Swali
Je! Inamaanisha nini kupotea kiroho?
Jibu
Neno waliopotea linatumika katika Biblia na katika makundi mengi ya Kikristo kurejelea watu ambao bado hawajapata uzima wa milele katika Kristo. Yesu alisema, “Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10). Wale ambao wamepotea kiroho wametengwa na Mungu na hawawezi kupata njia yao ya kurudi kwake.
Kupotea ni kutangatanga na kutokuwa na uwezo wa kutafuta njia ya kurudi. Mkweya mlima anaweza kuptoea anapofuata njia mbaya na hajui jinsi ya kurudi kwa njia sahihi. Mtoto anaweza kupotea wakati anatangatanga mbali na wazazi wake na hajui walipo. Wanadamu tumepotea kiroho kwa sababu tumeenda mbali na Mungu na hatujui jinsi ya kumpata tena.
Isaya 53:6 inasema, “Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye Bwana aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.” Biblia inalinganisha wanadamu na kondoo (Zaburi 23; Yohana 10:11-14) kwa sababu kiasili kondoo hawawezi kujikinga. Hawana hekima na huwa wanamfuata mchungaji, haijalishi mchungaji anawaelekeza wapi. Kindoo wanahitaji mchungaji ili kuishi. Mchungaji huwalinda kondoo dhidi ya mashambulizi, huwaongoza kwenye malisho mazuri, na kuwalinda ili wasipotee. Kondoo huwa na tabia ya kutangatanga kutoka kwenye kundi na wanaweza kulengwa kwa urahisi na Wanyama wanaowawinda. Katika maana ya kiroho, watu huwa na mwelekeo wa kutangatanga na kuwa shabaha rahisi kwa adui yetu, Sheteni. Biblia Yesu, Mchungaji wetu Mwema, tumepotea kiroho na hatuwezi kumpata Mungu peke yetu.
Yesu alisimulia mfano kuhusu mwana-kondoo aliyepotea ili kuelezea moyo wa Mungu kwa watu waliopotea (Luka 15:3-7). Mchungaji Mwema alikuwa tayari kuwaacha wale kondoo tisini na tisa zizini ili kwenda kumtafuta yule mwana-kondoo mmoja aliyepotea. Mwana-kondoo hangempata Mchungaji peke yake. Mfano huu unaonyesha fikira za Mungu kuhusu kila mtu. Yeye hasimamishwi na chochote katika kuwatafuta wale wanaomhitaji na kuwaleta salama katika uwepo Wake. Kama vile kondoo waliopotea hawawezi kumpta Mchungaji wao wenyewe, watu waliopotea hawawezi kumpta Mungu wao wenyewe (Zaburi 53:2-3; Warumi 3:11).
Dini ni jaribio la mwanadamu kumtafuta Mungu peke yake. Dini huunda lengo, ambalo linaweza kuwa mungu au hali ya juu zaidi, na kisha kutangaza hatua fulani muhimu ya kufikia lengo hilo. Kwa sababu ya dini, watu waliopotea wanajiona kuwa hawajapotea. Fikiria msafiri ambaye amepotea njia. Baada ya saa nyingi za kutafuta njia sahihi bila mafanikio, anaamua kukita kambi msituni asikojulikana na kusema ya kwamba sasa amefika nyumbani. Hatajaribu tena juhudi za kuokolewa. Ijapokuwa bado hajui alipo, kuyazoea mazingira yake ya karibu kunamfanya afikirie kuwa amepatikana.
Ukristo haufuati mtindo huo. Ukristo unafundisha kwamba ni bure kwa waliopotea kujaribu kumtafuta Mungu, na ndiyo maana Mungu alimtuma Yesu kutafuta waliopotea. Mungu alitufanyia yale ambayo hatungeweza kufanya sisi wenyewe (Warumi 5:8). Hata wakati hatujitambui kuwa tumepotea, Yeye anajua hali yetu. Kwa hiyo Mwana wa Mungu alishuka mbinguni ili kututafuta na kutuleta nyumbani (Wafilipi 2:5-8; Mathayo 18:11; Yohana 3:16-18).
Tumezaliwa tukiwa wapotevu kwa sababu tuna asili ya dhambi iliyorithiwa kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza (Mwanzo 3) ambayo hutusukuma kumwasi Mchungaji wetu (Warumi 3:23). Tuliumbwa ili tuwe nyumbani kwake, tukitembea kwa maelewano na utiivu. Lakini kwa sababu ya dhambi zetu, tumepotea (Isaya 59:2). Pengo kati yetu na Mungu haiwezekani kwetu kuliziba, na hatuwezi kupata njia yetu ya kurudi katika uwepo Wake. Watu waliopotea kiroho wamefungwa na dhambi zao na kuhukumiwa kuzimu (Luka 12:5; Warumi 6:23). Lakini ikiwa waliopotea wanaweka tumaini lao katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, daraja linafunguka mbele yao. Kwa sababu neema na upendo wa Mungu, waliopotea wanaweza kurudi kwa Mungu (1 Petro 2:25).
Kila binadamu amepotea au kuwa kwa Mungu. Sisi sote tuko katika mojawapo ya hayo makundi mawili. Hatua ya kwanza ya kuwa kwa Mungu ni kukubali kwamba tumepotea. Tunakubaliana na Mungu kwamba dhambi yetu instahili adhabu, na tunakubali kwamba adhabu aliyopata Yesu ilitosha kulipia. Tunapokea zawadi hiyo kwa unyenyekevu kupitia imani (Waefeso 2:8-9). Katika ubadilisho wa kiungu, Mungu huzitundika dhambi zetu msalabani na kuhamisha haki ya Kristo kwetu (Wakolosai 2:14). Kisha tunaingia katika uhusiano mpya na Mungu kama watoto Wake wapendwa. Hatutapotea tena. Tumepatikana, tumesamehewa, na kupewa mwanzo mpya (2 Wakorintho 5:17).
English
Je! Inamaanisha nini kupotea kiroho?