Swali
Lugha tano za mapenzi ni zipi?
Jibu
The 5 Love Languages: The Secret to Love That Lasts au Lugha 5 za upendo: Siri ya Upendo Unaodumu ni kitabu kilichoandikwa na Gary Chapman ambacho kinachunguzia njia ambazo watu hutoa na kupokea upendo. Katika kitabu hicho, Chapman anapendekeza kwamba kila mtu hupokea upendo kwa angalau moja ya njia hizo tano: maneno ya uthibitisho, matendo ya huduma, zawadi, wakati bora, na mguzo wa kimwili. Jinsi tunavyopokea upendo kwa kawaida ndivyo tunavyoonyesha upendo, lakini ikiwa mpendwa wetu hatapokea upendo kwa njia ile ile tunayopokea, anaweza kuhisi kwamba hapendwi. Lugha 5 za Upendo ziliuzwa zaidi katika New York Times #1 mwanzoni mwa miaka ya 1990 na imesalia kuwa maarufu kwa hekima yake isiyopitwa na wakati na inayotoa usaidizi wa vitendo.
Aina tano ambazo watu hutoa na kupokea upendo huathiri sana uhusiano. Tunapoelewa lugha ya upendo ya mtu mwingine, tunaweza kuonyesha heshima na upendo wetu kwake kwa ufanisi zaidi. Watu wengine wana lugha ya msingi ya mapenzi na lugha nyingine pia. Maswali ya bure yanapatikana kwneye tovuti ya Lugha 5 za Upendo ili mtu yeyote aweze kuamua lugha yake ya mapenzi na pia lugha za watu walio maishani mwao.
Yafutayo ni maelezo mafupi ya kila moja ya lugha tano za mapenzi:
1. Maneno ya uthibitisho. Baadhi ya watu wana mazoea zaidi kuliko wengine, kusikia maneno mazuri na yale mabaya kutoka kwa wale ambao maoni yao wanayathamini. Ingawa maneno mabaya, ya kukosoa yanaweza kuwafanya wahisi vibaya, maneno mazuri na yenye kutia moyo huwafanya wasitawi. Watu wanaohitaji uthibitisho wa maneno pia huwa huru na maneno yao ya kutia moyo. Wanafikiri kwamba, kwa sababu wanahitaji sana sifa ya maneno, wapendwa katika maisha yao pia wanayahitaji. Ingawa watu wengi hufurahia kusikia maneno ya sifa, wale ambao lugha yao kuu ya upendo ni maneno ya uthibitisho huyatamani sana. Mara nyingi watapanga maisha yao kwa uwezekano wa kupokea sifa, hata kupuuza kusema ukweli mbaya wakati inapobidi.
Wanandoa na wengine wanaotaka kuwasiliana na mtu aliye na lugha hii ya upendo ni lazima wajizoeshe kueleza hisia zao kwa maneno. Kwa mtu asiye na lugha hii ya upendo, inaweza kuwa vigumu mwanzoni kuzungumza kile anachofikiri kwamba mtu mwingine tayari anajua. Lakini uthibitisho rahisi kama vile “Ulifanya kazi nzuri!” au Ninajivunia wewe!” huchangia sana katika kujenga ujasiri na “kujaza mtungi wa upendo” wa mtu anayehitaji maneneno ya uthibitisho.
2. Metendo ya huduma. Wakati matendo ya huduma ni lugha ya msingi ya mtu, yeye hutafsiri msaada kama ishara ya upendo wa mtu. Kwa mfano, mwenzi wa ndoa anapofanya kazi za nyumbani, jitihada zake hutafsiriwa na mwenzi mwingine kuwa upendo, ingawa hakuna maneno halisi ya upendo yanayosemwa. Hata hivyo, ikiwa matendo ya huduma si lugha ya upendo ya mwenzi anayesaidia, mwenzi huyo anaweza kuwa hajui maana ya matendo hayo kwa mke au mume wao. Kwa mfano, mume anaeza kuosha vyombo kwa sababu vilikuwa vichafu. Lakini kwa mke, ambaye kwa kawaida huosha vyombo, tendo lake la huduma linasikika kama wimbo wa mapenzi.
Watu wenye lugha hii ya upendo mara nyingi hufanya jambo bila watu kutambua, wakifanya kile ambacho hakuna mtu mwingine aliyejitolea kufanya. Ni zawadi yao kwa watu wanaowajali. Wanafikiri kwamba wapokeaji wa huduma yao wataelewa sababu za huduma hiyo, lakini wanavunjika moyo wanapohisi wamepuuzwa. Kwa mfano, mke mwenye lugha hii ya upendo huhisi kupendwa na mume wake anapofanya mambo nyumbani, lakini anapomrudishia na kumfanyia jambo fulani, haipokei kama ishara ya upendo. Lugha yake ya upendo inaweza kuwa maneno ya uthibitisho, kwa hivyo majaribio ya mke wake ya kumwonyesha upendo kupitia vitendo vya huduma yatakosa kuthaminiwa, na “chombo chake cha upendo” kinaweza kubaki tupu.
3. Zawadi. Sisi sote tunawajua watu ambao hubeba zawadi kila mahali waendapo. Wanaweza kuwa “wananunua zawadi ndogo” kwa ajili ya watu maishani mwao. Watu hawa hustawi kwa kupeana zawadi, na, wanapopewa zawadi, kapu lao la upendo hujaa. Wakati mwingine watu hawaelewi hitaji hili la kuonyesha upendo kupitia utoaji wa zawadi na hutafsiri matoleo ya kila mara kama rushwa au matarajio ya kitu kama malipo. Zawadi zinapokuwa lugha kuu ya upendo ya mtu, kwa kawaida yeye huweka uzito mkubwa juu ya ubora wa zawadi hiyo na jitihada iliyofanywa ili kuipata. Zawadi hazihitaji kuwa ghali, lakini wakati mwingine hupewa maana zaidi kuliko ilivyokusudiwa na mtoaji. Kwa mfano, ikiwa hii ni lugha ya msingi ya mapenzi ya mwanamke, anaweza kutia maana zaidi kwa bangili kuliko vile mpenzi wake alivyokusudia. Aliipata ikiuzwa na alijua siku yake ya kuzaliwa ilikuwa inakaribia, kwa hivyo, kwa msukumo, aliinunua. Kwa upande mwingine, mwanamke huyo anatafsiri zawadi kama tamko la mpenzi wake la upendo na anaweza kudhani kuwa uhusiano huo unaendelea kuwa wa undani zaidi.
Ni muhimu kuelewa watu katika maisha yetu ambao wanatoa na kupokea upendo kwa njia ya kutoa zawadi. Wakati hii ndiyo lugha ya msingi ya upendo, wale wanaomjali mtu huyo wanaweza kujifunza kutoa zawadi kwa uangalifu ili kuonyesha upendo wao. Ua la waridi, mshumaa, au kadi ya kuchekesha inaweza kusaidia sana kujaza kapu la upendo la mtu ambaye anaelewa upendo kuwa ni kutoa zawadi.
4. Muda bora. Muda mzuri kwa kawaida huhusishwa na mazungumzo ya maana kwa watu walio na lugha hii ya msingi ya upendo. Masaa ya mazungumzo ya kina huunda muunganisho wa kihemko kwao. Kuna wazo kuwa, “Ikiwa mtu huyu ananijali vya kutosha kutumia wakati huu wote pamoja nami, basi ananipenda sana.”
Njia bora ziadi ya kuwasiliana kwa upendo na mtu ambaye lugha yake kuu ni wakati bora nikuondoa vikengeushi kama vile rununu na runinga na kumsikiliza kwa kweli anachosema. Tunaweza kujizoesha kutoa mwitikio wa maneno kuonyesha kwamba tunasikiliza. Hadhira iliyokengeushwa huwasiliana na zaidi na mtu huyo kuliko tunavyoweza kutambua ikiwa hii si lugha yetu ya msingi. Kuvuruga mara kwa mara humwambia mtu huyo, “Wewe si muhimu vya kutosha kwangu kukufikiria wewe pekee.” Wale wanaotaka kuwasilisha upendo kwa mtu anayetumia lugha hii ya msingi wanaweza kutenga nyakati mahususi za kukaa pamoja bila kukatizwa. Matukio ya pamoja, kucheka pamoja, na kuzungumza kuhusu mambo muhimu hujaza kapu la upendo la mtu anayehitaji muda bora.
5. Mguso wa kimwili. Mguso wa mwili ni muhimu kwa afya na ustawi wa kila mwanadamu. Watoto ambao hawapati mguso wa kutosha wa upendo wakiwa wachanga hawastawi na wanaweza kuwa na matatizo maisha yao yote. Lakini kwa baadhi ya watu hitaji la kuguswa kimwili ni kubwa kuliko lilivyo kwa wengine. Kukumbatia kwa upendo, kusugua mgongo, kushikana mikono, au kuminya bega, yote huwasilisha upendo kwa watu hawa. Vitendo hivyo vinaashiria upendo kwa wale walio na lugha hii ya msingi. Ingawa ngono inaweza kuwa sehemu ya lugha hii ya upendo, hitaji hili la mguso wa kimwili si la ngono. Kugusa, kupapasa, kukumbatiana na busu kwenye shavu hujaza kapu la upendo la wale walio na hitaji hili.
Walakini, mtu huyu anapojaribu kuonyesha mapenzi kwa mtu ambaye mguso wa kimwili sio lugha yake ya msingi, jambo hilo linaweza kutafsiriwa vibaya. Kesi za unyanyasaji wa kijinsia zimewasilishwa dhidi ya watu wasio na hatia ambao walidhani kwamba kugusa kwao kusio kwa kingono kulionyesha heshima na upendo wakati kwa kweli kulitafsiriwa kuwa ni mwaliko wa tendo la ngono. Watu walio na lugha hii ya msingi ya upendo wanahitaji kukumbuka kwamba kugusa kunaweza kumaanisha mambo mbalimbali, na nia yao haifahamiki wazi kila wakati. Hitaji hili pia linaweza kuleta mvutano katika ndoa wakati mwenzi wa ndoa anataka tu kubembeleza, lakini mwingine anatafsiri mguso wa kimwili kama mwaliko wa ngono. Kuwasiliana waziwazi kuhusu ni aina gani ya miguso inayohitajika kunaweza kuwasaidia wenzi wote wawili kujifunza kujaza kapu la upendo la mwingine.
Kunazo njia nyingi za kuonyesha upendo, na kama wafuasi wa Kristo, tunapaswa kutumia zote. Lakini katika mahusiano ni muhimu kuelewa jinsi tunavyopokea upendo na jinsi wale tunaowajali wanavyopokea upendo wetu. Kujielimisha wenyewe kuhusu utata wa asili ya mwanadamu hutusaidia kujua jinsi ya kuitikia wale ambao Mungu analeta katika maisha yetu, na Lugha 5 za upendo ni mahali pazuri pa kuanzia.
English
Lugha tano za mapenzi ni zipi?