settings icon
share icon
Swali

Je ni nini kuomba katika Roho?

Jibu


kuomba katika roho kumetajwa mara tatu katika maandiko. Wakorintho wa Kwanza 14:15 inasema, "Imekuaje basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia." Waefeso 6:18 inasema, "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote." Yuda 20 inasema,"Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika roho Mtakatifu." Hivyo, ni nini hasa maana ya kuomba katika Roho?

Neno la Kigiriki linalotafsiriwa "kuomba katika" linaweza kuwa na maana kadhaa tofauti. Linaweza kuwa na maana "kwa njia ya," "kwa msaada wa", "katika nyanja ya," na " katika uhusiano na." Naomba katika Roho haimaanishi maneno tunayoyasema. Badala yake, inaonyesha jinsi sisi huomba. Kuomba katika Roho ni kuomba kulingana na vile Roho anakuongoza. Ni kuomba kwa ajili ya mambo Roho anayuongoza kuombea. Warumi 8:26 inatuambia, "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maan hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Rooho mweneyew hutombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa."

Baadhi ya, kulingana na 1 Wakorintho 14:15, hulinganisha kuomba katika Roho na kuomba kwa lugha. Kwa kusunguzia Karama ya lugha, Paulo anataja "kuomba kwa roho yangu." Wakorintho wa Kwanza 14:14 yasema kwamba wakati mtu anaomba kwa lugha, yeye hajui akisemacho, kwa sababu yeye anasema katika lugha hajui. Zaidi ya hayo, hakuna mtu mwingine anaweza kuelewa kinachosemwa, isipokuwa kuwe mkalimani (1 Wakorintho 14:27-28). Katika Waefeso 6:18, Paulo anatufundisha "tuombe katika Roho wakati wote kwa kila aina ya sala na maombi." Je ni vipi tunaomba kwa kila aina ya maombi na dua na kuomba kwa ajili ya watu wa Mungu, kama hakuna mtu , ikiwa ni pamoja na mtu anayeomba, anafahamu ni nini kinasemwa? Kwa hivyo, kuomba katika Roho lazima ieleweke kuwa ni kuomba kwa nguvu za Roho, na uongozi wa Roho, na kulingana na mapenzi yake, si sawia na kuomba kwa lugha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuomba katika Roho ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries