settings icon
share icon
Swali

Kusudi la utawala wa Kristo kwa miaka elfu ni gani?

Jibu


Milenia (ambayo pia huitwa ufalme wa milenia) ndio utawala wa Kristo wa miaka 1,000 baada ya dhiki na kabla ya kila mtu wa ulimwengu kupelekwa mbinguni au jehanamu. Yesu atatawala kama mfalme wa Israeli na kwa mataifa yote ya ulimwengu (Isaya 2:4;42:1). Ulimwengu utaishi na amani (Isaya 11:6-9;32:18), na shetani atafungwa (Ufunuo 20:1-3), na katika mwanzo kila mtu atamwabudu Mungu (Isaya 2:2-3). Kusudi la utawala wa miaka elfu ni kutimiza zile ahadi ambazo Mungu alipea ulimwengu na haziwezi kutimizwa ikiwa shetani ako huru na binadamu kama ako na utawala wa kisiasa. Miongoni mwa ahadi hizi, ama agano, haswa zilipewa kwa taifa la Israeli. Na zingine zilipewa kwa Yesu, mataifa ya ulimwengu, na viumbe. Haya yote yatatimizwa kwa miaka elfu ya utawala wa Yesu.

Agano la Palestina, ambalo pia huitwa agano la ardhi ( Kumbukumbu la torati 30:1-10)
Mungu tayari ametimiza kipengele cha kibnafsi katika agano la Abrahamu; Abrahamu aliweza kuenda katika ardhi aliyopewa ahadi, akawa na kizzazi cha ukoo mwingi, na ni yeye babu wa mataifa mengi. Miaka kadhaa baada ya Abrahamu,Yoshua aliongoza Waisraeli ili kudai umiliki wa ardhi ya ahadi. Lakini Israeli haijawahi kumiliki mipaka maalum amabayo Mungu alipeana ahadi katika kitabu cha mwanzo 15:18-20 na Hesabu 34:1-12. Hata Sulemani hakuwai tawala ardhi hii maalum ( Mfalme ya kwanza 4:21-24). Hata hivyo, aliweza kutawala kutoka mto wa Misri hadi kwenye bahari kuu, lakini hakuweza kutawala eneo la mlima Hori hadi Hasarenani ( Hesabu 34:7-9)- ambayo siku hizi ni Lebanoni na Siria. Kuongezea ni kuwa, ahadi ambayo Mungu alikua amepea Abrahamu ni kuwa yeye na kizazi chake watakuwa na umiliki wa ardhi hiyo milele ( Mwanzo 13:15;17:8; Ezekia 16:60). Israeli ya sai inaweza kuwa inafuata mwelekeo huu, lakini bado hawana umiliki wa zile mipaka maalum amabazo Mungu alitaja.

Agano la Daudi ( Samueli ya pili 7)
Agano la Mungu na Daudi lilikua kwamba ukoo wa Daudi hautapotea kamwe na kuwa mrithi wa Daudi atakalia kiti cha enzi cha Israeli millele ( Samueli ya pili 7:16). Waandishi wa Kibiblia wanakubali kuwa Yesu ndiye timizo la agano hili- sababu ambayo inafanya nasaba yake kupewa baba wake wote walezi (Mathayo 1:1-17) na mamake (Luka 3:23-38). Wayahudi walielewa haya pale walipotandika matawi ya misabibu na vitambaa zao wakati Yesu alikua anaingia Yerusalemu ( Mathayo 21:1-17). Walikua wanatarajia akue kiongozi wa wanajeshi ama mwanasiasa ambaye angewaokoa kutoka kwa Warumi na kutengeneza Israeli ikue nji kuu, lakini hawakua wanaelewa kazi ya Yesu kwa kuwa nyakati zilikua za agano jipya na sio agano la Daudi. Utawala wa miaka elfu ndio mwanzo wa utawala wa Yesu wa milele kwa Israeli na dunia ( Ufunuo 20:4,6).

Agano jipya ( Yeremia 31:31-34)
Kazi ya agano jipya ( kifo na kufufuliwa kwa Yesu ) ni kupatanisha mioyo na Mungu, ambayo imetimizwa tayari, lakini bado hatujaona timizo lenyewe kwa ukamilifu. Yeremia 31:33 inasema, " Baada ya siku hizo, nitafanya agano lifuatalo na Waisraeli: Nitaiweka sheria yangu ndani yao, na kuiandika katika mioyo yao. Mimi nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Mimi Mwenyezi Mungu nimesema." Ezekieli 36:28 inaendelea kusema: " Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu." Isaya 59:20-21 inaelezea kwamba agano hili linawezekanana kwa sababu mwokozi, na patanisho ambayo anafanya itadumu milele. Agano hili halina maana kuwa kila Myahudi atapata kuokolewa, lakini lina maana kwamba Israeli kama nchi itamwabudu masihi wake. Manabii wa agano la kale ambao waliongea juu ya agano hili ikiwemo Isaya, Yeremia, Hosea na Ezekieli, wote waliandika kuwa litaweza kutimizwa baadaye. Kutoka wakati wao hadi leo, Israeli imekua nchi huru ambayo ilimwabudu masihi wake (Warumi 9-11). Watakuwa katika hizo miaka elfu za utawala wa Kristo.

Ahadi zingine
Hizi ni agano amabazo Mungu alifanya na Israeli na ambazo zitatimizwa wakati wa utawala wa Yesu wa miaka elfu, lakini Biblia pia inaelezea juu ya ahadi zingine ambazo zitatimizwa . Mungu aliahidi Yesu kwamba atafanya adui wake wawe kiti cha miguu, na wanafunzi wake watamwabudu wakiwa huru (zaburi 100). Mungu aliahidi mataifa ya ulimwengu kwamba wataishi kwa amani na Yesu kama mtawala wao (Danieli 7:11-14). Na pia aliahidi viumbe kwamba laana itaondolewa (Warumi 8:18-23), wanyama na dunia vitaweza kukombolewa kwa amani na ustawi ( Isaya 11:6-9;32:13-15), na binadamu wataokolewa kutoka kwa magonjwa (Ezekieli 34:16). Hizi pia zitataweza kutimizwa kwa miaka elfu ya utawala.

Kusudu kuu la utawala wa Yesu wa miaka elfu ni kutimiza utabiri uliopewa Israeli na ahadi ambazo zilipewa Yesu, mataifa, na dunia mzima. Agano za Mungu zilikua za kujitolea na kwa upande mmoja. Aliahidi atabariki Israeli na kupatanisha ulimwengu kwa njia maalum na hakika atatimiza.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kusudi la utawala wa Kristo kwa miaka elfu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries