Swali
Je! Ninawezaje kuyatoa maisha yangu kwa Mungu?
Jibu
Sisi sote tunaishi kwa kitu fulani. Tunaanza maisha tukiwa tumejitolea kikamilifu kujufurahisha wenyewe. Tunapokua hilo kwa kawaida halibadiliki sana. Lengo letu linaweza gaganyika zaidi kati ya zile sehemu ambazo ni muhimu kwetu, kama vile mahusiano, kazi, au malengo. Lakini jambo la msingi ni haja ya kutaka kujifurahisha. Kutafuta furaha ni safari ya kila mahali ulimwenguni.
Hata hivyo, hatukuumbwa ili tuishi kwa ajili yetu wenyewe. Tuliumbwa na Mungu, kwa mfano wake, kwa ajili ya mapenzi yake (Mwanzo 1:17; Wakolosai 1:16). Mwanafalsafa Blaise Pascal aliandika, “kunalo umbo ombwe lililoundwa na Mungu katika moyo wa kila mtu, na kamwe halitajazwa na kiumbe chochote kilichoumbwa. Linaweza kujazwa na Mungu, na kufanya kujulikana na Yesu Kristo.”
Katika historia yote, mwanadamu amejaribu kujaza ombwe kwa kila kitu isipokuwa Mungu: dini, falsafa, uhusiano wa kibinadamu au utajiri. Hakuna kinachotosheleza, vile inavyodhihirishwa na kukata tamaa, uchoyo, na hali ya kutokuwa na tumaini kwa ujumla ambayo ni sifa ya historia ya wanadamu. Yesu alisema, “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Katika Isaya 45:5 Mungu anasema, “Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu.” Biblia ni hadithi ya Mungu vile hajawai choka kumtafuta mwanadamu.
Tunapofikia kiwango cha kutambua kuwa maisha hayatuhusu sisi wenyewe, basi tuko tayari kuacha kutoroka kuotoka kwa Mungu na kumruhusu kuchukua nafasi yake. Njia pekee ambayo mtu yeyote kwetu anaweza kuwa na uhusiano na Mungu mtakatifu ni kukubali kwamba sisi ni watenda dhambi, kuacha dhambi hiyo, na kukubali dhabihu ambayo Yesu alitoa ili kulipia dhambi. Tanaungana na Mungu kwa njia ya maombi. Tunaomba kwa imani, tukiamini kwamba Mungu anatusikia na atatujibu. Waebrania 11:6 inasema, “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidi.” Tunaikiri dhambi, na kumshukuru Yesu kwa kututengenezea njia ya msamaha, na kumwalika atawale maisha yetu.
Kuja kwa Mungu kupitia kwa imani katika Yesu Kristo inamaanisha tunahamisha umiliki wa maisha yetu kwa Mungu. Tunamfanya Yeye kuwa mtawala, na Bwana wa maisha yetu. Tunabadilisha mioyo yetu ya zamani ya kujiabudu kwa ukamilifu wa Yesu (2 Wakorintho 5:21). Warumi 12:1 inatupa taswira ya maelezo ya kile hufanyika: “Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai.” Inatoa taswira ya madhabahu yaliyowekwa wakfu kwa yule Mungu wa kweli. Hebu fikiria ukitambaa juu ya madhabahu hayo na kusema, “Nipo hapa Mungu. Mimi ni mwenye dhambi, lakini bado wanipenda. Asante kwa kunikufia na kufufuka kutoka kwa wafu ndio dhambi zangu siweze kusamehewa. Nitakaze, na nifanye niwe mwana wako. Nichukue. Nichukue mzima. Ninataka kukuishia Wewe kwanzia sasa.”
Wakati tunajitoa kwa Mungu, Yeye hutuma Roho wake Mtakatifu kuishi ndani ya roho zetu (1 Yohana 4:13; Matendo 5:32; Warumi 8:16). Maisha sio kufanya chochote tunachotaka. Sisi ni wa Yesu, na miili yetu ni hekalu takatifu la Roho (1 Wakorintho 6:19-20).
Kuanzia wakati tunapotoa maisha yetu kwa Mungu, Roho Mtakatifu hutupatia nguvu na hamu ya kuishi kwa ajili ya Mungu. Anabadilisha “mahitaji” yetu. Tunapojisalimisha kila siku kwake, kuomba, kusoma Biblia, ibada, na ushirika na Wakristo wengine, tunakua katika imani yetu na katika ufahamu wetu wa jinsi ya kumpendeza Mungu (2 Petro 3:18).
Yesu alisema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate” (Luka 9:23). Mara nyingi, njia ambayo Mungu anatutakia inaongoza mwelekeo tofauti na ile ambayo sisi au marafiki wetu wangechagua. Ni chaguo kati ya njia pana na njia nyembamba (Mathayo 7:13). Yesu anajua kusudi alilotuumbia. Kugundua kusudi hilo na kuishi kwa ajili ya hilo ndio siri ya furaha ya kweli. Kumfuata Yesu ndiyo njia pekee tunayoweza kuipata.
English
Je! Ninawezaje kuyatoa maisha yangu kwa Mungu?