kwa nini niko hapa? (Tuko hapa kuwa na uhusiano na Mungu - Mwanzo 15: 6) (3) Ninaenda wapi? (Tuna makusudio baada ya kifo - Mwanzo 25: 8). Mwanzo unawasihi wanasayansi,mwanahistoria, mwanateolojia, mama mfanyikazi wa nyumbani, mkulima, msafiri, na mwanamume au mwanamke wa Mungu. Ni mwanzo unaofaa kwa ajili ya hadithi ya Mungu ya mpango wake kwa wanadamu, Biblia.

Mistari muhimu: Mwanzo 1: 1, "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Mwanzo 3:15, "Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino."

Mwanzo 12: 2-3, "Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa ".

Mwanzo 50:20, "Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo."

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Mwanzo kinaweza kugawanywa katika sehemu mbili: Historia ya kale na Historia ya kimwanaume. Historia ya kale inanakili (1) Uumbaji (Mwanzo sura ya 1-2); (2) Anguko la mwanadamu (Mwanzo sura ya 3-5), (3) mafuriko (Mwanzo sura ya 6-9), na (4) utawanyiko (Mwanzo sura 10-11). Historia ya kimwanaume inanakili maisha ya watu wanne wakubwa: (1) Ibrahimu (Mwanzo 12-25: 8); (2) Isaka (Mwanzo 21: 1-35-29); (3) Yakobo (Mwanzo 25: 21-50: 14); na (4) Yusufu (Mwanzo 30: 22-50: 26).

Mungu aliumba ulimwengu ambao ulikuwa nzuri na huru kutokana na dhambi. Mungu aliumba binadamu ili awe na uhusiano wa kibinafsi naye. Adamu na Hawa walitenda dhambi na hivyo wakaleta maovu na kifo ulimwenguni. Maovu yakaongezeka kwa kasi katika ulimwengu mpaka kulikuwa na familia moja tu ambayo Mungu hakupa kitu chochote nzuri. Mungu alituma mafuriko kuyafuta maovu, bali alimwookoa Nuhu na familia yake pamoja na wanyama katika safina. Baada ya mafuriko, binadamu wakaanza tena kuzaana na kuenea duniani kote.

Mungu alimchagua Ibrahimu, ambaye kupitia kwake Yeye angeumba watu waliochaguliwa na hatimaye Masihi aliyeahidiwa. Kizazi kilichochaguliwa kilipitishwa kwa mwana wa Ibrahimu Isaka, na kisha kwa mwana wa Isaka, Yakobo. Mungu alibadili jina la Yakobo kuwa Israeli, na wanawe kumi na wawili wakawa mababu wa makabila kumi na mawili ya Israeli. Katika uhuru wake, Mungu alifanya mwana wa Yakobo Yusufu kupelekwa Misri kwa matendo ya kudharauliwa ya ndugu zake Yusufu. Hili tendo, lengo lake lilikuwa uovu kutoka kwa nduguze, lilikuwa na lengo nzuri kwake Mungu na hatimaye lilisababisha Yakobo na familia yake kuokolewa kutokana na njaa na Yusufu, ambaye alikuwa na mamlaka ya juu zaidi katika Misri.

Ishara: Dhamira nyingi za agano jipya zina mizizi yao katika Mwanzo. Yesu Kristo ni mbegu ya mwanamke ambaye ataharibu nguvu za shetani (Mwa 3:15). Kama ilivyo na Yusufu, mpango wa Mungu kwa ajili ya mema ya watu kwa njia ya dhabihu ya Mwana wake ilikuwa na lengo nzuri, hata kama wale ambao walimsulubisha Yesu walikuwa na lengo la mbaya. Nuhu na familia yake ndio wa kwanza waliobaki kati ya wengi walioangaziwa katika Biblia. Licha ya shida na hali ngumu, Mungu daima hulinda anayebaki mwaaminifu kwa ajili yake. Wanaisraeli waliosalia wakarudi Yerusalemu baada ya utumwa wa Babeli, Mungu akahifadhi waaminifu wake kupitia mateso yote yalivyoelezwa katika Isaya na Yeremia, waumini wa makuhani 7000 walifichwa dhidi ya ghadhabu ya Yezebeli, Mungu anaahidi kwamba waumini wa Wayahudi siku moja watakumbana na Masihi wao wa kweli (Warumi 11). Imani iliyoonyeshwa na Ibrahimu itakuwa ni zawadi ya Mungu na msingi wa wokovu kwa Wayahudi na Mataifa yote. (Waefeso 2: 8-9; Waebrania 11).

Vitendo tekelezi: Dhamira ya maana ya Mwanzo ni kuwepo milele kwa Mungu na viumbe vyake vya dunia. Hakuna juhudi katika sehemu ya mwandishi kutetea kuwepo kwa Mungu; yeye tu anasema kwamba Mungu yupo, daima alikuwa, na daima atakuwa, Mwenyezi juu ya yote. Kwa njia hiyo hiyo, tuna imani katika ukweli wa Mwanzo, licha ya madai ya wale ambao watakataa. Watu wote, bila kujali utamaduni, utaifa au lugha, wanawajibika kwa Muumba. Lakini kwa sababu ya dhambi, iliyoletwa duniani katika Kuanguka, tumetengwa naye. Lakini kupitia taifa moja ndogo, Israeli, mpango wa ukombozi wa Mungu kwa wanadamu umeonyeshwa na kufanywa kupatikana kwa wote. Tunafurahi katika mpango huo.

Mungu aliumba ulimwengu, dunia, na kila kiumbe kilicho hai. Tunaweza kumwamini Yeye kushughulikia maitaji katika maisha yetu. Mungu anaweza kuchukua hali ya kukata tamaa, kwa mfano, Ibrahimu na Sara kukosa mtoto, na kufanya mambo ya ajabu kama sisi tutamwamini kwa urahisi na kutii. Mambo ya kutisha na yasiyo ya haki yanaweza kutokea katika maisha yetu, kama vile kwa Yusufu, lakini Mungu daima ataleta manufaa zaidi kama tutakuwa na imani kwake Yeye, na mpango wake huru. "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake." (Warumi 8:28).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Mwanzo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries