settings icon
share icon
Swali

Biblia inamaanisha nini kwa kufunga na kufungua?

Jibu


Dhana ya "kufunga na kufungua" imefundishwa katika Biblia katika Mathayo 16:19: "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni;na lo lote utakalolifunga duniani,litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni." Katika mstari huu, Yesu anazungumza moja kwa moja na mtume Petro na moja kwa moja kwa mitume wengine. Maneno ya Yesu yalimaanisha kuwa Petero angekuwa na haki ya kuingia ufalme mwenyewe, kwamba atakuwa na mamlaka ya jumla yanayoashiriwa kwa kumiliki funguo, na kwamba kuhubiri injili itakuwa njia ya kufungua ufalme wa mbinguni kwa waumini wote na kufunga kwa makafiri. Kitabu cha Matendo kinatuonyesha njia hii ikitumika. Kwa mahubiri yake siku ya Pentekoste (Matendo 2: 14-40), Petro alifungua mlango wa ufalme kwa mara ya kwanza. Maneno "funga" na "fungua" yalikuwa ya kawaida kwa uteuzi wa maneno kisheria wayahudi kumaanisha kutangaza kitu kilichokatazwa au kutangaza kuwa kumeruhusiwa.

Petro na watumishi wengine walikuwa waendelee na kazi ya Kristo hapa duniani katika kuhubiri injili na kutangaza mapenzi ya Mungu kwa watu, na walikuwa na silaha ya mamlaka sawa na Yake aliyomiliki. Katika Mathayo 18:18, kuna pia kumbukumbu ya uhakika kwa kufunga na kufungua katika mtazamo wa nidhamu ya Kanisa. Mitume hawanyang’anyi ubwana na mamlaka ya Kristo juu ya waamini binafsi na hatima yao ya milele, lakini wanajaribu mamlaka kuadhibu na, kama ikilazimu,wawatenge na kanisa wanachama wasiotii .

Kristo mbinguni anaidhinisha kinachofanyika katika jina lake na katika klitii neno lake ulimwenguni.katika Mathayo 16:19 na 18:18,sintaksi ya maandishi ya Kigiriki hufanya maana wazi. utakachofunga duniani, tayari kitakuwa kimefungwa mbinguni. Utakachofungua duniani tayari kitakuwa kimefunguliwa mbinguni. Hiyo ni kumaanisha, Yesu mbinguni anafungulia mamlaka ya Neno lake yanapoelekea ulimwenguni kwa ajili ya kutimiza madhumuni yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inamaanisha nini kwa kufunga na kufungua?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries