settings icon
share icon
Swali

Kwa nini mume na mke walionekana najisi baada ya kujamiiana?

Jibu


Walawi 15:18 inasema, “Ikiwa mtu atalala na mwanamke, na kukawa na kutoka kwa shahawa, ni lazima wote waoge kwa maji, nao watakuwa najisi mpaka jioni.” Amri hii lazima inaongelea kujamiiana kati ya wachumba waliooana, kwani Sheria mahali pengine inakataza uzinzi na uasherati. Kwa hivyo, wakati wowote mume na mke wanajamiiana, wanaweza kuonekana najisi siku nzima. Inaonekana ajabu, ikiwa ngono katika ndoa sio dhambi, kwamba itaweza fanya wachumba waliooana najisi.

Kuwa najisi kulingana na Sheria haikuwa kisawe na kuwa mwenye dhambi. Sheria ya Agano la Kale inaongea kuhusu aina mbili ya unajisi—maadili na kufuata utaratibu. Unajisi wa maadili ulisababishwa na matendo mabaya kama yale yaliyoorodheshwa katika Mambo ya Walawi 20:10-21, na ilikuwa na adhabu ya kati ya kukosa mtoto hadi kifo. “Unajisi” unasababishwa na ngono katika ndoa ni wa aina ya kufuata utaratibu na hahukubeba adhabu.

Mtu najisi alipaswa kuepuka kugusa vitu takatifu na kufuata maelekezo ya Sheria hili kurudi katika hali safi. Unajisi ulizuia mtu kukaribia madhabahu (Hesabu 5:3). Mtu najisi hangeweza kula chakula kilichobarikiwa au hata kukileta kama zaka (Walawi 7:20-21; Kumbukumbu 26:14). Ikiwa mtu alikuwa najisi wakati wa pasaka, angengoja mwezi mmoja kabla kusherehekea sikukuu (Hesabu 9:6-13).

Kwa kuongeza na mahusiano ya ngono katika ndoa, kulikuwa na sababu zingine za unajisi wa kufuata utaratibu. Utoaji wa shahawa usiku unaosababishwa na mwanaume kuwa najisi wa kufuata utaratibu kwa siku hiyo, na angelala nje ya kambi kwa siku moja (Kumbukumbu la Torati 23:10-11). Pia, wanawake walikuwa najisi wa kufuata utaratibu wakati wa kupata hedhi (Mambo ya Walawi 15:19-23) na baada ya kuzaa (Mambo ya Walawi 12:1-8). Katika ndoa, wawili wanakuwa mwili moja (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:4-6) na wanashiriki unajisi wa kufuata utaratibu katika kujamiiana (Mambo ya Walawi 15:18). Lakini hakuna kitu cha dhambi au mbaya kuhusu ngono katika ndoa, ambayo ilikuwa uvumbuzi wa Mungu na amri kwa wanadamu, hata kabla ya dhambi kuingia jamii ya binadamu (Mwanzo 1:28).

Tunaweza sadiki idadi yeyote ya sababu Mungu alikuwa nayo kwa kutengeneza kanuni hizi kuongoza unajisi, kuanzia usafi wa kimwili kwa watu binafsi na jamii na kwa kusaidia wanandoa kuthamini umaalum wa zawadi Yake ya ngono. Tofauti, baadhi ya jamii kongwe walifikia uchafu wa kushangaza na hali kali, kuishi kama wanyama wa porini na kuendeshwa kwa kila aina ya musukumo badala ya kuishi kama uumbaji wa juu wa Mungu, walioumbwa kwa mfano Wake (Mwanzo 1:26-27).

Lakini sababu ya mwisho ya kila kitu katika eheria ni kiroho. Katika kesi ya sheria ya kuongoza unajisi, sababu ilikuwa kuwaonyesha watu wa Israeli kwamba Mungu ni mtakatifu na mwanadamu sio mtakatifu. Ukweli kwamba mahusiano ya kawaida ya ngono yalisababisha wachumba waliooana kuwa najisi ya kufutuata utaratibu inaonyesha kwamba sisi ni najisi mbele za Mungu, hata kama hatufanyi dhambi moja kwa moja. Sisi ni watu walioanguka tunaoishi ulimwengu ulioanguka, na hata shughuli za kila siku za maisha zinatufanya najisi. Tunahitaji utakaso kabla tumkaribie Mungu Mtakatifu.

Mungu aliambia Israeli, “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu name nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu” (Mambo ya Walawi 20:26). Ukosefu wa utakatifu wa Israeli ulikuwa umewekwa mbele na katikati katika Sheria. “Basi Torati ni nini? Iliingizwa kwa sababu ya makosa” (Wagalatia 3:19). Kile Israeli inahitaji—na kile sisi wote tunahitaji—ni imani ya Ibrahimu, kwa sababu “wale walio wa Imani, hao ndio wana wa Ibrahimu” (mstari wa 7), hiyo ni, wale ambao wanaamini ahadi za Mungu ni wapokeaji wa Baraka za Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini mume na mke walionekana najisi baada ya kujamiiana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries