Swali
Je! Ni nini maana ya kuwa binadamu?
Jibu
Mungu amewaumba wanadamu tofauti na viumbe vingine vyote. Wanadamu wana mwili na sehemu ya kiroho: nafsi na roho. Sehemu ya kipengele hiki kisio cha mwili ni milki ya akili, hisia, na mapenzi. Wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Wanadamu wako tofauti sana na malaika, ambao hawana mwili halisi, na wanyama ambao hawana mfano wa Mungu.
Kunayo mitazamo tofauti ambayo sio ya kibiblia juu maana ya kuwa binadamu. Kwa mfano dini ya Kinostiki ina mtazamo kwamba mwanadamu kimsingi ni mtu safi, kiumbe cha kiroho ambaye ameunganishwa na mwili mpotovu. Mitazamo mingine, kama vile ausilia, unaona mwanadamu kuwa kifaa changamani, kisicho na roho hata kidogo-hisia na mawazo, au misukumo yoyote tunayopata ni matokeo ya athari za kemikali ndani ya akili zetu. Kati ya mitizamo hii hakuna ule ulio na uungwaji mkono wa Biblia.
Kuwa mwanadamu inamaanisha kuwa na mfano wa Mungu. Sisi sio viumbe takatifu, bali tunaakisi uungu. Mungu ana akili, hisia, na hiari. Kama wenye mfano wa Mungu sisi pia tuna akili, hisia na nia. Tunamiliki ubunifu, uvumbuzi, utungaji, usanaa, kutengeza wimbo, kuunda aina zote za kazi za sanaa. Tuna karama ya lugha inayohususha wazo kutoka kwa akili ya kujitambua kwa nyingine, kufunza maelfu ya maneno na kubuni maneno mapya wakati tunayahitaji. Tunaainisha na kuwapa wanyama majina, kama vile baba yetu Adamu alifanya (Mwanzo 2:19-20). Kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, tuna hadhi ya kimsingi na umuhimu wa asili.
Kuwa mwanadamu inamaana ya kuwa na kusudi. Jukumu la Mungu lililotajwa kwa Adamu na Hawa lilikuwa “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi” (Mwanzo 1:28). Bado tunalitimiza kusudi hili wakati tunawafuga mifugo nyumbani, kutumia rasilimali, na kuunda asili, na kutengeza maisha hata katika mazingira magumu zaidi bado. Lakini sisi ni zaidi ya waangalizi wa anga. Lengo letu linajumuisha kumjua Mungu na kuwa na uhusiano na Yeye. Kusudi letu kuu ni kumtukuza Mungu: “vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake” (Wakolosai 1:16).
Kuwa mwanadamu ni kuwa na mahitaji. Ni Mungu pekee anaweza kujikidhi. Tuna mahitaji ya kimwili, nafsi na roho. Miili yetu lazima ipate chakula, kinywaji na kupumzika ili kuishi. Nafsi zetu lazima ziwe na ushirika na wengine, njia za ubunifu, na nyakati za msisimuko wa akili, hisia ili tuwe na afya ya akili. Roho zetu lazima zilishwe Neno la Mungu na kuwa na uhusiano na Kristo (Luka 4:4; Yohana 6:35). Mtu yeyote anayekataa mahitaji yake katika mojawapo ya hizi sehemu tatu anakataa kukubali sehemu yake ubinadamu.
Kuwa binadamu maana yake ni kuwajibika kimaadili. Tuna uwezo wa kutambua lililo sahihi na lisilo sahihi. Baba yetu Adamu alikuwa na hiari huru na aliwajibika kwa uamuzi wa kiadili alioufanya wa kutii au kutotii muumba wake; kwa bahati mbaya, alichagua kutomtii Mungu (Mwanzo 2:16-17). Binadamu wote wana jukumu hilo la kiadili, na sisi wote tuko chini ya sharti sawia la kumtii Mungu. “Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake” (Ezekieli 18:20).
Kuwa mwanadamu humaanisha kuwa mwenye dhambi, angalau kwa sasa. Kwa bahati mbaya, sisi wote ni wenye dhambi (Warumi 3:23; 5:12). Tumevunja sheria za Mungu na badala yake kugeukia njia zetu wenyewe (Isaya 53:6; 1 Yohana 3:4). Dhambi yetu imetutenganisha na Muumba wetu na kutufanya tufe kiroho (Waefeso 2:1-10). Sisi ni watumwa wa dhambi, na hatuna uwezo wa kujiweka huru sisi wenyewe kutoka kwa uharibifu unaosababishwa (Warumi 6:23). Bila kuingilia kati, sisi tumehukumiwa milele kuwa mbali na Mungu (Yohana 3:16-18). Kwa sifa na utukufu kwa Mungu, hatupaswi kusalia katika hali hii. Kuna ukombozi unaopatikana katika Kristo Yesu. Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu msalabani, dhambi zetu zinaweza kusamehewa, na tunaweza kurejeshwa katika uhusiano na Mungu (Yohana 3:16-18; Waefeso 2:8-9). Kuwa mwanadamu inamaanisha kupendwa na kupewa nafasi ya kuwa wana Mungu (Yohana 1:12; 3:16).
Biblia inasema kwamba Mwana wa Mungu aliutwaa mwili wa mwanadamu na akawa mwana wa Adamu vile vile. Yesu Kristo alikuja kutoka mbinguni, akaishi maisha yasiyo na dhambi, akafa msalabani kama dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu, na kisha akafufuka tena. Wote wanaoweka imani yao katika Kristo wanapewa haki ya Mungu (2 Wakorintho 5:21). Tumefanywa upya (2 Wakorintho 5:17), na Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu (Waefeso 1:13-14). Ni kifo na ufufuo wa Kristo ambao hufanya tofauti kwa wanadamu.
Mwishowe, kuwa mwanadamu haitoshi. Uadamu unaharibiwa na dhambi na unakumbana na hukumu ya kweli ya Mungu. Ni wale tu walio katika Kristo watapata kuondolewa kwa uharibifu na kufutwa kwa kila chozi. “Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona Ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili” (Yohana 3:3).
English
Je! Ni nini maana ya kuwa binadamu?