Swali
Je, wale watu wanaodai kuwa wanazungumza na Mungu ni wenda wazimu?
Jibu
Hakuna jambo la kichaa, la kipuuzi, au lisilo na akili kuhusu mtu anayezungumza na mwingine. Maombi kwa ufupi ni mawasiliano na Muumba wetu. Mungu ni roho, lakini Yeye pia ni nafsi, kumaanisha kwamba ana utu, mwenye hisia, tamaa, na akili. Anafurahia utangamano na viumbe wake, na wakati tunachagua kumtafuta Yeye, Anaahidi kuwa tutampata Yeye (Yeremia 29:13). Biblia imejaa mawasiliano kati ya Mungu na watu, tukianzia Bustani mwa Edeni (Mwanzo 2:17). Mungu alimuumba mwanadamu kwa ajili ya ushirika, na mawasiliano sehemu kubwa ya hilo. Anatufurahia na anataka tumfurahie Yeye (Zaburi 37:4, 23).
Mungu mwenyewe anatualika tumwite, na anaahidi kujibu (Yeremeia 29:12; Zaburi 50:15; Waefeso 6:18; 1 Yohana 5:14). Yesu alitufundisha jinsi ya kuomba katika yale yamekuja kujulikana kama “Sala ya Bwana” (Luka 11:2-4). Sala yake mwenyewe iliyorekodiwa katika Yohana 17, pia ni kielelezo kizuri cha sala ya kutoka moyoni, ya kindani kati ya Baba na Mwana. Ikiwa tumekuwa watoto wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo, tunaweza kuomba kwa ukaribu na kujua kwamba Baba yetu anatusikia (Yohana 1:12).
Kunayo matukio mengi ya kutaja ya watu wenye akili timamu wakizungumza na Mungu. Baadhi yao wanaostahiki zaidi ni Musa (Kutoka 4:10), Eliya (Yakobo 5:17), Daudi (2 Sameli 24:10), na Yesu Mathayo 11:24; Yohana 17:1). Viongozi wengi wakuu wa zamani walitegemea maombi kufanya maamuzi yao. George Washington, Abraham Lincoln, na wengi wa Mababa waanzilishi wa Marekani waliamini sana nguvu ya maombi. Wanasayansi wakubwa kama vile Isaac Newton, Louis Pasteur, Francis Bacon, George Washington Carver, na Galileo pia waliamini katika maombi. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kuainishwa kama “mwendawazimu.”
Wale wanaotembea kwa karibu na Mungu pia husikia sauti Yake ikisungumza nao. Sauti ya Mungu ni nadra kusikika. Anazungumza ndani ya moyo wa mtu ambaye amejitoa kikamilifu kwake (Matendo 8:29; 10:19; 2 Wakorintho 12:9). Anazungumza kupitia Roho Wake Mtakatifu ndnai ya mioyo ya watoto wake ili kuwaongoza, kuwalinda na kuwatia moyo (Warumi 8:14; Wagalatia 5:18). Yesu alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu” (Yohana 10:27).
Wakati tunaweka imani yetu kwa Yesu Kristo kwa wokovu, Roho Mtakatifu wa Mungu huja kuishi ndani ya mioyo yetu (1 Wakorintho 6:9). Anatusaidia kuomba kwa njia inayowasilisha matamanio halisi ya mioyo yetu kwa Mungu (Warumi 8:26). Katika Yohana 14:26 Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Mara nyingi, jibu la Mungu kwa maombi yetu tayari linapatikana katika Neno lake. Tunapoomba, Roho Mtakatifu huleta Neno Lake akilini, nasi tunapata jibu letu. Wanadamu hawajawahi kuwa vile waliumbwa hadi wajifunze kuwasiliana na Muumba wao.
English
Je, wale watu wanaodai kuwa wanazungumza na Mungu ni wenda wazimu?