Swali
Biblia inasema nini kuhusu kuombea wagonjwa?
Jibu
Agano la Kale lina mifano michache sana ya watu kuponywa baada ya kuomba Mungu moja kwa moja kwa ajili ya uponyaji. Kawaida ombi la uponyaji hupatanishwa kupitia nabii ambaye anaweza kuomba uponyaji au kuwa njia ya nguvu ya Mungu kufanya muujiza wa uponyaji au hata ufufuo. Daudi aliomba kwamba mtoto wake machanga aponywe, lakini Mungu hakukubali ombi lake (2 Samweli 12:16-17). Hezekia alipoambiwa na nabii Isaya kwamba atakufa, aliomba apewe muda zaidi, na Mungu akampa miaka kumi na mitano zaidi ya kuishi (2 Wafalme 20).
Ikiwa kukosa uwezo wa kutopata watoto unachukuliwa kuwa ugonjwa, basi matukio ya kuomba kwa ajili ya “uponyaji” na Mungu kujibu hitaji hilo mara kwa mara ni mengi mno.
Katika Injili, Yesu aliwaponya wengi ambao walimuuliza Awaponye. Katika Matendo, watu kadhaa wanaponywa baada ya kuwauliza mitume kuwaponya, sawa na utaratibu wa Agano la Kale wa kutafuta uponyaji kutoka kwa nabii wa Mungu. Hakuna mojawapo ya matukio haya yanayoonekana kuwa na matumizi ya moja kwa moja kwetu hii leo.
Katika Wafilipi 1, Paulo anasema kwamba Epafrodito alikuwa mgonjwa, hata karibu kufa, lakini Mungu alimrehemu na kumponya (mistari ya 25-29). Tunaweza kudhani kwamba Paulo alimwombea Epafrodito, lakini hilo halijasemwa waziwazi. Katika 1 Timotheo 5:23, Paulo anataja kwamba Timotheo ana ugonjwa wa mara kwa mara unaoonekana kuwa unahusiana na tumbo, na anapendekeza kunywa divai kidogo. Hamwambii Timotheo kuomba uponyaji. Katika 2 Wakorintho 12, Paulo anaomba kwamba “mwiba katika mwili” wake uondolewe, lakini Mungu anakataa kufanya hivyo. Kwa sababu hiyo, Paulo anasema kwamba ataufurahia udhaifu wake-neno ambalo kwa kawaida hutumiwa kumaanisha magonjwa mbalimbali. Katika tukio hili, Paulo aliomba kwa ajili ya uponyaji, lakini ombi lake lilikataliwa. Badala ya kumfikia kwa uponyaji, Bwana alimwambia Paulo kutegemea neema Yake (mstari wa 9)
Maagizo pekee ya kibiblia yaliyo wazi kuhusiana na maombi ya uponyaji yanapatikana katika Yakobo 5:13-16: “Je, mtu yeyote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna yeyote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu. Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa. Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.”
Yakobo anatoa maagizo maalum. Mtu ambaye ni mgonjwa anatakiwa kuandaa kutaniko la kimaombi ya uponyaji kutoka kwa wazee. Wazee humpaka mgonjwa mafuta na kutoa sala ya imani, na Mungu anaahidi “kuwaponya.” Walakini, kwa kuwa muktadha wa karibu unahusiana na kukiri dhambi na msamaha, inaweza kuwa kwamba ugonjwa unaonekana ni matokeo ya dhambi maaalum. Walakini, utaratibu huu ni juhudi za kikundi zinazohusisha uongozi wa kanisa. Zaidi ya hayo, wazee ndio wanaoitwa kuonyesha imani katika sala yao. Hili lingeonekana kuondoa madai kwamba baadhi ya “waponyaji” hawawezi kuponya kwa sababu mgonjwa hana imani ya kutosha.
Kwanza, Yakobo 5:13-16 itaonekana kuhakikishia uponyaji kila wakati, lakini ni lazima tuyaangalie Maandiko yote. Kunazo vifungo kuhusu maombi, ambavyo vikichukuliwa kipekee, pia itaonekana kuwa Mungu “ashayajibu”:
Marko 11:24: “Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.”
Mathayo 21:22: “Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”
Yohana 14:13: “Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana.”
Yohana 15:7: “Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa.”
Yohana 16:23: “Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa.”
Vifungu hivi vinahitaji kueleweka katika muktadha mkubwa zaidi wa kusali sikuzote katika mapenzi ya Mungu, kama vile 1 Yohana 5:14 inavyosema: “Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” Sharti la kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu ni sawia na maagizo ya kuomba “katika jina la Yesu.” Kuomba katika jina la Yesu ni kuomba vile vitu vinavyomheshimu na kumtukuza Yesu. Kutamani vitu vilivyo kando na mapenzi ya Mungu haiwezi mheshimu Yesu.
Yesu anatoa kielelezo cha kuomba kadri na mapenzi ya Mungu. Katika Gethsemane, Aliomba kwamba, “kikombe hiki” (kusulubiwa) kingempita, Lakini “si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke” (Luka 22:42). Yesu hakuuepuka msalaba, kwa kuwa ilikuwa amapenzi ya Mungu kwamba ateseke kupitia msalaba huo.
Tukichukua mafundisho yote juu ya uponyaji na maombi kwa Pamoja, inafaa kuomba kwa ajili ya uponyaji au jambo linguine lolote tunalohisi kwamba tunahitaji au kutamani. Hata hivyo, siku zote tunahitaji kukiri kwa uangalifu kwamba tunakubali hukumu ya Mungu ili kutupa kilicho bora zaidi, na mara nyingi hatujui ni nini kinachofaa zaidi kwetu au kile kinacholingana na mpagno Wake mkubwa zaidi. Kuomba “si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke” hakutokani na ukosefu wa imani kama wengine wanavyofundisha; badala yake, ni kauli kuu ya imani katika wema wa Mungu na mpango na makusudi yake. Hakuna ushahidi katika Maandiko kwamba daima ni mapenzi ya Mungu kuponya. Kwa kweli, tunayo mifano mingi katika Maandiko ya Mungu kutoponya watu. Wakati mwingine ni mapenzi yeke sisi kuteseka katika magumu au magonjwa ili tuweze kuwa na kiwango cha juu zaidi cha afya ya kiroho kuliko ambavyo tungeweza kufikia.
English
Biblia inasema nini kuhusu kuombea wagonjwa?