Swali
Je, mahali patakatifu ni nini?
Jibu
Sehemu inayojulikana kama Makatifu atakatifu ilikuwa eneo la ndani na takatifu sana katika hema ya Kale ya Musa na hekalu la Yerusalemu. Mahali Patakatifu palijengwa kama mchemraba mkamilifu. Ilikuwa na sanduku la agano tu, ishara ya uhusiano maalum wa Israeli na Mungu. Kuhani mkuu wa IsraelI ndiye tu alipata kuingia katika mahali Patakatifu. Mara moja kwa mwaka (Yom Kippur) au siku ya Upatanisho, kuhani mkuu aliruhusiwa kuingia kwenye chumba kidogo cha kisicho na dirisha ili kuchoma uvumba na kuinyunyiza damu ya mnyama wa dhabihu kwenye kiti cha huruma cha Sanduku. kuhani alipata msamaha wa dhambi zake mwenyewe na za watu katika kufanya hivyo. Mahali Patakatifu ilikuwa imetenganishwa kutoka kwenye maskani yote ya hema / hekalu kwa pazia, kitambaa kikubwa, cha kitani nzuri na kitambaa cha rangi ya bluu, ya rangi ya zambarau na nyekundu na kilichopambwa na makerubi ya dhahabu.
Mungu alisema kwamba angeonekana katika mahali Patakatifu (Mambo ya Walawi 16: 2); hivyo basi pazia ilihitajika. Kuna kizuizi kati ya mwanadamu na Mungu. Utakatifu wa Mungu haukuweza kupatikana na mtu yeyote isipokuwa kuhani mkuu, mara moja kwa mwaka. "Macho ya Mungu ni safi sana na hayawezi kutazama mabaya" (Habakuki 1:13), na Yeye hawezi kutazama ukaidi. Pazia na mila iliofanywa na kuhani ilikuwa ni kukumbusha kwamba mtu hakuweza kuingia mbele ya uwepo wa Mungu kiholela. Kabla ya kuhani Mkuu kuingia mahali Patakatifu katika Siku ya Upatanisho, alipaswa kuoga, kuvaa nguo za kipekee, kuleta uvumba ili moshi ifunike macho yake kuzuia kumtazama Mungu, na kuleta damu ya sadaka kufanya upatanisho kwa dhambi zake (Kutoka 28; Mambo ya Walawi 16; Waebrania 9: 7).
Umuhimu wa Patakatifu pa Patakatifu kwa Wakristo unapatikana katika matukio yaliyozunguka kusulubiwa kwa Kristo. Wakati Yesu alikufa, jambo la kushangaza lilitokea: "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini" (Mathayo 27: 50-51a). Pazia hazikupazuliwa katikati mtu yeyote. Ilikuwa ni tukio lisilo la kawaida lililofanyika kwa nguvu za Mungu kufanya hatua maalum sana: kwa sababu ya kifo cha Kristo msalabani, mwanadamu hakuwa ametengana na Mungu tena. Mfumo wa hekalu la Agano la Kale ulifanyika kuwa bure pindi tu Agano Jipya liliidhinishwa. Hatuwatemei makuhani sasa ili kutoa sadaka ya ila mwaka mara moja kwa niaba yetu. Mwili wa Kristo "ulipasuka" msalabani, kama vile pazia lilipasuka ndani ya hekalu, na sasa tunapata kumwona Mungu kupitia Yesu: "... tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake" (Waebrania 10: 19-20).
Dhabihu ya wakati wote ya Kristo iliondoa umuhimu wa dhabihu ya mwaka, ambayo haiwezi kamwe kuondoa dhambi (Waebrania 10:11). Sadaka hizo zilikuwa tu kielelezo cha dhabihu kamili iliyokuja, ile ya Mwana-Kondoo Mtakatifu wa Mungu, aliyeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (Yohana 1:29). Mtakatifu wa Watakatifu, uwepo wa Mungu, sasa umefunuliwa wazi kwa wote wanaokuja kwa Kristo kwa imani. Ambapo, mbeleni kulikuwa na kizuizi kilichohifadhiwa na makerubi, Mungu amefungua njia kwa damu iliyomwagika ya Mwanawe.
English
Je, mahali patakatifu ni nini?