Swali
Ina maana gani kutembea na Mungu?
Jibu
Kuna watu wengi waliolezwa kama “wanaotembea na Mungu” katika Biblia,kuanzia Henoko katika Mwanzo 5:24. Nuhu pia anaelezwa kuwa “ mtu wa haki,mkamilifu katika vizazi vyake, Nuhu alikwenda pamoja na Mungu”( Mwanzo 6:9). Mika 6:8 inatupa ufahamu wa mapenzi ya Mungu kwetu: “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.”Kutembea na Mungu si shughuli iliyohifadhiwa kwa wachache wateule. Mungu anatamani watoto wake wote watembee na Yeye.
Nini hufanyika tunapotembea na mtu? Fikiria wewe na rafiki yako ya karibu mnajifurahisha kutembea kando ya barabara ya vijijini. Mko karibu. Mnazungumza, mnacheka, mnasikiliza na kushirikiana yaliyo mioyoni. Umakini wako wote umeelekezwa kwa mtu huyu kwa kutenga karibu kila kitu kingine. Unachunguza uzuri unaokuzunguka au vikwazo vya mara kwa mara, lakini unavyoona unamwonyesha rafiki yako. Mnashirikiana pamoja. Mko katika usawa, na nyote mnafurahia ushirika wa amani.
Kutembea na Mungu ni kama mfano huo. Tunapojiingiza katika uhusiano wa karibu wa moyo na Mungu kupitia imani kwa Mwana wake ( Waebrania 10:22), Yeye anakuwa tamanio kuu la moyo wetu. Kumjua Yeye, kusikia wito wake, kushiriki mioyo yetu naye,na kutafuta kumpendeza Yeye ndilo lengo letu kuu. Yeye anakuwa kila kitu kwetu. Kukutana naye si shughuli iliyotengwa kuwa ya Jumapili pekee. Tunaishi kutafuta ushirika na Yeye. A.W Tozer anasema kuwa lengo la kila Mkristo linafaa kuwa “ kuishi katika hali ya ibada isiyovunjika.” Hili litawezekana tu ikiwa tunatembea na Mungu.
Kama vile kutembea na rafiki wa karibu kunahitaji kusema “hapana” kwa mambo mengine mengi, vivyo hivyo kutembea na Mungu kunahitaji kuachana na chochote kinachoweza kutuzuia kutembea naye. Ikiwa uko matembezi na rafiki yako lakini ulikuja na kazoo na kuicheza wakati huo wote, matembezi hayo hayatakuwa ya kuridhisha kwa yeyote kati yenu. Wengi hujaribu kutembea na Mungu, lakini huleta mazoea kama ya kazoo, dhambi, burudani za kidunia, au mauhusiano yasiyo ya kiafya. Wanajua vitu hivi sio uchaguzi wa Mungu kwao, lakini wanajifanya kila kitu kiko sawa. Uhusiano huo sio wa kuridhisha kwa yeyote kati yao. Kutembea na Mungu kunamaanisha kwamba wewe na Mungu mnakubaliana juu ya maisha yako. “Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” ( Amosi 3:3 ). Kutembea na Mungu kunamaanisha kwamba umekubaliana mapenzi yako na Yake kuambatana na kujitahidi kila siku kuona wewe ni “msulubiwa pamoja na Kristo”( Wagalatia 2:20). Haufai kuwa mkamilifu,kama vile hakuna mmoja wetu ambaye ni mkamilifu ( Warumi 3:10). Lakini tamaa ya moyo wako iwe ni kumfurahisha Mungu, na ukue tayari kuacha Roho yake ikufinyange uwe sawa na mfano wa Mwana wake ( Warumi 8:29).
Biblia inapozungumza juu ya “kutembea,” mara nyingi inaashiria mtindo wa maisha. Tunaweza kutembea katika njia za ulimwengu pia (2 Wafalme 8:27; Waefeso 2:2; Wakolosai 3:7). Katika Agano jipya, kutembea na Mungu mara nyingi huitwa “ kutembea kwa Roho” ( Wagalatia 5:16; Warumi 8:4). Kutembea na Mungu kunamaanisha kuwa tunachagua kumtukuza Yeye kwa njia zote tunazoweza, bila kujali gharama ya kibinafsi. Na kuna gharama. Kutembea na Mungu pia ina maana kuwa hatuwezi tembea na watu waovu kama marafiki ( Zaburi 1:1-3). Tunachagua njia nyembamba badala ya njia pana ya uharibufu ( Mathayo 7:13-14). Hatuishi kwa kufurahisha mwili wetu wa dhambi ( Warumi 13:14). Tunatafuta kuondoa kila kitu katika maisha yetu ambacho hakitufanyi kutembea pamoja na Yeye (Waebrania 12:2). Tunatumia 1 Wakorintho 10:31 kwa ukamilifu: “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.”Njia za Mungu zinaonyeshwa katika mawazo yetu, matendo yetu, motisha zetu, na maamuzi yetu ya maisha kwa sababu tunatumia muda mwingi pamoja Naye.
Si vigumu kuwatambua watu ambao wanatembea na Mungu. Maisha yao ni tofauti kabisa na yale ya ulimwengu unaowazunguka, kama nyota katika anga la usiku ( Wafilipi 2:15). Wao huzaa matunda ya Roho ( Wagalatia 5:22-23) badala ya matunda ya tamaa ya mwili ( Wagalatia 5:19-21). Katika Matendo ya Mitume 4:13 Petro na Yohana walikamatwa kwa sababu ya kuhubiri na kuletwa mbele ya mamlaka. “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.” Tunapotembea na Mungu kila siku,ulimwengu hauwezi kutoa shahidi kwamba, licha ya udhaifu wetu na ukosefu wa maarifa katika maeneo fulani, tumekuwa pamoja na Yesu.
English
Ina maana gani kutembea na Mungu?