settings icon
share icon
Swali

Je, siri kuu ni gani ya kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo?

Jibu


Maisha ya ushind ya Kikristo nimaisha ambayo mtu anaishi kwa imani, katika kujisalimisha kwa Mungu mara kwa mara. Maisha ya ushindi ya Kikrito yana mizizi na msingi katika imani. Waebrania 11 yote inasimulia hadithi za wanaume na wanawake ambao kwa imani, walishinda kwa namna fulani. Mungu wetu ni mshindi siku zote, haijalishi adui ni nani. Hata hivyo msalaba wa Kristo sio kwamba Bwana alishindwa, bali ni ushindi: “Sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje,” Yesu alisema katika juma la mwisho la huduma Yake duniani. Mbele ya hakimu kuhani mkuu, Yesu alishuhudia haijalishi adui ni nani. Hata msalaba wa Kristo sio kwamba Bwana alishindwa, bali ni ushindi: “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Marko 14 :62). Huo ndio ushindi ambao waumini hushiriki.

Maisha ya ushindiya Mkristo ni maisha anayoishi mtu kwa ushindi juu ya “Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima” (1 Yohana 2:16). Ni kuushinda woga, na kujua amani ya Mungu (Yohana 14:27; 16:33). Ni ustahimilivu kupitia “shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga” (Warumi 8:35), ikituonyesha kuwa “na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda” (aya ya 37). Maisha ya Ukristo yenye ushindi kwa kawaida huongoza kwenye kwa ushindi kwa kifo chenyewe (1 Wakorintho 15:54-55) na thawabu tukufu mbinguni (Ufunuo 21:7).

“Mwenye haki ataishi kwa imani” (Warumi 1:17), ni ngumu sana kusisitiza sana umuhimu wa imani katika kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo: “Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko ushindi uushindao ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu. Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu (1 Yohana 5:4-5).

Sehemu ya kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo ni kushughulika ipasavyo na majaribu. Waraka wa Kwanza wa Wakorintho 10:13 inasema, “Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.” Katika muktadha wa mstari huu, Paulo anazungumza na kanisa lililozungukwa na ibada ya sanamu na majaribu. Kulikuwa na mikazo ya kijamii, ya kifedha, na ya kisiasa ya kurudi kwenye njia zao za zamani na kushiriki katika mazoea ya kikafiri. Mungu katika uaminifu wake aliwaambia, na anatuambia na sisi pia, kwamba hakuna jaribio mahali popote, wakati wowote ambalo litamshangaza, na Yeye daima atafanya njia ya kuliepuka na hivyo kustahimili. Wakati Mkristo anakumbana na jaribio, wakati wote Mungu atatoa njia iliyo wazi ya kuepuka dhambi, lakini bado ni chaguo la mtu binafsi kuchukua njia ya kutoroka au la. Kuepuka majaribu kunahitaji kujitiisha kwa Mungu kila wakati.

Katika Yohana 15, Yesu anasimulia mfano unaotupa siri ya maisha ya ushindi ya Kikristo. Yesu Kristo ndiye mzabibu, chanzo cha uhai na afya na uzima, na sisi ni matawi, na kikamilifu tunategemea mzabibu. Neno lililotumiwa mara kwa mara katika kifungu hicho mara nyingi hutafsiriwa kama “kaa” au “baki.” Neno la Kigiriki linamaanisha “kaa ulipo.” Mkristo yuko wapi? Mkristo yuko ndani ya Kristo (Waefeso 2:13).

Maisha ya ushindi ya Mkristo ni safari ya imani, sio kwa wokovu wa milele tu, bali maamuzi ya kila siku yanayojengwa katika mtindo wa maisha unaoakisi Kristo (Wagala 2:20). Imani ni uhakikisho tulivu kwamba kile ambacho hatuoni bado ni halisi zaidi, kikubwa zaidi, cha kuamikika zaidi kuliko kile tunachokiona (Waebrania 11:1). Maisha ya imani yanaamua kumwamini Mungu katika mambo yote (Warumi 4:3). “Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo alikoketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani. Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Wakati Kristo, aliye uzima wenu, atakapotokea, ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu” (Wakolosai 3:1-4).

Maisha ya Ukristo ya ushindi ni kuishi katika kulenga mambo ya mbinguni, na sio mambo ya ulimwenguni. Yesu ndiye kielelezo chetu katika hili: “Basi na tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Mtafakarini sana yeye aliyestahimili upinzani mkuu namna hii kutoka kwa watu wenye dhambi, ili kwamba msije mkachoka na kukata tamaa” (Waebrania 12:2-3). Uzima wa milele wa waumini umelindwa na Kristo. Nasi pia tuko katika mkono wa kuume wa Mungu kwa imani. Mkristo mshindi ni yule ambaye anaishi katika ukweli huo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, siri kuu ni gani ya kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries