Swali
Biblia inasema nini kuhusu kuchukulia kabila zingine kuwa duni kuliko yako?
Jibu
Ethnolojia ni imani kwamba kabila fulani ni bora kuliko makabila mengine yote na makabila mengine yote yanapaswa kupimwa kulingana na kabila ya mtu. Ni mfumo wa imani ambazo huongoza kwa kiburi na ukosefu wa kutowajali wengine. Kwa kuwa rangi mara nyingi ni sehemu ya kabila, mara nyingi inahusiana na ubaguzi wa rangi, ambao umekuwa janga kwa ubinadamu kwa karne nyingi. Hamna nafasi ya ukabila miongoni mwa watu wa Mungu ambayo inaelekeza katika ubaguzi wa rangi. Nia kama hiyo ni kinyume na maandiko na haimpendezi Mungu.
Kibiblia, kuchukulia kabila lako kuwa bora kuliko linguine ni dhambi. Wanaume na wanawake wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27; 9:6), ijapokuwa mfano huo umetiwa doha na dhambi. Mungu haonyeshi mapendeleo na majalio (Kumbukumbu 10:17; Matendo 10:34). Yesu hakuyatoa maisha yake kwa ajili ya jamii fulani, utamaduni, au kabila, bali kwa kifo chake “ukamnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa” (Ufunuo 5:9). Maandiko yanatuambia kwamba Yesu alikuja kuokoa ulimwengu, Wayahudi na watu wa Mataifa. Paulo analithbitsha hili kwa kusema, “Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28) na “Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote, na ndani ya wote” (Wakolosai 3:11).
Yesu alishinda vizuizi vyote vya rangi, tamaduni, na ukabila kwa kifo chake msalabani. Paulo aliandika juu ya kuunganishwa kwa Myahudi na Mmataifa katika Waefeso 2:14: “Kwa maana yeye mwenyewe ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa wawili, yaani, Wayahudi na watu wa Mataifa, tuwe wamoja kwa kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui uliokuwa kati yetu,” Ukabila uwe umetokana na chuki ya kihistoria, mawazo potovu, au majivuno ya wazi ya kibinadamu, ni kinyume kabisa na Neno la Mungu. Tumeamrishwa kupendana sisi kwa sisi kama vile Yeye alivyotupenda sisi (Yohana 13:34), na amri kama hiyo inazuia ubaguzi wowote unaotegemea rangi, kabila, au utamaduni.
English
Biblia inasema nini kuhusu kuchukulia kabila zingine kuwa duni kuliko yako?