settings icon
share icon
Swali

Je, ni namna gani milele katika moto wa Jehanamu ni adhabu ya haki kwa ajili ya dhambi?

Jibu


Hili ni suala kwamba ambalo huwasumbua watu wengi walio na uelewo usiokamilika wa mambo matatu: asili ya Mungu, asili ya mwanadamu, na asili ya dhambi. Kama binadamu wa dhambi, asili ya Mungu ni dhana ngumu kwtu kufahamu. Sisi huwa tunamwona Mungu kama mpole na wa huruma ambaye mapenzi yake kwa ajili yetu yanapewa kipaumbele na hupita sifa zake zote. Bila shaka Mungu ni upendo, mpole, na wa huruma, lakini Yeye ni wa kwanza na zaidi ya hayo ni mtakatifu na Mungu wa haki. Hivyo mtakatifu ni Yeye Yule hawezi kuruhusu dhambi. Yeye ni Mungu ambaye hasira yake ni nzito dhidi ya waovu na waasi (Isaya 5:25; Hosea 8:5; Zakaria 10:3). Yeye si tu Mungu wa upendo pekee -Yeye mweneyewe ni upendo! Lakini Biblia pia inatuambia kwamba anachukia kila aina ya dhambi (Mithali 6:16-19). Na wakati Yeye ni mwenye huruma, kuna mipaka katika rehema yake. "Mtafuteni Bwana maadamu anapatikan, mwiteni maadamu yu karibu; Mtu mbay na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake na amrudie Bwana naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa." (Isaya 55:6-7).

Mwanadamu amepotoshwa na dhambi, na kwamba dhambi daima moja kwa moja asi dhidi ya Mungu. Wakati Daudi alitenda dhambi kwa kufanya uzinzi na Bathsheba na kumfanya Uria kuuawa, yeye alijibu kwa sala ya kuvutia: "Nimekutenda dhambi Wewe peke yako na kufnay maovu mbele za macho yako … " (Zaburi 51:4). Tangu Daudi alikuwa amekwisha tenda dhambi dhidi ya Bathsheba na Uria, ni jinsi gani yeye anawezaa kudai kuwa amesini dhidi ya Mungu? Daudi alielewa kwamba dhambi zote hatimaye ni asi dhidi ya Mungu. Mungu ni wa milele na usiye na mwisho (Zaburi 90:2). Matokeo yake, dhambi zote inahitaji adhabu ya milele. Mungu ni mtakatifu, kamili, na aliye na tabia iliyo ya milele amechukizwa na dhambi zetu. Ingawa akili zetu za dhambi zilizo na mwisho ni za muda, kwa Mungu-ambaye hana mipaka ya muda, dhambi ambayo anaichukia unaendelea sana. Dhambi zetu milele ziko mbele yake na lazima milele tuadhibiwe ili kukidhi haki yake takatifu.

Hakuna mtu anaelewa hili bora kuliko mtu aliye katika moto wa Jehanamu. mfano kamili ni hadithi ya mtu tajiri na Lazaro. Alikufa, na tajiri kwenda kuzimu wakati Lazaro alienda peponi (Luka 16). Bila shaka, tajiri alikuwa na ufahamu kwamba dhambi zake zilitendwa wakati alikuwa hai. Lakini, cha kushangaza, yeye kamwe anasema, "Nilifikaje hapa?" Swali Hili kamwe haliulizwi katika moto wa Jehanamu. Hasemi, kuwa "Je, mimi kwa kweli ninastahili hili? Je, unafikiri hii haipiti kiwango? juu kidogo sana?" Yeye tu anauliza kwamba kama mtu anaweza kwenda kwa ndugu zake ambaye bado wakoi hai na kuwaonya dhidi ya hatma yake.

Kama mtu tajiri, kila mwenye dhambi katika kuzimu ana utambuzi kamili kwamba yeye anastahili kuwa huko. Kila mwenye dhambi ana taarifa za kutosha, wanatambua, na wenyei dhamiri kwaamba, katika kuzimu, anakuwa wa matezo yake mwenyewe. Huu ni uzoefu wa mateso katika kuzimu-mtu hufahamu kikamilifu dhambi yake na dhamiri bila kushitaki dhamira yake, bila misaada hata wakati mmoja. hatia ya dhambi huzalisha aibu na chuki ya binafsi milele. Tajiri alijua kwamba adhabu ya milele kwa ajili ya maisha ya dhambi ni haki wanastahili. Hiyo ndio kwa nini yeye kamwe hakupinga au kuuliza maswali ya kwa nini yuko katika moto wa Jehanamu.

Ukweli wa hali halisi ya laana ya milele, kuzimuni milele, na adhabu ya milele ni ya kutisha na ya shaka. Lakini ni vizuri sana kwamba tuweze kwa kweli, kuwa na hofu. Wakati hili linaweza kuonekana mbaya, kuna habari njema. Mungu anavyotupenda (Yohana 3:16) na anataka sisi tuokolewe kutoka kuzimu (2 Petro 3:9). Lakini kwa sababu Mungu pia ni wa haki, hawezi kuruhusu dhambi zetu kwenda bila adhabu. Mtu alipe kwa kwa ajili yake. Katika huruma yake kubwa na upendo, Mungu alitoa malipo yake mwenyewe kwa dhambi zetu. Yeye alimtuma Mwana wake Yesu Kristo kulipa adhabu kwa dhambi zetu kwa kufa msalabani kwa ajili yetu. Kifo cha Yesu ni kifo takatifu kwa sababu yeye ni Mungu / mtu aisye na mwisho, kulipa madeni yetu ya dhambi ya milele, ili isiwe ni lazima sisi kulipa katika moto wa Jehanamu milele (2 Wakorintho 5:21). Tukiziungama dhambi zetu na kuweka imani yetu katika Kristo, tukiomba msamaha kwa Mungu kwa msingi ya sadaka ya Kristo, sisi tutaokolewa, kusamehewa, kutakaswa, na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. Mungu alitupenda sisi sana kiasi kwamba alitoa njia ya wokovu wetu, lakini kama sisi tunakataa zawadi yake ya uzima wa milele, sisi hukabiliana na matokeo ya milele ya uamuzi huo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni namna gani milele katika moto wa Jehanamu ni adhabu ya haki kwa ajili ya dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries