settings icon
share icon
Swali

Je, ninafaa kuangalia nini katika mume?

Jibu


Wakati mwanamke Mkristo anatafuta mume, yeye anapaswa kutafuta mume "atakaye upenda moyo wangu" (Matendo 13:22). uhusiano muhimu zaidi ambao mtu yeyote kati yetu anaweza kuwa nao ni uhusiano na Bwana Yesu Kristo. Uhusiano huo huja kabla ya wmingine wote. Kama uhusiano wetu wima na Bwana uko vile unafaa uwe, basi uhusiano wetu usawa utadhihirisha ukweli huo. Kwa hiyo, mume kamili lazima awe mtu ambaye mtazamo wake uu katika kutembea katika kutii neno la Mungu na ambaye anataka kuishi hivyo, ili maisha yake yaleter utukufu kwa Mungu (1 Wakorintho 10:31).

Ni nini baadhi ya sifa nyingine unapaswa kuangalia? Mtume Paulo anatupa sisi sifa tunapaswa kuangalia katika mume katika 1 Timotheo sura ya 3. Katika fungu hili kuna sifa kwa kiongozi katika kanisa. Hata hivyo, sifa hizo lazima zineemaeshe maisha ya mume yeyote ambaye anatembea "katika kumpenda Mungu." Sifa zinaweza kufafanuliwa kama ifuatavyo: mtu anatakiwa kuwa na subira na kudhibitiwa katika mwenendo wake, si wa kujazwa na kiburi lakini mwenye mawazo kiasi, akiwa na uwezo wa kudhibiti hisia zake, kutokana na neema kwa wengine, kwa uvumilivu anafundisha, sio wa kutumia mvinyo au wa kutumia karama za Mungu bila mpango, si wa vurugu, asiye yadhamini maisha ya kawaida tu, bali anamtizamia Mungu, asiye mkaidi au kuwa mkonde ili kufanya makosa kwa urahisi, na wa kushukuru kwa kile ambacho Mungu amewapa, badala ya kuona wivu kwa vipawa vya wengine wamepokea.

Sifa za hapo juu zaelezea mtu ambaye anajihuzisha kikamilifu katika mchakato wa kuwa muumini mkomavu. Huyo ni aina ya mtu mwanamke inapaswa kuangalia kama mume kamili. Naam, kivutio cha kimwili, maslahi sawia, uwezo nyongeza na udhaifu, na hamu ya watoto ni mambo ya kuzingatia. Mambo haya, ingawa, lazima yawe ya pili baada ya sifa za kiroho ambazo mwanamke anapaswa kuangalia katika mume. Mume unaweza mwamini, heshimu, na kufuata katika njia ya utauwa ni wa thamani kubwa zaidi kuliko mume anayeonekana vizuri, maarufu, wa nguvu, au fedha.

Hatimaye, wakati "unamtafuta" mume, ni lazima tujizalimishe kwa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Kila mwanamke anatamani kupata mume wake "wa haiba mkuu," lakini ukweli ni kwamba yeye pengine huolewa na mume aliye na adhaifu mwingi sana vile yeye ana. Basi, kwa neema ya Mungu, watatumia wakati wote pamoja kujifunza jinsi ya kuwa na mapenzi, na watumishi wa kila mmoja. Ni lazima kuingia katika uhusiano muimu wa pili zaidi ni uhusiano wa maisha yetu (ndoa), si chini ya wingu la hisia, lakini macho yakiwa yamefunguka. Uhusiano wetu muhimu zaidi, na Bwana na Mwokozi wetu, lazima uwe lengo la maisha yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninafaa kuangalia nini katika mume?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries