Swali
Je! Kuna uwezekano wa kuokolewa/kusamehewa baada ya kuwa na alama ya mnyama?
Jibu
Alama ya mnyama ni alama itakayo pachikwa usoni mwa mtu au katika mkono wake wa kuume katika nyakati za mwisho kama ishara ya kiapo cha utiivu kwa Mpinga Kristo (Ufunuo 13:15-18). Zaidi ya hayo, hakuna yeyote ataruhusiwa kufanya biashara bila alama hiyo (Ufunuo 13:17). Inaonekana kwamba aina fulani za ibada za Mpinga Kristo zimehuzishwa na kupokea alama hii ya mnyama (Ufunuo 14:9; 16:2), na wale watakao asi kuiabudu sanamu ya mnyama watauawa (Ufunuo 13:15).
Swali basi linaibuka ya kwamba ikiwa mtu ambaye amekwisha pokea alama ya mnyama anaweza kusamehewa. Jibu kwa swali hili linaonekana kuwa ni “la.” Ufunuo 14:10-11, ikielezea hatima ya mtu yeyote atakaye chukua alama ya mnyama, inasema hivi, “yeye pia atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa yeyote anayepokea chapa ya jina lake.”
Hatima ya milele kwa wale watakao chukua alama ya mnyama ni ziwa la moto. Je! ni kwa nini kuchukua alama ya mnyama ni dhambi ya laana ya milele dhidi yake Mungu? Ni kwa nini Mungu amhukumu kwenda kuzimu kwa kuchukua alama ya mnyama? Inaonekana kuwa, kuchukua alama ya mnyama ni jambo la kufuru la uasi wa makusudi dhidi yake Mungu. Kupokea alama ya mnyama kwa kawaida ni kumwabudu Shetani. Wale ambao watachukua wamefanya uamuzi wa kumtumikia Shetani badala ya kumtumikia Mungu na kumpokea Kristo kama Mwokozi. Wakati watu watafanya uamuzi huo katika kipindi cha dhiki, Mungu ataitikia ombi lao la kutengwa Naye milele.
English
Je! Kuna uwezekano wa kuokolewa/kusamehewa baada ya kuwa na alama ya mnyama?