Swali
Je, ni makosa kutamani kitu?
Jibu
Kutamani ni hali ya kuwa binadamu. Mungu aliumba wanadamu na hisia na shauku. Tunapotamani kitu, tunakubali kwamba kuna kitu nje ya udhibiti wetu ambacho tunatamani sana. Katika ufunuo 3:15 Yesu anasema, “Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa moja au linguine.” Aliwapa wanadamu hiari huru ya kuchagua na kwa kuwaumba hivyo, anaturuhusu kimakusudi uhuru wa kumchagua au la. Alipokuwa duniani, Yesu alionyesha “tamaa” ingine aliposema, “Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa” (Luka 12:49). Alijua kuwa kusulubishwa kulikuwa karibu, na baada ya hapo angemimina Roho Mtakatifu juu ya wafuasi wake (Matendo 1:8). Yesu alitamani sana kumtuma Roho, lakini alijua ilimbidi kwanza apatwe na hofu ya kusulubishwa. “Matakwa” yake hayakuwa mabaya. Hiyo ni kuwa binadamu.
Tamaa inaweza kuwa mtangulizi wa mabadiliko. Ikiwa matakwa yanategemea ukweli na mabadiliko mazuri, inaweza kuwa lengo na kisha uhalisi. Ingawa matamaa yanaweza kuwa na makosa ikiwa tunayatanguliza mbele ya mpango wa Mungu kwa ajili yetu. Wakati Yesu, kule Gethsemane, “alipotamani” kwamba Baba Yake angetafuta njia nyingine ya kuwakomboa wanadamu, Hakumalizia maombi yake hapo. Hakuruhusu tamaa Yake ya kibinadamu kutawala mapenzi ya Mungu. Alishindana kieleke ndani ya roho yake hadi alipoweza kusema kwa ukweli, “Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke” (Luka 22:42).
Tamaa inaweza kuwa mbaya ikiwa matamaa yetu yanaelekezwa kwa kitu kingine isipokuwa Mungu Mwenyewe. “Kutamani nyota” kunaweza kuwa na mvuto wa kimapenzi, lakini nyota haiwezi kusaidia mtu yeyote. Ni lazima tutegemee Muumba wa nyota kwa ajili ya majibu ya sala, sio nyota zenyewe.
Tamaa pia linaweza kuwa baya ikiwa lengo la tamaa hiyo ni dhambi. Kwa mtu aliyeolewa kutamani mwenzi wa mtu mwingine ni makossa (kumbukumbu 5:21). Kutamani sana vitu vingi vya kimwili au kutamani pesa zaidi ya unayohitaji ni makosa (Mithali 23:4; 1 Timotheo 6:9-10). Tamaa inapotegemea kutoridhika na yale ambayo Mungu ameagiza kwa ajili yetu kabila, taifa, aina ya mwili, au familia-ni tamaa mbaya. Hitaji letu halisi ni kujifunza kushukuru kwa kile ambacho Mungu ametupa na kujifunza kutumia kila kitu kwa utukufu na kusudi lake (1 Wakorintho 10:31; Wakolosai 3:16).
Zaburi 37:4 inasema, “Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.” Wakati kumpendeza Bwana ni furaha yetu kuu, Yeye hurekebisha matamaa yetu. Anabadilisha matamaa ya mioyo yetu ili kupatana na matamaa Yake kwetu-matamaa Yake huwa yetu ili kwamba tunatamani mambo yanayomfurahisha. Katika mchakato huo, tunajikuta tumefurahi. Tunaweza kuomba kwa ujarisi, kulingana na mapenzi yake, wakati tunajua kwamba tunataka kile anachotaka. Tunapotamani mambo yanoyoendana na mpango wake, tunaweza kuomba kwa ujarisi kwamba anasikia na atatujibu (Yohana 15:7; 1 Yohana 5:14; Mathayo 21:22).
Hakika Biblia inatuamuru tutamani hekima (Mithali 24:14), karama za kiroho (1 Wakorintho 14:1), Siku ya Bwana (2 Petro 3:12), kufunuliwa kwa mwisho wa watoto wa Mungu ni nani (Warumi 8:19), na wokovu wa wengine (Warumi 10:1). Wakati kiini cha matamaa yetu ni matamaa ya Mungu, tunaweza kumwomba Mungu hayo kwa imani. Wakati tuna mtazamo wa kimbingu, matamaa yetu yanatakazwa, “Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:15).
English
Je, ni makosa kutamani kitu?