settings icon
share icon
Swali

Je, kujizuia kufanya ngono kabla ya ndoa ni ujumbe wenye uhalisi?

Jibu


Watu wengi katika tamaduni za kisasa wametangaza kwamba maadili ya ngono hayapo tena, kwamba kujizuia si jambo halisi, bali ni jambo la zamani na limepitwa na wakati. Je, kujizuia kufanya ngono kabla ya ndoa ni jambo halisi katika “utamaduni wa sasa kuhusu ndoa”?

Mungu alikusudia ngono ifurahiwe ndani ya uhusiano wa ndoa uliojitolea. Mungu alipowaleta Adamu na Hawa pamoja katika ndoa, alianzisha uhusiano wa “mwili mmoja”. Mwanzo 2:24 inatuambia kwamba mwanamume ataacha familia yake, na kujiunga na mke wake, na kuwa “mwili mmoja” pamoja naye. Kuna mistari mingi inayotangaza ngono kabla ya ndoa kuwa dhambi (Matendo 15:21; 1 Wakorintho 5:1; 6:13, 18; 10:8; 2 Wakorintho 12:21; Wagalatia 5:19; Waefeso 5:3; Wakolosai 3:5; 1 Wathesalonike 4:3; Yuda 7). Biblia inaamuru kujizuia kabisa kabla ya ndoa. Ngono kati ya mume na mke ndiyo mahusiano ya ngono ambayo Mungu anakubali (Waebrania 13:4).

Kweli ya Mungu ni ya milele— na sio ya kizamani au isiyo halisi. Walakini, ukweli wa Mungu sio rahisi kila wakati! Kujizuia kufanya ngono kabla ya ndoa mara nyingi ni vigumu na kunahitaji kujitolea, kujidhibiti, na mbinu fulani. Kwa kiwango fulani, inamlazimu mtu kuwa mwasi katika utamaduni “ulioerevuka kijinsia.”

Kwa kweli, falsafa ya elimu ya ngono imeleta mambo yasiyo mazuri katika utamaduni wetu— uraibu wa ponografia, magonjwa ya zinaa, uharibifu wa kihisia, na uavyaji mimba unapohitajika. Wengi katika utamaduni wa leo wanasema kwamba “kupatana kiholela” ndio lengo la usiku. Wasio na wapenzi huenda kutoka chumba cha kujivinjari hadi kingine wakitafuta kuchumbiana na mtu asiyemfahamu kwa ngono ya kiholela. Lakini hivyo sivyo Mungu alivyopanga ngono ifanye kazi.

Mwanamitandao Matt Walsh anaeleza hili vizuri: “Kueleza ngono kuwa ya kawaida’ ni kama kueleza dari ya Kanisa la Sistine Chapel kuwa “mchoro mdogo mzuri’…Watu wanaopunguza na kupuuza dhamani ya ngono ndio wanaopata kujionyesha kuwa ‘wameelimika kingono.”

Labda uko kwenye uhusiano wa kujitolea, labda hata umepatiwa ahadi ya ndoa. Kwako, ngono haitakuwa ya “kawaida”; hata hivyo, Mungu anataka ungojee uhusiano wa ndoa kabla ya kujamiiana. Kusubiri uhusiano huu wa karibu na wa kipekee uliotolewa na Mungu hadi wakati wa ndoa, kutaimarisha uhusiano wako na kuzuia majuto ya siku zijazo.

Wengi wanaona kujizuia na ngono kuwa jambo lisilowezekana kwa sababu hakuna mtu ambaye amewaonyesha jinsi ya kuishi. Ikiwa mtu anatikisa kidole tu na kusema, “Usifanye ngono kabla ya ndoa,” lakini hatoi zana za kuishi kulingana na ujumbe huo, kujizuia inakuwa vigumu zaidi. Hapa kuna vidokozeo kutoka kwa wale ambao wamekumbana na majaribu na kutembea katika njia ya kujizuia.

Elewa kwamba unaweza kuwa mwasi katika utamaduni. Hakuna mtu anayepaswa kukulazimisha kufanya ngono kabla ya ndoa. Ikiwa unataka kumheshimu Mungu kwa kutojamiiana hadi uhusiano wa ndoa, basi unaweza kufanya hivyo!

Lenga macho yako kwenye tuzo. Tuzo hiyo sio mwenzi wako wa baadaye. Sio usiku wa harusi yako, lengo lako la mwisho ni kuwa zaidi kama Kristo. Huo ndio mpango wa Mungu kwako.

Usijiweke katika hali ambapo utajaribiwa kulegeza masharti ya maadili yako—au usafi wako wa kingono. Hii inaweza kumaanisha kutokuwa pamoja, peke yenu. Unajua hali hizo zilivyo, kwa hivyo ziepuke.

Chumbia watu walio na nia kama yako. Wakati nyinyi nyote mnataka kujizuia, mnaweza kusaidiana kuweka ahadi ya kujizuia.

Weka mipaka. Uliza rafiki mzuri au mshauri awe mwajibikaji wako.

Kujizuia kufanya ngono ni zaidi ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa. Jitahidi kuwa na usafi wa kingono katika nyanja zote za maisha yako—katika mawawzo, kwa maneno, kwa vitendo. Ikiwa unafikiria au kuzungumza juu ya ngono mara nyingi, utakuwa na wakati mgumu zaidi kutoifanya.

Iwapo utamaduni unasema kujizuia ni jambo halisi au la, hiyo haibadilishi kweli ya Mungu. Ameweka ngono ili iwe katika mipaka ya ndoa, na Atakuandaa wewe kumheshimu Yeye kwa kujizuia. 1 Wakorintho 10:13 iansema, “Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.”

Je! inawezekana kujizuia na ngono? Naam. Je! Kujizuia ni rahisi kila wakati? La, lakini kwa Mungu, inawezekana.

Kumbuka: Labda tayari umepoteza ubikira wako. Tafadhali fahamu kwamba Mungu ni wa neema. Anataka uje kwake kwa toba, na atakusamehe dhambi zako na kuuponya moyo wako. Hujachelewa kufanya uchaguzi wa kuishi kwa haki na kwa njia zinazompendeza.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kujizuia kufanya ngono kabla ya ndoa ni ujumbe wenye uhalisi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries