settings icon
share icon
Swali

Masadukayo na Mafarisayo walikuwa akina nani?

Jibu


Injili yarejelea mara nyingi Masadukayo na Mafarisayo, kuwa Yesu alikuwa katika vita vya mara kwa mara pamoja nao. Masadukayo na Mafarisayo yalikuwa nia makundi tawala kwa wa Israeli. Kuna kufanana kati ya makundi haya mawili lakini tofauti muhimu yao pia ni nyingi.

Masadukayo: Wakati wa Kristo na wakati wa Agano Jipya, Masadukayo walikuwa maarufu. Wao wakijifanya kuwa tajiri na walikuwa na vyeo vya nguvu, ikiwa ni pamoja na kile cha makuhani na kuhani mkuu, na wao walikuwa wengi kwa wale 70 wa halmashauri ya chama tawala cha kuitwa Sanhedrin. Walifanya bidii kuweka amani na kukubaliana na maamuzi ya Roma (Israeli wakati huu ilikuwa chini ya utawala wa Kirumi), na walionekana kuwa na wasiwasi zaidi na siasa kuliko dini. Kwa sababu walikubalika na Roma na walikuwa matajiri sana, hakuwa na uhusiano mwema na watu wa kiwango cha chini, wala mtu wa kawaida kuwapisha katika maoni makuu. Mtu wa kawaida alihusiana bora na wale ambao ni wa kikundi cha Mafarisayo. Ingawa Masadukayo walikuwa na nyadhifa nyingi katika baraza, historia inaonyesha kwamba muda mwingi huwa walikuwa wanafuata mawazo ya wachache Mafarisayo, kwa sababu Mafarisayo walikuwa maarufu kwa raia.

Kidini, Masadukayo walikuwa kihafidhina zaidi katika eneo moja kuu la mafundisho. Mafarisayo waliumpa utamaduni simulizi mamlaka sawa na Neno la Mungu lililoandikwa, wakati Masadukayo walichukulia Neno lililoandikwa kuwa kutoka kwa Mungu. Masadukayo huhifadhi mamlaka ya Neno la Mungu lililoandikwa, hasa vitabu vya Musa (Mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati). Huku wao wanaweza kupongezwa kwa hili, wao dhahiri hawakuwa kamili katika maoni yao ya mafundisho. Zifuatazo ni orodha fupi za imani walishikilia ambazo huitilafiana na maandiko:

1. Walikuwa wa kujitegemea sana kwa uhakika wa kukanusha kuhusika kwa Mungu katika maisha ya kila siku.

2. Walikataa ufufuo wowote wa wafu (Mathayo 22:23, Marko 12: 18-27; Matendo 23: 8).

3 Walikataa maisha yoyote ya baadaye, wakishikilia kwamba roho aliangamia wakati wa kifo, na kwa hiyo wanakana adhabu yoyote au malipo baada ya maisha ya hapa duniani.

4 Wao alikanusha kuwepo kwa ulimwengu wa kiroho, yaani, malaika na mapepo (Matendo 23: 8).

Kwa sababu Masadukayo walijihuzisha zaidi na siasa kuliko dini, hawakuwa na aja na yanayohusika na Yesu mpaka wakawa na hofu kuwa anaweze kuleta makini zisizohitajika kutoka Kirumi. Ilikuwa ni katika hatua hii kwamba Masadukayo na Mafarisayo waliungana pamoja kumweka Kristo katika kifo (Yohana 11: 48-50; Marko 14:53, 15: 1). Tajo linguine la Masadukayo hupatikana katika Matendo 4: 1 na Matendo 5:17, na Masadukayo ni wanaohusishwa na kifo cha Yakobo na historia Yosefe (Matendo 12: 1-2).

Masadukayo walikoma kuwepo katika AD 70. Tangu chama hiki kuwepo kwa sababu ya mahusiano yao ya kisiasa na ukuhani, wakati Roma iliharibu Yerusalemu na hekalu mwaka A.D 70, Masadukayo waliharibiwa pia.

Mafarisayo: Tofauti na Masadukayo, Mafarisayo wengi wao walikuwa wafanyabiashara wa kiwango cha kati, na kwa hiyo walikuwa wanawasiliana na mtu wa kawaida. Mafarisayo waliheshimika sana na mtu wa kawaida kuliko Masadukayo. Ingawa walikuwa wachache katika baraza na kuwa na nyadhifacchache kama makuhani, hao walionekana kudhibiti vyombo vya maamuzi vya baraza mbali zaidi kuliko Masadukayo, tena kwa sababu wao walikuwa na msaada wa watu.

Kidini, walikubali Neno lililoandikwa kuwa liliongozwa na Mungu. Wakati wa huduma ya Yesu huku ulimwenguni, hii ingekuwa chenye Agano la Kale lipo sasa. Lakini pia waliupa mamlaka sawa tamaduni simulizi na jaribio la kuitetea nafasi hii kwa kusema kuwa kihistoria ilienda hadi kwa Musa. Kwa kujibuka tena katika karne, mila hizi ziliongeza kwa Neno la Mungu, ambalo ni kinyume (Kumbukumbu 4: 2), na Mafarisayo walitaka kutii mila hizi kwa ukali pamoja na Agano la Kale. Injili ina wingi wa mifano ya Mafarisayo wakichukulia mila hizi kuwa sawia na Neno la Mungu (Mathayo 9:14, 15: 1-9; 23: 5; 23:16, 23, Marko 7: 1-23; Luka 11:42) . Hata hivyo, hazikubaki kuwa za kweli kwa Neno la Mungu katika kumbukumbu ya baadhi ya mafundisho mengine muhimu. Tofauti na Masadukayo, waliamini yafuatayo:

1. Wao waliamini kwamba Mungu hudhibitiwa mambo yote, lakini maamuzi yaliyotolewa na watu binafsi pia yamechangia mwendo wa maisha ya mtu.

2. Wao waliamini katika ufufuo wa wafu (Matendo 23: 6).

3 Wao waliamini katika maisha ya baadaye, na malipo sahihi na adhabu kwa mtu binafsi.

4 Wao waliamini kuwepo kwa malaika na mapepo (Matendo 23: 8).

Ingawa Mafarisayo walikuwa wapinzani wa Masadukayo, walifanikiwa kuweka tofauti zao juu ya tukio moja- hukumu ya Kristo. Ilikuwa ni katika hatua hii kwamba Masadukayo na Mafarisayo waiiungana pamoja na kuweka Kristo kwa kifo (Marko 14:53, 15: 1; Yohana 11: 48-50).

Huku Masadukayo waliisha kuwepo baada ya uharibifu wa Yerusalemu, Mafarisayo, ambao walikuwa na wasiwasi zaidi na dini kuliko siasa, waliendelea kuwepo. Kwa kweli, Mafarisayo walikuwa kinyume dhidi ya uasi ambao ulipelekea kuharibiwa kwa Yerusalemu mwaka A.D 70, na wao walikuwa wa kwanza kufanya amani na Warumi baadaye. Mafarisayo pia walihusika na mkusanyiko wa Mishnah, hati muhimu kwa kuzingatia muendelezo ya Uyahudi zaidi ya uharibifu wa hekalu.

Wote Mafarisayo na Masadukayo walipokea wingi wa masambulizi mbalimbali kutoka kwa Yesu. Pengine somo bora tunaweza kujifunza kutokana na Mafarisayo na Masadukayo ni kuwa tusiwe kama wao. Tofauti na Masadukayo, sisi huamini kila kitu Biblia inasema, ikiwa ni pamoja na miujiza na maisha ya baadaye. Tofauti na Mafarisayo, sisi hatupaswi kuchukulia kila mila kama yenye mamlaka sawa na bibilia, na tusiruhusu uhusiano wetu na Mungu kupungua na kuwa orodha ya sheria na mila.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Masadukayo na Mafarisayo walikuwa akina nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries