settings icon
share icon
Swali

Kusudi la mahari lilikuwa gani katika (Mwanzo 31:15)?

Jibu


Mahari, wakati mwingine huitwa gharama ya bi arusi, ilikuwa malipo ambayo mwanamume alitoa kama zawadi kwa familia ya mwanamke ambaye alitamani awe mke wake. Katika Mwanzo 29, Yakobo alimpenda Raheli na akajitolea kufanya kazi kwa miaka saba kwa baba yake, Labani, ili akaweze kupewa Raheli katika ndoa. Huu ni mfano mmoja wa mkataba wa kale wa mahari.

Katika siku za Yakobo, kutoa mahari kwa Raheli ilikuwa jukumu iliyotarajiwa kidesturi katika utamaduni. Kupanga kulipia mahari lilikuwa jambo lililokubalika pia. Mwanachuoni mmoja asema, “Kuhusu ndoa kwa ujumla, viabo vya Nuzi vilisema kwamba ikiwa mwanamume atafanya kazi kwa muda kwa ajili ya baba ya msichana ambaye angependa kumuoa, basi angekuwa na haki ya kumchukua msichana huyo kuwa mke wake” (Stuard A. West, “The Nuzi Tablets,” Bible and Spade 10:3–4, Summer–Autumn 1981, p. 70).

Kwa kuwa Yakobo hakuwa na chanzo kingine kikubwa cha mapato wakati huo, alijitolea kufanya kazi ndio Raheli awe mke wake. Alielewa kuwa hilo ndilo pendekezo pekee angefanya na limpendeze Labani. Wasomi wanaona kwamba vibarua katika Mashariki ya Karibu ya kale kwa ujumla walipata kati ya shekeli nusu na shekeli moja kwa mwezi. Labani angeona pendekezo la miaka saba ya kazi bila malipo kuwa ukarimu sana. Yakobo alitaka kutoa pendekezo lake la kuvutia ili kuhakikisha Labani “ameitikia” kumpa Raheli katika ndoa.

`Yakobo alidanganywa na Labani na kwanza akampa Lea dadaye Raheli, kuwa mke wake. Ili kumwoa Rahili, Yakobo alipaswa kukubali miaka mingine saba ya kazi. Hatimaye wakati ulipofika wa Yakobo na familia yake kuondoka katika nyumbaya Labani, Lea na Raheli walisema, “Je bado tu tunalo fungu lolote katika urithi wa nyumba ya baba yetu? … Sio kwamba ametuuza tu, bali ametumia hata na vile vilivyolipwa kwa ajili yetu” (Mwanzo 31:14-15). Miaka ya kazi ya Yakobo kwa ajili ya Raheli ilionekana waziwazi na wanawake hao kuwa njia ya mapato kwa Labani—mapato ambayo alikuwa ametumia, akiwaacha binti zake bila urithi.

Bado leo hii, mfumo wa mahari unatumiwa katika sehemu nyingi za ulimwengu, hasa katika India, Bangladesh, Pakistan, Sri Lanka, na Nepal. Mchakato unahitaji ushirika wa familia zote mbili na kujitolea kwa kina kwa mume mtarajiwa kabla ya ndoa. Katika mataifa ya Magharibi, mapokeo tofauti yamejibuka ambayo yahusisha kuwauliza wazazi wa mwanamke baraka zao katika ndoa. Pia kwa kiasi fulani utata ni kwamba, leo hii, mahari mara nyingi huchukuliwa kuwa ni pesa au bidhaa nyingine ambazo mwanamke huleta kwenye ndoa badala ya kile ambacho mwanamume hutoa.

Mfumo wa mahari ni utaratibu wa muda mrefu katika utamaduni wa Mashariki ambao bado unatumika hadi leo hii. Faida ni pamoja na uhusiano wa karibu kati ya familia zote mbili na uhakikisho wa kujitolea kwa mwanamume katika ndoa. Kizuizi kinaweza kuwa ukosefu wa pesa ambacho hutumika kama kigezo kwa uwezo wa mtu kuoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kusudi la mahari lilikuwa gani katika (Mwanzo 31:15)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries