settings icon
share icon
Swali

Ni nani walikuwa baba wa kanisa wa kitambo?

Jibu


Kuhani wa kanisa la kale wako katika makundi matatu ya msingi: Kuhani mitume, kuhani wa kabla -Nicene wa kanisa, na kuhani wa baada ya Nicene wa kanisa. Kuhani mitume ndio walikuwa kama Kilementi wa Roma ambao walitangamana na mitume na pengine walifundishwa na wao, wakichukua mila na mafundisho ya mitume wenyewe. Linus, aliyetajwa katika 2 Timotheo 4:21, alikuja akawa askofu wa Roma baada ya Petero kuuwawa kwa ajili ya Yesu, na Kilementi alirithi kutoka kwa Linus. Linus na Kilementi wa Roma wote, kwa hivyo,wanachukuliwa kuwa kuhani mitume.Hata hivyo, inaonekana kuwa hakuna maandiko ya Linus yaliyodumu, wakati mengi ya maandiko ya Kilementi wa Roma yalidumu. Kuhani mitume wanawezekana kuwa walikuwa wamepita zaidi kutoka kwa mandhari hiyo tangia mwanzo wa karne ya pili, isipokuwa kwa wale wachache ambao walikuwa wanafunzi wa Yohana, kama vile Polycarp. Mila ni kwamba mtume Yohana alikufa katika Efeso karibu AD 98.

Kuhani wa kabla ya Nicene walikuwa wale waliokuja baada ya kuhani mitume na kabla ya Baraza la Nicea katika AD 325. watu hao binafsi ni kama vile Iraenus, Ignatius, na Justin Martyr ndio kuhani wa kabla ya Nicene.

Kuhani wa baada ya Nicene wa kanisa ni wale waliokuja baada ya Baraza la Nicea katika AD 325. Hawa ni watu kama vile Augustine, askofu wa Hippo, ambaye mara nyingi huitwa papa wa [kanisa Katoliki] kwa sababu ya kazi yake kubwa katika mafundisho ya kanisa; Chrysostom,anayeitwa "golden-mouthed" kwa ajili ya ujuzi na ufasaha wake bora wa kusema; na Eusebius, ambaye aliandika historia ya kanisa kutoka kuzaliwa kwa Yesu hadi kwa AD 324, mwaka mmoja kabla ya Baraza la Nicea.Amejumulishwa katika zama za baada ya Nicene tangu hakuandika historia yake mpaka baada ya Baraza la Nicea kufanyika. Papa wengine wa baada ya Nicene walikuwa Jerome, ambao alitafsiri Agano Jipya la Kigiriki kwenda kwa valigeti ya Kilatini , na Ambrose, ambaye aliwajibika kwa kiasi kikubwa kubadili konsitebo mtawala hadi Ukristo.

Hivyo, nini kuhani wa kanisa la kale waliamini? Kuhani mitume walishughulika sana kuhusu kutangaza injili kuwa tu kama vile mitume wenyewe waliitangaza.Hawakuwa na haja ya kutunga mafundisho ya kiteolojia, kwa ajili ya injili waliyojifunza kutoka kwa mitume ilikuwa ya kutosha kabisa kwao. Kuhani mitume walikuwa wenye raghba kama mitume wenyewe katika kufichua na kuweka wazi mafundisho yoyote ya uongo ambayo yalijibuka katika kanisa la kitambo.Imani kamili ya ujumbe ilihifadhiwa kwa mahitaji ya kuhani mitume kutaka kukaa waaminifu kwa injili iliyofundishwa kwao na mitume.

Kuhani wa kabla ya Nicene pia walijaribu kukaa waaminifu kwa injili, lakini walikuwa na wasiwasi ya ziada.Sasa, kulikuwa na maandiko kadhaa ya uongo yakidai kuwa na uzito sawa na maandiko imara ya Paulo, Petero, na Luka. Sababu kwa hizi hifadhi za uongo zilikuwa na ushahidi. Kama mwili wa Kristo ungeweza kushawishika kupokea hifadhi ya uongo , basi kosa lingeingia polepole kwa kanisa. Hivyo kuhani wa kabla ya Nicene walitumia muda wao mwingi kutetea imani ya Kikristo kutoka kwa mafundisho ya uongo, na hii lilipelekea kwa mwanzo wa utengenezaji wa mafundisho yaliyokubalika ya kanisa.

Kuhani wa baada ya Nicene walichukua misheni ya kutetea injili dhidi ya kila aina ya uasi, hivyo zaidi na zaidi kuhani wa baada ya Nicene waliendelea kuvutiwa zaidi katika mbinu za kutetea injili na pia katika kupeleka injili katika njia ya kweli na haki. Hivyo, walianza kuanguka kutoka kwa imani ya kweli ambayo ilikuwa fadhila mahususi ya kuhani mitume. Hii ilikuwa miaka ya mwanateolojia na majadiliano yasiyoisha kwa mada ya kunga kama vile "ni malaika wangapi wanaweza kucheza juu ya kichwa cha zuzu."

Kuhani wa kanisa la kitambo ni mfano kwetu juu ya nini maana ya kumfuata Kristo na kutetea ukweli. Hakuna kuhani wa kanisa la kale hata mmoja alikuwa mkamilifu, tu kama vile hakuna hata mmoja wetu mkamilifu. Baadhi ya kuhani wa kanisa la kale walishikilia imani ambayo Wakristo wengi siku hizi huzichukulia kutokuwa sawa.Hatimaye kilichokuja kikawa masomo ya dini ya kikatoliki kina mizizi yake katika maandiko ya kuhani wa kanisa wa baada ya Nicene. Wakati tunaweza kupata maarifa na ufahamu kwa kujifunza kutoka kwa kuhani wa kanisa la kitambo, bila shaka imani yetu lazima iwe katika Neno la Mungu, si katika maandiko ya viongozi wa Kikristo wa kitambo. Tu Neno la Mungu ni mwongozo usio na dosari kwa imani na mazoezi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nani walikuwa baba wa kanisa wa kitambo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries