Swali
Je, nawezaje kushinda shinikizo la rika?
Jibu
Kwa nini tunakabiliwa na shinikizo la wenzetu? Biblia inatuambia wazi kwamba hatupaswi kutarajia maisha yetu kuwa kama maisha ya watu wengine (wasioamini ) katika ulimwengu huu. Kama Wakristo, sisi ni wageni hapa duniani (1 Petro 2:11 ), na ulimwengu huu si nyumbani kwetu. Kama vile Kristo alivyokataliwa, na bado anakataliwa, na watu wengi ambao wanataka kuishi maisha yao kwa njia yao wenyewe na isiyompendeza Mungu, tutakutana na watu kama hao ambao watatuchukia kwa imani yetu.
Katika sura ya kwanza ya 1 Wathesalonike, Paulo anazungumzia jinsi tunavyoweza kujua kuwa sisi ni Wakristo. Kati ya mambo anayosisitiza (ona 1 Wathesalonike 1:6 ) ni ukweli kwamba tunapaswa kuwa na furaha licha ya mateso. Tunapaswa kutarajia kukabiliana na majaribu na dhuluma kama wakristo, lakini tufarijike kwa kwa sababu Mungu yuko katika udhibiti na atalipa kisasi kwa kila uovu utakaofanywa dhidi yetu. Katika 2 Wathesalonike, Paulo anazungumzia matatizo ambayo kanisa hili lilikuwa linaendelea kukumbana nayo. Aliwaambia kwamba wakati Kristo atakaporudi na Mungu kuhukumu ulimwengu, Mungu “kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi, na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja nasi” ( 2 Wathesalonike 1:6-7 ). Ingawa Wakristo wengi hawatakabiliwa na mateso kama yale ya Wathesalonike, au kama ya wale wanaoishi nchini Sudan ambao wanauwawa kwa sababu ya imani yao, bado tunateseka kwa njia fulani, kama vile mateso ya shinikizo la rika.
Biblia inasema nini kuhusu kukabiliana na shinikizo la rika? Biblia haijatumia kamwe maneno “shinikizo la rika” lakini inatuambia jinsi tunavyopaswa kukabiliana na majaribu mengi tutakayokabiliana nayo katika maisha yetu, hasa yale yanayohusisha wasioamini. Warumi 12:2 inasema, “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza,na ukamilifu.”
Warumi 12:14-16 inasema, “Wabarikini wanaowaudhi, barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio, lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili”
1 Petro 1:13-21 inasema, “kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa , Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya dhamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu, ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.”
Biblia inatuambia kwamba tunaweza kumwamini Mungu kwamba atafanya kazi yote pamoja kwa wema wa watoto wake ( Warumi 8: 28 ). Hata hivyo, Biblia haihadi maisha rahisi, bali maisha ambayo yanamtukuza Mungu tunapojifunza changamoto ngumu na kushinda mashambulizi ya Shetani ambayo ingekuwa ngumu kushinda bila Mungu. Tunafananishwa na “Kristo” wakati Mungu anatubadilisha kupitia maisha yetu yote ( Warumi 8:29-30 ). Jipe faraja kwamba Kristo Mwenyewe alijaribiwa kwa njia zote tulizojaribiwa; anaelewa jinsi ilivyo ngumu. Hata hivyo, Biblia inatuhakikishia kwamba Mungu atatoa njia ya kutoroka kutoka kwa kila jaribu ( 1 Wakorintho 10:13). Weka imani yako yote na tumaini kwa Mungu. Mwache yeye awe nguvu yako pekee ( Wafilipi 4:13) na mwongozo wako ( Zaburi 23).
Shinikizo la rika litakuwa jambo la muda mfupi maishani mwetu. Shinikizo la rika kwa kiasi kikubwa linahusu kutokuwa na uhakika na hamu ya kukubalika na watu wote waliohusika. Watu wengi huishia kugundua kuwa kuwatisha wengine ili kujihisi muhimu ni njia ya kudhibiti na ni ishara ya kukosa ukomavu. Wale waliokuwa wafuasi mara nyingi hutambua umuhimu wa kufanya maamuzi yao wenyewe na kuwa watu binafsi badala ya kudhibitiwa na mtu mwingine. Hatupaswi kukubali shinikizo la rika, kwa chochote kile kinachotokea. Kusimama kwa imani yetu na kwa kile Biblia inafundisha kutamfurahisha Mungu. Kupitia historia, wale ambao hawakutishwa kusimama kwa imani zisizopendwa wamekuwa watu wanaobadilisha dunia na kufanya mambo kutokea. Kuna mengi katika ulimwengu huu tunayohitaji kubadilisha, na watu wengi ambao wanahitaji kufahamishwa kuhusu Kristo. Kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yetu na kudhibiti tabia zetu ni jambo ambalo shetani anatumai tutafanya; ikiwa hatutasimama kwa yale yaliyo sahihi kwa sababu ya shinikizo la rika, tunasimama kwa yale yasiyo sahihi.
English
Je, nawezaje kushinda shinikizo la rika?