settings icon
share icon
Swali

Je! Ninawezaje kuacha kuwa na woga katika kuomba hadharani?

Jibu


Watu wengi huona kusali mbele ya hadhara au katika kikundi kuwa jambo la kuogofya. Kuzungumza hadharani kwa aina yoyote ni moja ya hofu kuu inayopatikana kwa watu. Maombi ya hadhara huongeza shinikizo la ziada la kipengele cha kiroho na huwafanya watu kuwa na woga zaidi kwa sababu ya athari inayoweza kuwa nayo kwa watu wengine. Inafaa ikumbukwe, hata hivyo, ingawa sala inaamriwa na Mungu, sala ya hadharani haijaamrishwa. Kwa hakika, Yesu alisema tunaposali, tuingie chumbani, tufunge mlango na tuombe kwa siri (Mathayo 6:6). Kwa hiyo jambo la kwanza kuelewa kuhusu maombi ya hadhara ni kwamba sio la lazima kwa maisha ya Kikristo.

Kwa wale wanaotaka kujiunga katika kuomba hadharani, kunazo njia nyingi za kupunguza woga ambao mara nyingi huambatana na tukio hilo. Kwanza, ni muhimu kuomba pamoja na kundi la watu ambao tunastarehe nao, wale ambao tuna uhakika kwamba hawatatuhukuu kwa maombi yetu yasiyo na ufasaha. Kuomba pamoja na wengine kunaweza kuwa faraja kuu tunaposikia mahitaji yetu yakiinuliwa hadi kwenye kiti cha neema na wale wanaotujali vya kutosha kufanya hivyo. Wengine wanaotusikia tukiwaombea wanatiwa moyo vivyo hivyo. Kundi la watu wanaopendana na wamehitikiana kwa upendo na unyenyekevu kwa kawaida watapunguza woga wa wale ambao ni waoga kuomba hadharani.

Njia nyingine ya kupunguza mzigo wa woga ni kuomba kimya-kimya kabla ya kusimama hadharani kuomba, kumsihi Mungu aongoze akili na mioyo yetu kwake na mbali na sisi wenyewe. Wakati tunaelekeza mawazo yetu kwa Muumba wa ulimwengu na kujiruhusu kuzamishwa katika asili Yake kuu, tutapata mawazo yetu na hisia kujihusu zitaanza kudidimia. Chenye tunafaa kujishughulisha nacho ni kile Mungu anasema kutuhusu, na sio kile watu wengine wanachofikiria kutuhusu. Mungu anatupenda na upendo usiobadilika, na ikiwa sis ni wake kwa njia ya Kristo, ameweka dhambi zetu mbali nasi kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi (Zaburi 103:12), na anatualika kuja kwa ujarisi mbele ya kiti chake cha enzi cha neema (Waebrania 4:16). Kuzingatia kwamba Yeye hatuhukumu kwa kutokuwa na ufasaha itachangia katika kupunguza woga. Watu hutazama kwa nje, na hii ni pamoja na usemi, lakini Mungu huangalia moyo (1 Samweli 16:7).

Mwisho, watu wengi wanaona kwamba kurudia-rudia maombi katika hadhara kutapunguza woga. Kuomba pamoja na wengine kunaweza kuwa jambo la kujenga sana, lakini hatimaye sala ni fursa ya kuwasiliana na Baba yetu wa mbinguni ambaye huona mioyo yetu na anajua tunachohitaji kabla hata hatujaomba. Haitaji kusikia ufasaha katika maombi yetu ili atubariki na kutukaribia. Anachoomba ni moyo uliotubu na roho ya unyenyekevu, mambo amabyo hatakataa kamwe (Zaburi 51:17), haijalishi maombi yetu ni ya ufasaha kiasi gani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ninawezaje kuacha kuwa na woga katika kuomba hadharani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries