Swali
Je! kutakuwa na machozi mbinguni?
Jibu
Biblia haitaji kamwe machozi mbinguni. Yesu anazungumza juu ya furaha inayotukia mbinguni wakati mwenye dhambi mmoja anatubu (Luka 15:7,10). Biblia inasema kwamba, hata sasa, wale wanaomwamini Yesu Kristo “mnamwamini na kujawa na furaha isiyoneneka yenye utukufu usioelezeka” (1 Petro 1:8)—kiwa maisha yetu ya kidunia yana sifa ya shangwe hivyo, je, shangwe ya mbinguni itakuaje? Hakika, mbinguni kutakuwa mahali pa furaha zaidi. Kinyume chake, Yesu alieleza kuzimu kuwa mahali pa kulia na “kusaga meno” (Luka 13:28). Kwa hiyo, baada ya kuangalia Maandiko kwa upesi, inaonekana kwamba machozi yatakuwa sehemu ya milki ya kuzimu, na hakutakuwa na machozi mbinguni.
Ahadi ya Mungu daima imekuwa kuondoa huzuni ya watu wake na badala yake kuwapa furaha. “Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha” (Zaburi 30:5). Na, “Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe” (Zaburi 126:5). Kama katika mambo mengine yote, Yesu ndiye kielelezo chetu katika hili. Bwana wetu ndiye “ mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2). Kilio cha Yesu kilileta shangwe inayotungojea.
Wakati unakuja ambapo Mungu ataondoa machozi yote kutoka kwa waliokombolewa. “Yeye atameza mauti milele. Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote; ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. Bwana amesema hili” (Isaya 25:8). Mtume Yohana ananukuu unabii wa Isaya anapoandika maono yake ya mbinguni katika Ufunuo 7:17. Mwishoni kabisa wa wakati, Mungu anatimiza ahadi yake: “Atafuta kila chozi kutoka macho yao” (Ufunuo 21:4). Kinachovutia ni wakati wa tukio hili: linatokea mbele ya Kiti Kikuu cha Enzi Cheupe cha Hukumu (Ufunuo 20:11-15) na baada ya kuumbwa kwa mbingu mpya na dunia mpya (Ufunuo 21:1).
Fikiria hili: ikiwa Mungu atafuta kila chozi baada ya uumbaji mpya, hiyo inamaanisha kwamba kuna uwezekano wa kuwa na machozi hadi wakati huo. Inaweza kuwaziwa, ingawa hakuna uhakika, kwamba kuna macho mbinguni kuelekea uumbaji mpya. Machozi mbinguni yanaonekana kuwa sio mahali pake, lakini hapa kuna nyakati chache ambazo tunaweza kukisia kwamba machozi yanaweza tiririka, hata mbinguni:
1) Katika Kiti cha Hukumu cha Kristo. Waumini watakabiliwa na wakati ambapo “ubora wa kazi ya kila mtu” (1 Wakorintho 3:13). yule ambaye kazi zake zinapatikana kuwa “miti, majani, au nyasi…atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa- lakini tu kama mtu aliyenusurika kwenye moto” (aya ya 12 na 15). Kuteseka kwa kupoteza thawabu kwa hakika kutakuwa wakati wa huzuni-je huu unaweza kuwa wakati wa machozi mbinguni, tunagundua ni kiasi gani tulipaswa kumheshimu Bwana? Labda.
2) Wakati wa dhiki. Baada ya muhuri wa tano kuvunjwa, mateso ya waumini wakati wa dhiki yanazidi. Wengi wanauawa na mnyama au Mpinga Kristo. Hawa wanaokufa kwa ajili ya imani wanaonyeshwa katika Ufunuo 6 wakiwa chini ya madhabahu mbinguni, wakimngojea Bwana kulipiza kisasi: “Hata lini, Ee Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, hutawahukumu na kulipiza kisasi juu ya watu waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” (mstari wa 10). Nafsi hizi ziko mbinguni, lakini bado wanakumbuka tukio la kifo chao, na wanatafuta haki. Je, watu hawa wanaweza kuwa wanaendelea kutoa machozi wanapokesha? Labda.
3) Katika adhabu ya milele ya wapendwa. Tukifikiri kwamba watu mbinguni wana ujuzi fulani juu ya kile kinachotokea duniani, huenda tukajua wakati mpendwa wetu atakapomkataa Kristo na kuingia katika umilele usiomwogopa Mungu. Hii itakuwa maarifa ya kufadhaisha, kwa kawaida. Wakati wa Hukumu ya Kiti Kikubwa cha Enzi Cheupe, je, wale walio mbinguni wataweza kuona matukio, na ikiwa ndivyo, watamwaga machozi juu ya wale waliohukumiwa? Labda.
Tena, tumekuwa tukikisia. Hakuna mtajo wa kibiblia wa machozi mbinguni. Mbinguni kutakuwa mahali pa faraja, pumziko, ushirika, utukufu, sifa, na furaha. Ikiwa kuna machozi, kwa sababu zilizoorodheshwa hapo juu, wote watafutwa katika hali ya milele. “Wafarijini, wafarijini watu wangu, asema Mungu wenu” (Isaya 40:1). Na, “Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, “Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya!” (Ufunuo 21:5).
English
Je! kutakuwa na machozi mbinguni?