settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu mahusiano ambayo ni sumu?

Jibu


Mahusiano ambayo ni sumu ni yale ambayo yanatia sumu amani yetu na uwezo wetu wa kufurahia mtu mwingine. Mahusiano ambayo ni sumu yatamwacha mtu akiwa amechoka, kuchanganyikiwa, na, katika hali nyingine, kuhuzunika. Mahusiano ambayo ni sumu yanaweza kuathiri ushirikiano wa kibiashara, timu ya michezo, na, bila shaka, familia. Ukosefu wa maelewano fulani katika mahusiano ni kawaida; ingawa, baadhi ya watu uingiza sumu katika kila mahusiano, kufanya kutoa na kuchukua afya kutowezekana. Hao ni watu ambao ni sumu, na Biblia ina ushahuri kwetu jinsi ya kuwashughulikia.

Kutakuwa na watu fulani ambao kampuni yao hatuipendelei, lakini hilo haliwafanyi kuwa sumu. Tunaweza kuwa kinyume moja kwa moja katika fikra na mtu lakini tunaweza endelea mahusiano imara. Watu katika pande tofauti ya wigo wa kisiasa wanaweza furahia urafiki wa mwingine, mashabiki wa timu pinzani za michezo wanaweza kuwa mahusiano ya kirafiki, na Wakristo wanaweza kushiriki mwingiliano wa kiafya na wasio Wakristo. Lakini wakati mtu ni sumu, hana uwezo wa kuhifadhi mahusiano ya kiafya na yeyote. Wale pekee ambao wako tayari kuteseka na madai ya kibinafsi ya mtu ambaye ni sumu anaweza kuvumilia mahusiano kama hayo kwa muda mrefu.

Sababu kadhaa ambazo huaamua ikiwa mahusiano ndio sumu au ni mtu ni sumu:

1. Mahusiano huwa ya upande mmoja kabisa kwa faida ya mtu ambaye ni sumu. Watu ambao ni sumu ni wabinafsi ajabu na wanaeza kufikiria juu yao pekee na kile wanachotaka wakati huo. Huu ni uhalifu wa moja kwa moja wa Wafilipi 2:3-4, ambayo inasema, “Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake. Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.” Watu ambao ni sumu wanaweza jifanya wanafanya kitu kwa manufa ya mtu mwingine, lakini kila wakati kuna nia tofauti ambayo ni kile ambacho kitawafaidi wao.

2. Kuna vituko daima katika mahusiano ambayo ni sumu. Cha kushangaza, watu ambao ni sumu mara nyingi wao ndio wanatangaza kwa wote wasikie jinsi “wanachukia vituko”. Bado wanaichochea kila mahali waendapo. Wanaonekana kunawiri kwa hilo. Hawawezi enda kutoka sehemu moja hadi ingine kwa namna rahisi na ya moja kwa moja. Daima wanaingiza sababu, uongo, udanganyifu na hali zenye wazimu ambazo zinachosha kila mtu katika dunia yao. Wanafurahia kutatiza hali rahisi kwa sababu wanataka umakini uaangaziwe kwao.

3. Wao kila wakati wako sahihi. Kila wakati. Watu ambao ni sumu wanatazama kwa dharau kwa yeyote ambaye atajaribu kuwakosoa au kutofautiana na wao. Wanaficha kiburi yao kali na unyenyekevu bandia, lakini kwa nadra hakuna majuto yeyote ya kweli kwa sababu hawaamini wana makossa. Ni kosa la kila mtu mwingine. Mithali 16:18 inasema, “Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.” Majivuno yametawala watu ambao ni sumu, hata wakati wanajaribu kuyaficha kwa kujihurumia au kujifanya wanyonge. Ikiwa huko kwa mahusiano ambayo ni sumu, “uharibifu” ambayo ni sumu mtu amepata kwa sababu ya kiburi mara nyingi hukuangukia wewe pia.

4. Wengine wanahofia makabiliana au marithiano na watu ambao ni sumu. Wanaweza onekana wacheshi na wa furaha kwa wageni, lakini wale wako katika uhusiano na mtu ambaye ni sumu anajua hadithi kamili. Kila maathiriano, haijalishi yanaweza anza bila hatia, yanaishia na furukuta ya hanjari. Kila mtu mwingine yeyote anaachwa ameanguka wakati mtu ambaye ni sumu anaenda bila kufadhaika. Ikiwa utakuwa na wasiwasi kwa kufikiria mathiriano mengine na mtu katika maisha yako, kwa makosa ambayo si yako, inawezekana uko katika mahusiano ambayo ni sumu.

5. Watu ambo ni sumu wanafurahia kuwa waathirika. Kila kitu kinachowafanyikia watu ambao ni sumu, ulimwengu lazima utambue. Wanafikiria hawapaswi kuchukuliwa hatua, kwa sababu sio makosa yao-ingawa ilikuwa makosa yao. Kujihurumia kunajitokeza kwao, ingawa wanaweza ificha kwa nguvu bandia. Wanapenda kuonekana mashahidi na wanaweza jenga hali ambazo zitawaonyesha hivyo. Wale ambao wako katika uhusiano na watu ambao ni sumu mara nyingi wanamalinzia kuonekana watu wabaya. Mara nyingi wageni hukumu kimya kimya marafiki au familia ambao “sio wavumilivu” wa huyu mwathirika masikini, ambayo inaunda mgawanyiko na mavurugano katika mahusiano ya pembeni.

6. Watu ambao ni sumu husema uwongo. Ikiwa midomo yao inasonga, wanadanganya. Wanaongea uwongo kwa urahisi kuliko jinsi wataongea ukweli na ni washawishi kwamba hata wale ambao wanajua vyema kuwaliko wanashuku mitazamo yao wenyewe. Watu ambao ni sumu wanathibitisha uwongo wao kwa kujiambia wenyewe kwamba hawakuwa na chaguo. Wakati wanapatikana katika uwongo, wanaweza jifanya wanajutia, lakini katika wakati huo wote wanaeza kuwa wanaficha uwongo zingine kadhaa ambazo hakuna mtu amezigundua bado. Maandiko yana maneno makali kwa waongo. Mungu ana sera hata kidogo ya kuwavumilia waongo, na hapumbazwi na sababu yao yeyote (Ufunuo 21:8). Mithali 6:16-19 inaorodhesha vitu saba ambavyo Mungu anachukia, na uwongo uko katika orodha mara mbili.

Mfalme Sauli ni mfano wa mtu ambaye ni sumu. Alianza vizuri, lakini mamlaka, kiburi, na wivu ulilemaza moyo wake. Wivu wake wa ghadhabu kwa kijana Daudi ulijidhihirisha wenyewe hadharani katika hisia zilizochanganyikiwa. Wakati mmoja Sauli alikuwa mtulivu na kufurahia mziki wa Daudi; wakati mwingine anajaribu kumuua (1 Samweli19:9-10). Sauli anaonekana kuonyesha majuto, lakini muda mfupi baadaye anawinda Daudi tena (1 Samweli 24:16-17; 26:2, 21). Baadaye, Sauli alikiuka amri zito sana kutoka kwa Bwana hili watu waweze kufikiria vizuri juu yake (1 Samweli 15). Dhambi hiyo iligharimu Sauli ufalme wake.

Tumeitwa kwa amani (Wakolosai 3:15), lakini mahusiano ambayo ni sumu yanaharibu amani. Watu wengine ni wenye matusi kwamba hawawezi turuhusu kutafuta au kupatanisha amani katika sehemu yoyote. Wakati uhusiano unaendelea kujazwa na vituko ambavyo havihitajiki, wakati unajipata unaogopa mlipuko mwingine, wakati hauwezi kuamini chochote huyu mtu anasema, au wakati mtu anaharibu sifa yako na akili zako timamu, basi ni wakati wa kujitenga mbali katika uhusiano.

Zaburi 1 inatoa mafudisho maalum kuhusu kujitenga kutoka kwa waovu wapumbavu. Tunabarikiwa wakati hatutafuti urafiki na wao au kusikiliza ushauri wao. Watu ambao ni sumu wanakaa katika kiwango hicho. Hawafurahi kuharibu maisha yao; lazima wachukue wengine pamoja nao. Inasaidia kukumbuka kwamba hauwezi badilisha mtu ambaye ni sumu, hasa kutoka ndani ya mahusiano mbayo ni sumu. Hauwezi saidia mtu ambaye ni sumu ila tu anataka kusaidiwa.

Wale wa kufurahisha watu mara nyingi ndio waathiriwa wa mahusiano ambayo ni sumu kwa sababu wanataka mtu ambaye ni sumu akuwe kama wao. Lakini kuna nyakati wakati kufunga mlango wa mahusiano ni kitu cha busara kufanya (Mithali 22:24-25). Ikiwa umeolewa na mtu ambaye ni sumu ambaye amegeuza mahusiano yako hadi ndoa ambayo ni sumu, basi ni wakati wa kuipigia kwaheri.

Katika kila hali inayohusisha mahusiano ambayo ni sumu, chukua jambo kwa Mungu katika maombi. Piga kelele hili “upokee huruma na kupata nehema” ikusaidie wakati wa mahitaji (Wabrania 4:16). “Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.” (1 Petro 5:7). Omba kwa Bwana bila kukoma hili kubadilisha moyo wa mtu anayeleta sumu. Kuna matumaini na uponyaji ndani Yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu mahusiano ambayo ni sumu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries