Swali
Kusudi la maombi ni gani?
Jibu
Maombi ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikristo. Ni jinsi tunavyowasiliana na Bwana na kumsifu. Ili kuelewa kusudi la maombi, ni muhimu kwanza kuelewa kile maombi hayako. Kunayo mitazama mingi potofu katika ulimwengu na utamaduni kuhusu maombi, hata miongoni mwa Wakristo, na haya yanapaswa kushughulikiwa kwanza. Maombi sio
• Kubishana na Mungu.
• Kumpa Mungu masharti
• Kumwomba Mungu mazuri tu.
• Zoezi la matibabu, aina ya kutafakari.
• Kumsumbua Mungu na kuchukua wakati wake
• Namna ya kumtawala Bwana.
• Njia ya kuonyesha hali ya kiroho ya mtu mbele ya wengine.
Watu wengi wanaamini maombi yanahusu tu kumwomba Mungu mambo. Ingawa dua ni sehemu ya maombi (Wafilipi 4:6), sio kusudi pekee la maombi. Kuomba kwa ajili ya mahitaji yetu na ya wengine kunahitajika na kunanufaisha, lakini kuna mengi zaidi kwa maombi. Mungu si jini wa kichawi anayejibu kila tunalotaka was si Mungu dhaifu anayewza kudhibitiwa na maombi yetu.
Njia bora ya kujifunza kuhusu kusudi la maombi ni kujifunza mfano wa Yesu wakati wa huduma Yake duniani. Yeus alijiombea mwenyewe wakati wa huduma Yake duniani. Yesu alijiombea mwenyewe na kwa ajiliya wengine, na aliomba ili kuzungumza na Baba. Yohana 17 ni mahali pazuri pa kuona Yesu akitumia maombi. Haombi tu kwamba Baba atukuzwe bali pia anawaombea wanafunzi Wake na “wale wote watakaoniamini kupitia neno lao” (Yohana 17:20). Kujisalimisha kwa mapenzi ya Baba kulikuwa sehemu nyingine ya maisha ya maombi ya Yesu, vile imeangaziwa katika Sala yake ya Gethsemane: “Lakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe” (Mathayo 26:39). Katika ombi lolote tulilo nalo, ni lazima tujisalimishe kwa mapenzi ya Mungu.
Licha ya kuwaombea wengine, maombi pia ni njia ya kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Yesu aliweka mfano, alipokuwa akiomba kwa Baba katika huduma yake ya dunia (Luka 6:12; Mathayo 14:23). Wale walio katika mahusiano kwa kawaida wanatafuta kuwasiliana wao kwa wao, na maombi ni mawasiliano yetu na Mungu. Mifano mingine mizuri katika Biblia ya wale waliotumia wakati katika maombi ni Daudi, Hezekia, na Paulo.
Hatimaye, lengo kuu la maombi ni kuabudu. Tunapoomba kwa Bwana, tukitambua Yeye ni nani na amefanya nini, nit endo la ibada. Kuna mifano mingi ya maombi kuwa tendo la ibada katika Biblia, ikijumuisha 2 Wafalme 19:15, 1 Mambo ya Nyakati 17:20; Zaburi 86:12-13 na Warumi 11:33-36. Jinsi tunavyoomba inapaswa kuakisi kusudi hili; lengo letu linapaswa kuwa juu ya Mungu ni nani, na sio sisi wenyewe.
Cha kushangaza, mfano wa maombi ambayo Yesu aliwapa wanafunzi katika Mathayo 6:9-13, inayojulikana kama Sala ya Bwana, ina vipengele hivi vyote. Sehemu ya kwanza inajumuisha sifa na kumbwabudu Mungu (Mathayo 6:9), na kisha sehemu ya pili inaendelea na kuomba ili mapenzi ya Mungu yatimizwe (Mathayo 6:10). Baada ya haya, kuna dua kwa ajili yetu na wengine (Mathayo 6:11-12), pamoja na kuomba nguvu za kukabiliana na majaribu (Mathayo 6:11-12), pamoja na kuomba nguvu za kukabiliana na majaribu (Mathayo 6:13). Yesu alitoa mfano wa maombi haya kwa wanafunzi wake, na inaonyesha sababu zote za maombi kwa lengo kuu la ibada.
Maombi ni sehemu muhimu ya maisha ya Mkristo, na maisha ya maombi ya mtu yanapaswa kuanzishwa. Maombi hayaathiri maisha yetu pekee bali maisha yaw engine, lakini pia ni njia ya kuwasiliana na Bwana na kukua katika uhusiano wetu Naye. Katika kiini cha maombi ni tendo la ibada kwa Bwana. Neno la Mungu husisitiza juu ya nguvu na kusudi la maombi, na kwa hivyo, halipaswi kupuuzwa.
English
Kusudi la maombi ni gani?