settings icon
share icon
Swali

Kwa nini tutafiti Agano la Kale?

Jibu


Kuna sababu nyingi za kusoma Agano la Kale. Moja , Agano la Kale huweka msingi kwa mafundisho na matukio ya kupatikana katika Agano Jipya. Biblia ni ufunuo wa kuendelea. Kama unaruka nusu ya sehemu ya kwanza ya kitabu chochote nzuri na kujaribu kumaliza, utakuwa na wakati mgumu kuelewa wahusika, njama, na mwisho. Katika njia sawia, Agano Jipya laweza tu kueleweka kabisa wakati tunauona msingi wake wa matukio, wahusika, sheria, mfumo wa sadaka, maagano, na ahadi za Agano la Kale.

Kama tungekuwa na Agano Jipya pekee, tutakuja kwa Injili bila kujua ni kwa nini Wayahudi walikuwa wakimtazamia Masihi (Mwokozi mfalme). Sisi hatungeelewa ni kwa nini Masihi alikuja (ona Isaya 53), na sisi hatungeweza kuwa na uwezo wa kumtambua Yesu wa Nazareti kama Masihi kupitia kwa unabii mwingi wa kina kuwa walipewa habari zake [ kwa mfano, mahali pakepa kuzaliwa (Mika 5: 2), njia yake ya kifo (Zaburi 22, hasa mistari 1, 7-8, 14-18; 69:21), ufufuo wake (Zaburi 16:10 ), na maelezo mengi zaidi ya huduma yake (Isaya 9:2; 52:3 )].

Utafiti wa Agano la Kale ni muhimu kwa ajili ya kuelewa mila za Wayahudi zilizotajwa katika Agano Jipya. Sisi hatuwezi elewa njia Mafarisayo walibadilisha sheria ya Mungu kwa kuongeza mila zao wenyewe, au ni kwa nini Yesu aliudhika huku akisafisha Hekalu, au ni wapi ambapo Yesu aliyapata maneno Yeye aliyatumia katika majibu yake mengi kwa wote waliompinga.

Agano la Kale limekumbukumbu unabii mbalimbali wa kina ambao unaweza tu kuwa kweli kama Biblia ni neno la Mungu, na si ya mtu (kwa mfano, Daniel 7 na sura zifuatazo ). Unabii wa Danieli unatoa maelezo maalum kuhusu kuinuka na kuanguka kwa mataifa. Nabii hizi ni sahihi, kwa kweli, wale wasiwasi huchagua kuamini yaliandikwa baada ya ukweli.

Tunapaswa kulichunguza Agano la Kale kwa sababu ya masomo mengi linayo kwa ajili yetu. Kwa kuangalia maisha ya wahusika wa Agano la Kale, tunaona mwongozo kwa ajili ya maisha yetu. Sisi tunahimizwa kumwamini Mungu bila kujali (Danieli 3). Sisi hujifunza kusimama imara katika imani yetu ( Danieli 1) na si kwa kusubiri malipo ya uaminifu wetu (Danieli 6). Sisi hujifunza na ni bora kukiri dhambi mapema na kwa dhati badala ya kunyoshea kidole cha lawama (1 Samweli 15). Tunajifunza kuwa tusichejeze na dhambi, kwa sababu tutajipata nje (Waamuzi 13-16). Sisi hujifunza kwamba dhambi yetu ina madhara siyo tu kwa mwenyewe lakini kwa wapendwa wetu Mwanzo 3) na, kinyume chake, kwamba tabia yetu nzuri ina malipo kwa ajili ya sisi na wale walio karibu nasi (Kutoka 20:5-6).

Utafiti wa Agano la Kale pia unatusaidia kuelewa unabii. Agano la Kale lina ahadi nyingi kwamba Mungu bado atatimiza kwa taifa la Wayahudi. Agano la Kale inaonyesha mambo kama vile urefu wa dhiki, jinsi utawala ujao wa Kristo wa miaka 1,000 utatimiza ahadi zake kwa Wayahudi, na jinsi hitimisho la Biblia linakutanisha mwisho wenye mwanya vile tulivo eleza katika hapo mwanzo.

Kwa muhtasari, Agano la Kale linaturuhusu sisi kujifunza jinsi ya kumpenda na kumtumikia Mungu, na linatuonyesha zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Inaonyesha ikirudia mara kwa mara unabii ulio timizwa kwa nini Biblia ni ya kipekee miongoni mwa vitabu takatifu peke yake na ni biblia pekee ina uwezo wa kuonyesha kwamba yatangaza kile iko: Neno la Mungu lililo na pumzi. Kwa ufupi, kama wewe bado hujaingia ndani katika kurasa za Agano la Kale, wewe unakosa mengi ambayo Mungu ako nayo tayari kwa ajili yako.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini tutafiti Agano la Kale?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries