settings icon
share icon
Swali

Je, kuwepo kwa Mungu mmoja kunaweza thibitika?

Jibu


Neno “monotheisimu” (kuwepo kwa Mungu mmoja) linatokana na maneno mawili, “mono” (moja) kumaanisha “udogo” na “theisimu” (uungu) maana yake imani katika Mungu. Hasa, monotheisimu ni imani katika Mungu mmoja wa kweli ambaye ni Muumba wa viumbe wote. Monotheisimu hutofautiana hali na ya kuwa na imani katika miungu, ambayo ni imani katika miungu wengi na akiwepo Mungu mkuu juu ya wote. Pia ni kinyume na ushirikina, ambayo ni imani katika kuwepo kwa mungu zaidi ya moja.

Kuna hoja nyingi kwa monotheisimu, ikiwa ni pamoja na wale wa kutoka ufunuo maalum (maandiko), ufunuo asili (falsafa), kama vile masuala ya kihistoria. Haya tu yataelezwa tu kwa ufupi hapa chini, na hii isichukuliwe kuwa orodha nzima.

Hoja ya Kibibilia kuhusu Monotheisimu ni: Kumbukumbu la Torati 4:35: “Wewe ulionyeshwa mambo haya ili upate kujua ya kuwa Bwana ni Mungu; badala yake hakuna mwingine.” Kumbukumbu 6:4 “Sikieni, enyi Israeli, Bwana Mungu wetu Bwana ni mmoja.” Malaki 2:10a, “Je, sisi zote hatuna Baba mmoja? Je, si Mungu moja alituumba? 1 Wakorintho 8:6 “Hata hivyo kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka na kwa ajili yake sisi tunaishi; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye kupita kwake vitu vyote vinatoka na ambaye kwa njia yake sisi tunaishi. Waefeso 4:6: “Mungu Mmoja na Baba wa vyote, ambaye ni juu ya yote na katika yote na ndani ya wote.” 1 Timotheo 2:5: “Maana yuko Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, amabaye ni Kristo Yesu.” Yakobo 2:19: “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja. Ni vyema, hata mapepo wanaamini kwamba kuna Mungu mmoja na hutetemeka kwa hofu.”

Ni wazi, kwa watu wengi kuwa, haitoshi kusema kwamba kuna Mungu mmoja tu, kwa sababu Biblia inasema hivyo. Hii ni kwa sababu bila Mungu hakuna njia ya kuthibitisha kwamba Biblia ni neno lake katika nafasi ya kwanza. Hata hivyo, mtu anaweza kusema kwamba tangu Biblia ina ushahidi zaidi wa kuaminika usio wa kawaida kuthibitisha yale inayofundisha, umonotheisimu waweza thibitishwa kwa misingi hii. Hoja kama hiyo itakuwa sawa na imani na mafundisho ya Yesu Kristo, ambaye imeonekana kuwa alikuwa Mungu (au angalau kitu cha mwisho kuithinishwa na Mungu) kwa kuzaliwa kwake kwa muujiza, maisha, na muujiza wa ufufuo wake. Mungu hawezi nena uongo au kudanganywa, kwa hivyo, chenye Yesu aliamini na kufundisha ni kweli. Kwa hiyo, umonotheisimu, ambao Yesu aliuamini na kufundisha, ni wa kweli. Hoja hii inaweza kuwa ya kuvutia sana kwa wale wasio na ufahamu wa uthibitisho wa kiroho wa maandiko na Kristo, lakini hii ni sehemu nzuri ya kuanzia kwa aliye na ufahamu wa nguvu zake.

Hoja ya kihistoria kuhusu umonotheisimu ni hoja ambayo msingi wake ni wa umaarufu wa juu mno kutuhumiwa, lakini ni kitu cha kuvutia kiasi ambacho umonotheisimu umeathiri dini za dunia. Nadharia maarufu ya mabadiliko ya maendeleo ya kidini inatokana na mtazamo badiliko wa hali halisi kwa ujumla, na asili ya mabadiliko ya utu ambayo inaona “ufinyu” wa tamaduni kama zinawakilisha hatua za awali za maendeleo ya kidini. Lakini matatizo ya haya mabadiliko nadharia ni kadhaa. 1) aina ya maendeleo inayoelezea haijawahi onekana, kwa kweli, inaonekana hakuna maendeleo zaidi kuelekea umonotheisimu ndani ya utamaduni wowote, kinyume inavyoonekana kuwa halisi. 2) ule mtindo wa kusomea asili ya tamaduni, kisasi na mira za watu wafafanua “ufinyu” unalinganisha maendeleo ya teknolojia, lakini vigumu kigezo hiki kuridhisha kwa vile kuna vipengele vingi vya utamaduni huo. 3) hatua zinazokisiwa mara nyingi hukosa au kurukwa. 4) Hatimaye, tamaduni nyingi washirikiana kuonyesha uhalisi wa monotheisimu mapema katika maendeleo yao.

Tunachokiona ni Mungu mmoja ambaye ni wa ubinafsi, na wa kiume, anaishi katika anga, ana ujuzi mkubwa na nguvu, aliumba ulimwengu, ni mwandishi wa maadili ambayo sisi tunawajibikia, na ambaye sisi tumemuasi na hivyo tumemetengwa kutoka kwake, lakini pia ametoa njia ya maridhiano. Karibu kila dini hubeba tofauti ya huyu Mungu katika wakati tofauti kabla ya kupelekwa katika machafuko ya ushirikina. Hata hivyo, inaonekana kwamba dini nyingi zimeanzia katika kuabudu Mungu mmoja na “kuendelea” katika ushirikina, na uchawi. (Uislamu ni baadhi ya kesi chache sana, baada ya kuja kwa mzunguko kamili wa imani ya Mungu mmoja.) Hata kwa harakati hii, ushirikina ni mara nyingi wajidhihirisha wazi kwa Mungu mmoja au imani kwa Mungu mmoja bila kukataa miungu mingine. Ni nadra sana dini za ushirikina ambazo hazishikilii mmoja wa miungu yake kuwa huru juu ya mapumziko, pamoja na miungu midogo kazi huwa ni kupatanisha.

Hoja za kafalsafa / Kibibilia kuhusu uungu mmoja, kunazo hoja nyingi za kifalsafa za kutokuwa na uwezekano ya kuwa kuna Mungu zaidi ya mmoja katika kuwepo kwa Mungu mmoja. Wingi wa hizi hoja za kimsingi hutegemea mpango mkubwa juu ya nafasi ya mtu na juu ya asili ya ukweli. Kwa bahati mbaya, katika nakala hii fupi itakuwa vigumu kupinga kwa ajili ya nafasi hizi za kimsingi cha elimu ya juu zaidi na kisha kwendelea kuonyesha hasa ni nini wanaashiria kuhusu uungu mmoja, lakini baki ukijua kwamba kunoa hoja za nguvu kifalsafa na kiteolojia ambazo zinaupa msingi ukweli huu ambao unarejelea milenia (Na wingi wa hizi hujidhihirisha dhahiri). Kwa ufupi, basi, hapa kunao hoja tatu mtu anaweza kuchagua moja na kuichunguza:

1. Kama kulikuwa na Mungu zaidi ya mmoja, ulimwengu ungekuwa katika machafuko kwa sababu ya wabunifu wengi na mamlaka, lakini siyo katika machafuko, kwa hiyo, kuna Mungu mmoja tu.

2. Tangu Mungu ni kiumbe kamili, kamwe hakuwezi kuwa na Mungu wa pili, kwa sababu wangekuwa tofauti katika baadhi ya njia, na kuwa tofauti kwa ukamilifu hiyo ni kuwa chini ya kamilifu na kukosa kuwa Mungu.

Tangu Mungu hana mwisho wake, hawezi kuwa na sehemu (kwa ajili ya sehemu haziwezi kujumlishwa kufikia umilele). Kama kuwepo kwa Mungu si sehemu kwake (ambayo ni kwa ajili ya mambo yote ambayo inaweza kuwa na kutokuwepo au kisicho na uhai) basi lazima awe na mwisho usio na kikomo. Kwa hivyo, hakuwezi kuwa viumbe wawili wasio na mipaka, kwa sababu mmoja kazima awe tofauti na mwingine.

Mtu anaweza taka kupinga kwamba wingi wa hizi utakuwa si utawala wa kikundi kidogo cha “miungu,” na kwamba hiyo ni mzuri. Ingawa tunajua kuwa huu si ukweli wa Bibilia, hakuna kitu kibaya kwa kuwa na dhana kama hii. Kwa njia nyngine, Mungu angeweza kuumba kikundu vidogo vyan “miungu,” lakini ilitokea tu kuwa hakutaka kufanya hivyo. Kama ingekuwa hivyo, hizi “miungu” zingekuwa na upungufu, aliumba vitu vingine vingi kama malaika (Zaburi 82). Hii haina madhara kwa kesi ya umonotheisimu (uungu umoja), ambayo haisemi kwamba hakuwezi kuwa na viumbe vyovyote vya kiroho ni vile tu kwamba hakuwezi kuwa na Mungu zaidi ya moja.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuwepo kwa Mungu mmoja kunaweza thibitika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries