settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kwamba kitanda cha ndoa hakinajisiwe (Waebrania 13:4)?

Jibu


Sura ya 13 ni sura ya mwisho ya kitabu cha Waebrania na inaishia na mfululizo wa mawaidha ya mwisho kwa Wakristo. Mstari wa 4 unasema, “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.” Neno la Kigriki linalotafsiriwa “kutotiwa unajisi” limetumiwa tu katika namna hii hasa mara nne katika Agano Jipya, na linamaanisha “kutochafuliwa” au “kutengwa.” Waebrania 7:26 inatumia neno hili kumwelezea Yesu Kristo, kuhani wetu mkuu, na Yakobo 1:27 inasema kwamba dini “iliyo safi” ni ile inayosaidia wajane na yatima na kubaki bila mawaa na ulimwengu.

Kitanda cha ndoa kinapaswa kuwekwa safi au bila unajisi. Kwa maneno mengine, uhusiano wa kimapenzi unaoshirikiwa kati ya mume na mke unapaswa kutengwa kwa ajili ya wanandoa hao peke yao. Mungu aliumba muungano wa kijinsia kuwa kati ya mume na mke. Pekee yao. Hakuna matumizi mengine ya kujamiiana yanayokubaliwa katika Maandiko. Kunajisi au kutumia vibaya zawadi ya Mungu ya ngono ni kuchafua kitanda cha ndoa.

Kitanda cha ndoa kinaweza kuchafuliwa kwa njia kadhaa:

1. Uasherati. Watu wawili ambao hawajafunga ndoa wanapofanya ngono, wanachafua zawadi nzuri ya Mungu ya ngono. Wale ambao hawajaapa wenyewe kwa wenyewe katika muungano wa kudumu wa maisha hawana haki ya kutumia kilele cha nadhiri kama hiyo. Ngono iliundwa kuwa tendo la mwisho la kuwekwa wakfu wakati wanandoa wanapoahidiana maisha yao katika agano takatifu. Aina zote za kujamiiana nje ya muungano wa ndoa zinaleta aibu kwa taasisi yenye heshima ya ndoa (1 Wakorintho 6:18)

2. Uzinzi. Wakati mmoja au wote wawili wanahusika katika kingono na ile hali wameoleka kwa mtu mwingine, Mungu huita matendo yao ya ngono uzinzi. Uzinzi ulikuwa na adhabu ya kifo chini ya Agano la Kale la Mungu na Israeli (kumbukumbu 22:22; Walawi 20:10). Ingawa hatuishi tena chini ya agano hilo, uzinzi bado uko juu katika orodha ya maovu ya Mungu ya kiadili (Mathayo 5:28, 32) na kila mara inatajwa kuwa ni dhambi inayowazuia wahusika wasiotubu kuurithi ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:19; 1 Wakorintho 6:9).

3. Ushoga. Uchafu mwingine wa kitanda cha ndoa ni upotovu wa wanaume kufanya mapenzi na wanaume au wanawake na wanawake. Licha ya ulimwengu wetu wa sasa kukumbatia zoezi la ushoga, kitendo hiki kiovu hakijawahi na hakitawahi idhinishwa au kubarikiwa na Mungu. Ushoga ni upotoshaji wa zawadi ya Mungu ya umoja wa kimwili kati ya mume na mke na ndiyo shughuli pekee ya ngono inayoitwa chukizo (Walawi 20:13). Marufuku dhidi ya ushoga yanabeba haki hizo hizo kwa Agano Jipya, kama zilivyoorodheshwa pamoja na dhambi zile zinazowaweka wasiotubu nje ya ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9; 1 Timotheo 1:9-10; Yuda 1:7).

4. Ukahaba. Mithali 7 inatoa maelezo ya kina juu ya uharibifu unaokuja juu ya kijana anayejirihusu kushawishiwa na kahaba. Dhambi ya ukahaba mara nyingi hutumika kama sitiari kwa Israeli wasio waaminifu (Hosea 4:15; Yeremia 3:8; Waamuzi 8:33). Wakristo wanaonywa kuepuka uasherati huo kwa sababu ya utakatifu wa kitanda cha ndoa (1 Wakorintho 6:15-16; Waefeso 5:3).

5. Ponografia. Kutumia ponofrafia ili kujiridhisha kingono ni njia ya kisasa zaidi ya kuchafua kitanda cha ndoa. Vitabu vya ponografia, video, kutuma ujumbe mfupi wa ngono, na utumizi wa nyenzo nyinginezo za ngono waziwazi pia huchafua utakatifu wa muungano wa kingono kati ya mwanamme na mke. Ponografia ina athari ya kuleta wageni ndani ya chumba cha kulala, hata kama ni kupitia kwa macho tu. Yesu alionya kwamba tamaa inayohusishwa na kumtazama mwanamke ni sawa na uzinzi mbele za Mungu (Mathayo 5:28). Ponografia imechochea tamaa ya ngono hadi kiwango inakua sanaa, lakini bado inaharibu moyo na unajisi wenye dhambi wa tendo la ngono.

Mungu aliwaumba wanadamu kuwa safi mwili na roho. Muungano wa kijinsia kati ya mume na mke ulikuwa sehemu ya usafi huo (Mwanzo 2:24-25). Adamu na Hawa walipofanya dhambi, ngono ilichafuliwa pamoja na kila kitu kingine. Yesu alinunua uwezo wa kuridhisha usafi huo kupitia kifo chake cha dhabihu msalabani (2 Wakorintho 5:21). Hakuna dhambi, ikiwa ni pamoja na uasherati, ambayo ni kubwa mno kwa uwezo wa kifo hicho cha upatanisho na ufufuo kusamehewa. Ingawa tunaweza kuwa tumenajisi kitanda cha ndoa kwa njia nyingi, Mungu anaweza kurejesha usafi wa kijinsia na utakatifu tunapotubu na kuweka maisha yetu kumfuata Yeye (Zaburi 51:7; 1 Yohana 1:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kwamba kitanda cha ndoa hakinajisiwe (Waebrania 13:4)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries