settings icon
share icon
Swali

Je! Ikiwa tulizaliwa katika dhambi, je, kuna haki gani kwa Mungu akituhukumu kwa ajili ya dhambi zetu?

Jibu


Mashtaka ya kwaida dhidi ya Ukristo ni kwamba unahukumu watu kwa njia isiyo ya haki. Hasa, baadhi ya watu husema kwamba Mungu hutuachilia kwa majaribu na kisha hutuadhibu kwa makossa Aliyoyasababisha. Ikiwa hiyo ni kweli, ingekuwa hali isiyo ya haki. Je! hivyo ndivyo Ukristo unavyofanya kazi? Je, Mungu anatuhukumu kwa njia isiyo ya haki kwa jambo ambalo hatuna uwezo nalo? Majibu yanapatikana katika Biblia.

Kwanza, ni lazima tujue Biblia inasema nini kuhusu kuzaliwa kwetu katika dhambi. Daudi, mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu mwenyewe aliandika katika Zaburi 51:5, “Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.” Mtume Paulo aliandika kwamba sisi sote tunatimiza “tamaa za asili yetu ya dhambi” (Waefeso 2:3). Hiyo inamaanisha, kiasili kuna kitu ndani yetu ambacho hutusukuma katika dhambi.

Hakika Biblia inafunza kwamba tunazaliwa katika dhambi. Je! Mungu aliamua kiholela kwamba watu wangezaliwa wakiwa wenye dhambi? Jibu linapatikana kuhusiana na mwanadamu wa kwanza, Adamu. Adamu alipoumbwa (bila dhambi) na Mungu na kuwekwa katika bustani mwa Edeni, pia alipewa sheria rahisi (Mwanzo 2:16-17). Adamu aliasi sheria ya Mungu, na Mungu akamtangaza kuwa na hatia na kumhukumia kifo. Uamuzi wa Adamu wa kutotii ulimfanya awe na hatia mbele za Mungu. Alikuwa baba wa jamii ya kibinadamu, na tabia zake zilipitishwa kwa watoto wake. Warumi 5:12 inasema kwamba dhambi iliingia ulimwenguni kupitia Adamu, na kifo kilikuja kupitia dhambi, kwa sababu wote walifanya dhambi. Kama wazao wa Adamu, tulipokea asili ya dhambi iliyopitishwa kutoka kwa baba zetu. Hilo hutufanya tuzaliwe katika dhambi, tukiwa na mwelekeo wa asili wa kufanya makosa.

Wengine wanaweza bishana kwamba hatuwezi kuchagua familia yetu, kwa hivyo Mungu hawezi kutuwajibisha kwa asili ya dhambi. Huku huenda hatuna chaguo lolote kuhusu jinsi tunavyozaliwa, Biblia iko wazi kwamba tuna chaguo kuhusu dhambi zetu. Hapo awali, tulisoma andiko la Waefeso 2:3, linalosema kwamba tunatosheleza tamaa za asili yetu ya dhambi. Huo ni uchaguzi. Warumi 5:12 inasema kwamba “wote wametenda dhambi.” Sisi ni wenye dhambi kwa matendo na pia kwa asili. Dhambi yetu wenyewe ndio inatuhukumu, na si ya dhambi ya Adamu tu. Tumezaliwa katika dhambi, lakini tunaendelea kutenda dhambi kwa uchaguzi wetu binafsi. Tunapochagua dhambi, tunakuwa na hatia mbele za Mungu, na hukumu yake ni ya haki.

Mungu si wa haki tu pekee, bali ni mwenye rehema. Mafundisho ya Biblia kuhusu dhambi ya kibinafsi hayaishii kwa tangazo la hatia ya mwandamu. Warumi 5, ambayo inatuambia kwamba dhambi na kifo viliingia ulimwenguni kupitia mtu mmoja, pia inatuambia juu ya baraka kubwa zaidi, ambayo pia ilikuja kupitia kwa mtu mmoja. Karama ya Mungu ya neema ilikuja kwa njia ya Yesu Kristo (Warumi 5:15) na ikajawa kwa wengi. Aya ya 19 inasema, “Kwa maana kama vile kwa kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.” Mungu ni mwenye haki katika kuadhibu dhambi ya Adamu kwa jamii yote ya wanadamu, na yuko haki katika kutumia kifo cha Yesu Kristo kwa wote ambao watampokea kwa imani. Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, ili ulimwengu upate uzima kwa imani katika dhabihu yake. Hiyo sio “haki”-hiyo ni neema!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ikiwa tulizaliwa katika dhambi, je, kuna haki gani kwa Mungu akituhukumu kwa ajili ya dhambi zetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries