Swali
Je! Ninawezaje kuushinda ubaya kwa wema (Warumi 12:21)?
Jibu
Warumi 12:21 inasema, “Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.” Mstari huu unafuata mawaidha kama vile “Wabarikini wale wanaowatesa” (aya ya 14) na “Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu” (aya ya 17). Maudhui ya kifungu ni jinsi ya kupenda kwa uaminifu (mstari wa 9), na maagizo yanatuhitaji kuweka kando mielekeo yetu ya asili. Njia za Mungu daima zinatia changamoto asili yetu ya kimwili na zinatuita kuishi katika ngazi ya juu kwa nguvu za Roho. Njia ya kibinadamu ni kuwalaani wale wanaotulaani na kujaribu kushidna uovu kwa uovu zaidi. Lakini, kulingana na Warumi 12:21, tunaweza tu kuushinda ubaya kwa wema. Wema wa Mungu una nguvu kuliko uovu wowote.
Yesu alikuwa kielelezo kikamilifu cha kuushinda uovu kwa wema: “Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutishia, bali alijikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki” (1 Petro 2:23). Katika kujisalimisha kwa uovu wa watekaji wake, alishinda dhambi, Shetani, na mauti (Waefeso 4:8-10). Uovu ulifikiri ulishinda siku ile ulipomsulubisha Kristo msalabani. Lakini kwa sababu Yesu alijitoa kikamilifu kwa mapenzi na mpango wa Baba yake, Mwana wa Mungu alishinda uovu wao kwa wema. Ingawa matendo dhidi ya Kristo yalikuwa maovu yenyewe, kifo cha Yesu na ufufuo wa baadaye ulishinda uovu huo kwa kununua msamaha na uzima wa milele kwa kila mtu ambaye angeamini (Yohana 1:12; 3:16-18; 20:31).
Tunashinda ubaya vivyo hivyo kwa wema. Bwana anasema kuwa kisasi ni chake na atalipiza (Waebrania 10:30). Tunaweza kujikabidhi kwa Mungu, vile Yesu alivyofanya, na kujua kwamba atafanya kazi kwa hata matendo maovu yaliyotendwa dhidi yetu kwa manufaa yetu (Mwanzo 50:20; Warumi 8:28). Tunapokataa kulipiza kisasi kwa wale wanaotutesa, matendo yao maovu yanasimama peke yake, ilhali kulipiza kisasi kunatushusha kwenye ngazi ya wachochezi. Wakati watu wawili wanapigana, na mmoja anamshambulia mwingine waziwazi, uovu unawekwa wazi kwa watu wote kuona. Wakati tunajibu kwa neno la upole, au ukarimu kwa mtu aliyetukosea, tunamwacha mtenda uovu peke yake katika uovu wake.
Mithali 25:21-22 inasema, “Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale; kama ana kiu, mpe maji anywe. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye Bwana atakutuza.” Paulo ananukuu kifungu hiki katika Warumi 12:20, kabla ya amri yake ya “kuushinda ubaya kwa wema.” “Unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.” labda inarejelea mwitikio wa asili kwa adui kwa fadhili. Hakuna kitu kinachotufanya tuhisi haya na kuhaibika kwa matendo yetu kuliko mtu kujibu tabia yetu ya kuumiza kwa msamaha wa upole. Kuonyesha fahdili mahali pa makosa, kunaonyesha tofauti kubwa kati ya mambo hayo mawili. Lengo la mwitikio wa upole kwa adui si kuaibisha au kupata neno la mwisho bali ni kusaidia kurahisisha toba kwa mtenda maovu.
Ikiwa tutakumbuka mambo machache muhimu, tunapiga hatua katika kuushinda ubaya kwa wema:
1. Mimi si mwamuzi; Mungi ndiye mwamuzi. Atafanya yaliyo ya haki (Mwanzo 18:25).
2. Kama Mkristo mwitikio wangu kwa ubaya haupaswi kuiga tabia ya ulimwengu, bali kuakishi Kristo, aliye ndani yangu (Warumi 12:1-2).
3. Kuangazia Yesu Kristo kunanisaidia kujua jinsi ya kujibu wakati ninafanyiwa vibaya (Waebrania 12:2).
4. Mungu daima ananitazama na kutathmini maamuzi yangu, na Anataka kunitunuku kwa kumtii Yeye (Mathayo 5:43-38).
Yesu aliwakumbusha Mafarisayo kwamba Shetani hawezi kumfukuza Shetani (Mathayo 12:25-28). Vivyo hivyo, uovu hauwezi kufukuza uovu. Jibu la uovu huzidisha uovu. Wakati tunajibu uovu kwa unyenyekevu na neema, tunathibitisha kwamba wema hushinda uovu. Hatuwezi kuwazuia watu kutufanya maovu, lakini hawawezi kutulazimisha kushiriki nao. Haihitaji nguvu, uwezo, au hekima kulipiza kisasi dhidi ya watenda maovu. Lakini kurudisha wema kwa ubaya ni mojawapo ya dhihirisho kubwa la ukomavu.
English
Je! Ninawezaje kuushinda ubaya kwa wema (Warumi 12:21)?