settings icon
share icon
Swali

Ni namna gani Mkristo anastahili kupigana na hisia za hatia kuhusu dhambi za zamani, hata kama kabla ya au baada ya wokovu?

Jibu


Kila mtu ametenda dhambi, na moja ya matokeo ya dhambi ni hatia. Tunaweza kushukuru kwa hisia na hatia kwa sababu hutusukuma kutafuta msamaha. Wakati mtu anarudi kwa Yesu Kristo kutoka dhambi kwa imani, dhambi yake husamehewa. Toba ni sehemu ya imani ambayo inaongoza kwa wokovu (Mathayo 3:2; 4:17; Matendo 3:19).

Katika Kristo, hata dhambi ya kutisha zaidi hufutwa (angalia 1 Wakorintho 6:9-11 kwa orodha yote ya matendo maovu ambayo yanaweza kusamehewa). Wokovu ni kwa neema , na neema husamehe. Baada ya mtu kuokolewa, yeye bado hufanya dhambi, na anapofanya , Mungu bado ahidi msamaha. "Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki " (1 Yohana 2:1).

Uhuru kutokana dhambi, hata hivyo, daima haumanishi kuwa uhuru na hisia hatia. Hata wakati dhambi zetu zimesamehewa, sisi bado hukumbuka. Pia, tuna adui wa kiroho, anayeitwa "mshitaki wa ndugu zetu" (Ufunuo 12:10) ambaye bila kuchoka anatukumbusha makosa yetu, makosa, na dhambi. Wakati Mkristo anahisi hisia za hatia, ni yeye lazima afanye mambo yafuatayo:

1) Ungama yote yanayojulikana, ya awali ambayo haijatubu dhambi. Katika baadhi ya matukio mengine, hisia ya hatia ni sahihi kwa sababu ya kukiri kunahitajika. Mara nyingi, sisi uhisi hatia kwa sababu sisi tuna hatia! (Angalia maelezo ya Daudi kuhusu hatia na suluhisho katika Zaburi 32:3-5).

2) Muulize Bwana akuonyeshe dhambi zingine zozote ambayo unahitaji kuungama. Kuwa na ujasiri wa kuwa wazi kabisa na mwaminifu mbele za Bwana. "Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, unijaribu, uyajue mawazo yangu; uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, ukiongoze katika njia ya milele" (Zaburi 139:23-24).

3) Tumainia ahadi za Mungu kwamba Yeye atasamehe dhambi na kuondoa hatia, kwa kuzingatia damu ya Kristo (1 Yohana 1:9, Zaburi 85:2; 86:5, Warumi 8:1).

4) Katika hafla wakati hisia na hatia hutokeza juu ya dhambi tayari ishakiriwa na kuachwa, kataa hisia kama vile hatia ya uongo. Bwana amekuwa mwaminifu kwa ahadi zakeza kusamehe. Kasome na kutafakari juu ya Zaburi 103:8-12.

5) Muulize Bwana amkemee shetani, mshtaki wako, na muulize Bwana akurejeshee furaha ambayo huja kutoka kuwekwa uhuru na hatia (Zaburi 51:12).

Zaburi 32 ni utafiti wa faida sana. Ingawa Daudi alikuwa ametedna dhambi sana, alipata uhuru kutoka kwa dhambi na hisia na hatia. Alipambana na sababu ya hatia na hali halisi ya msamaha. Zaburi 51 ni kifungu kingine kizuri cha kuchunguza. Mkazo hapa ni ungamo la dhambi, kama Daudi anavyomwomba Mungu amwondoe kwa moyo imejaa hatia na huzuni. Matokeo ni urejesho na furaha.

Mwisho, kama dhambi imeungamwa, tubu, na kusamehewa, ni wakati wa kusonga mbele. Kumbuka kwamba sisi ambao tumekuja kwa Kristo tumefanywa viumbe vipya ndani yake. "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Krisot amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya"(2 Wakorintho 5:17). Sehemu ya "kale" ambayo imepita ni kumbukumbu ya dhambi za zamani na hatia inayozalisha. Kwa bahati mbaya, baadhi ya Wakristo hukabiliwa na kugaga katika kumbukumbu ya maisha yao ya zamani ya dhambi, kumbukumbu ambayo inapaswa kuwa amekufa na kuzikwa muda mrefu uliopita. Hizi si sababu ambazo hupinga ushindi wa maisha ya Kikristo Mungu anatutakia. Msemo busara ni "Kama Mungu amekuokoa toka mfereji wa maji machafu,usirudi kupiga mbizi na kuogelea humo."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni namna gani Mkristo anastahili kupigana na hisia za hatia kuhusu dhambi za zamani, hata kama kabla ya au baada ya wokovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries