settings icon
share icon
Swali

Je, tunafaa kuishi maisha yetu namna gani katika mwanga wa kurudi kwa Kristo?

Jibu


Tunaamini kwamba kurudi kwa Yesu Kristo ni kweli, yaani, kurudi kwake kunaweza kutokea wakati wowote. Sisi, pamoja na mtume Paulo, tunatizamia "tukilitazamia tumaini lenye Baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu" (Tito 2:13). Kujua kwamba Bwana angeweza kurudi hii leo, baadhi yaw engine hujaribiwa kuacha kile wanachokifanya na "kusubiri" kuja kwake.

Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya kujua kwamba Yesu anaweza rudi leo hii na kujua kwamba atarudi leo hii. Yesu alisema, "Hakuna mtu anajua juu ya siku au saa" (Mathayo 24:36). Wakati wa kuja kwake ni kitu ambacho Mungu hajamfunulia mtu yeyote, na hivyo, mpaka atuite kwake mwenyewe, hatuna budi kuendelea kumtumikia. Katika mfano wa Yesu wa vipaji kumi, mfalme anayeondoka kwenda safari anawaamrisha watumishi wake na "kuchukua hadi pale atakaporudi" (Luka 19:13).

Kurudi kwa Kristo daima kumeelezwa katika maandiko kama motisha kubwa kwa hatua, si kama sababu ya kusitisha kutoka kwa kitendo. Katika 1 Wakorintho 15:58, Paul anatamatisha mafundisho yake juu ya kunyakuliwa kwa kusema, "mkazidi san kutenda kazi ya Bwana sikuzote.” Katika 1 Wathesalonike 5:6, Paulo anamalizia somo la kuja kwa Kristo kwa maneno haya "Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. “ Kwa mapumziko na "kushikilia ngome" kamwe haikuwa lengo la Yesu kwa ajili yetu. Badala yake, sisi hufanya kazi wakati tunaweza. "Usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi" (Yohana 9:4).

Mitume waliishi na kutumikia pamoja na wazo kwamba Yesu anaweza kurudi ndani ya maisha yao; je ingekuaje kama wangekoma kufanya kazi yao na "kusubiri"? Wao hawangekuwa watiifu kwa amri ya Kristo ya "kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri habari njema kwa kila kiumbe" (Marko 16:15), na hivyo basi Injili haingenea. Mitume walielewa kwamba kurudi kwa Yesu kulikua karibu maana ni lazima wajishughulishe wao wenyewe na kazi ya Mungu. Waliishi maisha ya ukamilifu, kana kwamba siku hiyo ndio ilikua yao ya mwisho. Sisi pia, lazima ktone kila siku kama zawadi na kuitumia kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunafaa kuishi maisha yetu namna gani katika mwanga wa kurudi kwa Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries