Swali
Nimetenda dhambi. Je, ninahitaji kubatizwa tena?
Jibu
Swali ya iwapo mtu ambaye amekwisha tenda dhambi anafaa kubatizwa tena ni swali la kawaida. Kwanza, ni muhimu tuelewe ubatizo ni nini. Ubatizo hautuokoi wala kuosha dhambi zetu. Ubatizo ni kielelezo tu cha kile ambacho kimetokea katika maisha ya muumini anapomwamini Yesu Kristo. Ubatizo ni dhihirisho la unganiko la muumini na Kristo katika kifo, kuzikwa na kufufuka kwake. Warumi 6:3-4 inatufunza, “Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima.” Tendo la kuingia kwa maji ni taswira ya kuzikwa pamoja na Kristo. Tendo la kutoka kwa maji linadhihirisha ufufuo wa Kristo na utambulisho wetu naye tunapofufuliwa na “kuenenda katika upya wa uzima” (Warumi 6:4).
Ubatizo ni wa maaana kwa sababu ni hatua ya utii- tangazo la hadharani la imani katika Kristo na kujitolea kwake, na kujitambulisha na kifo cha Kristo, kuzikwa na ufufuo wake. Ikiwa tunamjua Yesu Kristo kama Mwokozi na kuelewa ubatizo unamaanisha nini tunapobatizwa, basi hatuhitaji kubatizwa tena. Ikiwa tulimjua Yesu kama Mwokozi lakini hatukuelewa kwa kweli maana ya ubatizo, basi labda tunahitaji kubatizwa tena. Lakini hili ni suala la dhamiri kati ya muumini na Mungu.
Ni muhimu pia kuelewa kwamba waumini wataendelea kutenda dhambi, ingawa dhambi inapaswa kuwa na mshiko mdogo sana juu yetu tunapokua katika Kristo, na matukio ya kutenda dhambi yanapaswa kuendelea kupungua katika maisha yetu yote. Tunapofanya dhambi, tunapaswa kuiungama kwa Mungu, tukimwomba atusamehe na kurejesha ushirika wetu wa karibu naye. Tunayo ahadi kwamba “Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Hakuna mahali ambapo Biblia inasema ni lazima tubatizwe tena ili tusamehewe.
English
Nimetenda dhambi. Je, ninahitaji kubatizwa tena?