Swali
Je! Neno Kristo inamaanisha nini?
Jibu
Mshangao kwa baadhi, "Kristo" sio jina la mwisho la Yesu (jina la ukoo). "Kristo" linatoka kwa neno la Kigiriki Kristos, maana yake "mtiwa Mafuta" au "aliyetiwa wakfu." Hili ndilo neno la Kigiriki linalofanana na neno la Kiebrania Mashiak, au "Masihi." Yesu ni jina la kiwanadamu la Bwana alilopewa na Mariamu na malaika Gabrieli (Luka 1:31). "Kristo" ni jina lake la cheo, likiashiria kuwa Yesu alitumwa kutoka kwa Mungu kuwa Mfalme na Mkombozi (ona Danieli 9:25; Isaya 32:1). "Yesu Kristo" linamaanisha "Yesu Masihi" au "Yesu Mtiwa Mafuta."
Katika Israeli ya kale, wakati mtu alipewa nafsi ya mamlaka, Mafuta yalimiminwa kichwani mwake ishara kuwa ametiwa wakfu kwa kazi ya Mungu (mfano, 1Samueli 10:1). Wafalme, makuhani, na manabii walitiwa wakfu namna hiyo. Kutiwa Mafuta ilikuwa tendo la ishara kuonyesha chaguo la Mungu (mfano 1 Samueli 24:6). Ijapokuwa maana ya kihalisia la kutiwa Mafuta linarejelea kule kupaka mafuta, pia linaweza rejelea kutiwa wakfu na Mungu, hata kama mafuta hayatumiki hasa (Waebrania 1:9).
Kunayo mamia ya vifungu vya kinabii katika Agano la Kale ambavyo vinalenga kukuja kwa Masihi ambaye atakomboa watu Wake (mfano Isaya 61:1; Danieli 9:26). Israeli ya kale ilidhani Masihi wao angekuja na nguvu za kijeshi ili kuwaokoa kutoka utumwa wa miongo mingi na wafalme wa dunia hii na mataifa kafiri. Lakini Agano Jipya linaonyesha ukombozi bora zaidi anaoutoa Kristo Masihi-ukombozi kutoka kwa nguvu na adhabu ya dhambi (Luka 4:18; Warumi 6:23).
Biblia inasema kuwa Yesu alitiwa wakfu kwa mafuta katika matukio mawili tofauti na wanawake wawili tofauti (Mathayo 26:6-7; Luka 7:37-38), lakini wakfu muhimu ulikuja wa Roho Mtakatifu (Matendo 10:38). "Kristo" kuwa jina la Yesu inamaanisha Yeye ndiye mtiwa Mafuta wa Mungu, yule mmoja aliyetimiza nabii za Agano la Kale, Mwokozi mteule ambaye alikuja kukomboa wenye dhambi (1 Timothy 1:15), na Mfalme wa wafalme ambaye atarudi tena kuanzisha Ufalme wake duniani (Zekaria 14:9).
English
Je! Neno Kristo inamaanisha nini?