settings icon
share icon
Swali

Nimekuwa nikiishi na mtu asiyeamini kwa miaka mingi. Hivi majuzi nilikuja kwa imani katika Kristo. Nifanye nini?

Jibu


Hakuna jibu rahisi kwa hali yako ngumu. Huenda mnapaswa kutengana, ukimweleza mwenza wako waziwazi kwamba umekuwa usiyemtii Mungu katika kuishi pamoja kabla ya ndoa, na kwamba kuendelea kuishi pamoja ni kuendeleza uasherati. Maandiko yako wazi kwamba uasherati ni dhambi na kwamba miili yetu imeundwa kumtukuza Bwana: “kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:20). Mungu hakukuokoa ili uendelee katika dhambi (Warumi 6:1-4).

Unaweza kuoa, ukiondoa wasiwasi wa uasherati, lakini ukifanya hivyo, unatengeneza nira isiyo sawa ambayo Mungu anakataza (2 Wakorintho 6:14). Sasa kwa kuwa Kristo ameingia maishani mwako upendo wako mkuu ni Kwake (Luka 14:26). Na kumpenda Bwana kunaenda sambamba na kumtii Bwana (Yohana 14:15).

Kanuni za kibiblia zilizowasilishwa hadi sasa ni waziwazi; hata hivyo, kunaweza kuwa na mazingatio mengine ambayo yanatatiza sualo hilo. Kwa mfano, kuna watoto wanaohusika? Pia, mahali unapoishi, ni sheria gani zinazohusu ndoa ya sheria ya kawaida? Inaweza kuwa tayari umefunga ndoa kisheria, kulingana na maelezo ya sharia ya ndoa katika eneo lako. Iwapo mlibadilishana viapo visivyo rasmi sio mbele ya ofisa, basi uwezekano mmoja ni kuadhimisha ndoa ambayo tayari mmejitolea. Ikiwa mwenzi wako wa ndoa ambaye si muumini hataki kuidhinisha uhusiano huo kwa leseni rasmi, kanuni ya 1 Wakorintho 7: 15 inaweza kutumika.

Zaidi ya kuomba juu ya suala hili na kuyachunguza Maandiko, ni muhimu kupata mshauri wa Mungu—mchungaji au mtu ambaye kwa hakika anaelewa Biblia na ambaye ana uzoefu mwingi wa maisha—ambaye unaweza kushiriki naye habari zote za hali yako. Unapofuata kanuni za Maandiko, omba kwa ajili ya ujasiri na neema. Njia ya kufuata itawekwa wazi. Amini kwamba Mungu anajua kweli ni nini kilicho bora kwako. Amini kwamba Yeye ana nia nzuri moyoni kwa ajili yako.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nimekuwa nikiishi na mtu asiyeamini kwa miaka mingi. Hivi majuzi nilikuja kwa imani katika Kristo. Nifanye nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries