Swali
Ni jinsi gani mimi ninaweza kuelewa kitabu cha Ufunuo?
Jibu
La muhimu katika kutafsiri Biblia, hasa kwa kitabu cha Ufunuo, ni kuwa na ufafanusi thabiti. ufafanusi ni utafiti wa kanuni za tafsiri. Kwa maneno mengine, ni njia ya kutafsiri maandiko. Ufafanusi wa kawaida au tafsiri ya kawaida ya maandiko ina maana kwamba kama mstari au kifungu kinaonyesha wazi mwandishi alikuwa anatumia lugha ya mfano, ni lazima ieleweke katika maana yake ya kawaida. Sisi si hatustahili kuangalia kwa maana nyingine kama maana ya asili ya msitari una maana. Pia, sisi hatustahili kufanya maandiko kuwa ya kiroho kwa kushirikisha maana kwa maneno au misemo wakati mwandishi yu wazi, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, maana ieleweke kama ilivyoandikwa.
Mfano mmoja ni Ufunuo 20. Wengi hutoa maana mbalimbali kwa marejeo ya Kipindi cha miaka elfu. Hata hivyo, lugha haimaanishi kwa njia yoyote kwamba ushahidi wa miaka elfu moja kuchukuliwa kwa maana ya kitu kingine chochote Zaidi ya kipindi halisi cha miaka elfu moja.
Muhtasari rahisi kwa kitabu cha Ufunuo hupatikana katika Ufunuo 1:19. Katika sura ya kwanza, Kristo aliyefufuka na kuinuliwa anazungumzia Yohana. Kristo anamwambia Yohana "kwa hiyo andika, yale uliyoyaona, na yenye yako sasa na yatayofanyika baadaye." Mambo Yohana alikwisha yashuhudia ni kumbukumbu katika sura ya 1. "Mambo ambayo yalikuwa" (yaliokuwapo katika siku ya Yohana) ni kumbukumbu katika sura ya 2-3 (barua kwa makanisa). "Mambo yatakayofanyika" (mambo ya baadaye) ni kumbukumbu katika sura 4-22.
Kwa ujumla, sura ya 4-18 ya Ufunuo inazungumzia hukumu ya Mungu juu ya watu wa dunia. Hukumu hii si kwa ajili ya kanisa (1 Wathesalonike 5:2, 9). Kabla ya hukumu kuanza, kanisa itakuwa imeondolewa kutoka dunia katika tukio liitwalo kunyakuliwa (1 Wathesalonike 4:13-18, 1 Wakorintho 15:51-52). Sura ya 4-18 huelezea wakati wa "shida ya Yakobo" -matatizo kwa ajili ya Israeli (Yeremia 30:7; Danieli 9:12, 12:1). Pia ni wakati Mungu atawahukumu walio kufuru kwa sababu ya uasi wao dhidi yake.
Sura ya 19 inaeleza kurudi kwa Kristo na Kanisa, bibi harusi wa Kristo. Akiweza mnyama na yule nabii wa uongo na kuwatupa wao katika ziwa la moto. Katika sura ya 20, Kristo anamfunga Shetani na kumtupwa katika shimo la kuzimu. Basi, Kristo anauansisha ufalme wake hapa duniani ambao utadumu miaka 1000. Mwishoni mwa miaka 1000, Shetani atafunguliwa na anaongoza uasi dhidi ya Mungu. Yeye kwa haraka anashindwa na pia kutupwa katika ziwa la moto. Kisha hukumu ya mwisho hutokea, hukumu kwa makafiri wote, wakati wao pia watatupwa katika ziwa la moto.
Sura ya 21 na 22 hueleza kile kinajulikana kwetu kama hali ya milele. Katika sura hizi Mungu anatuambia namna milele pamoja naye itakuwa. Kitabu cha Ufunuo kinaeleweka. Mungu hangeweza kupeana hicho kitabu kwetu kama maana yake kamwe ilikuwa siri. Muhimu katika kuelewa kitabu cha Ufunuo ni kukitafsiri kijuu juu iwezekanavyo- kinasema chenye kinamaanisha na kumaanisha chenye kinasema.
English
Ni jinsi gani mimi ninaweza kuelewa kitabu cha Ufunuo?