settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu majaaliwa dhidi ya hiari uhuru?

Jibu


Wakati wa kujadili juu ya majaliwa (kabla ya kuchagua) dhidhi ya hiari uhuru, watu wengi wanapendelea upande mmoja kwa nguvu hivyo kwamba wanakataa kabisa uwezekano wa upande mwingine kuwa na hata dalili ya ukweli. Wale wanaosisitiza sana utawala wa Mungu katika kuchagua watakaookolewa mara nyingi huchukua msimamo unaofanana na uamuzi mgumu au falsafa ya jaala (usioepukika). Wale wanaosisitiza uhuru wa kibinadamu wanakaribia kukanusha utawala wa Mungu. Walakini, ikiwa maneno yanaeleweka kwa mjibu wa Biblia, mjadala haupaswi kuwa majaliwa dhidhi ya hiari uhuru, bali badala yake majaliwa na hiari uhuru ya kiwango.

Vifungu kama vile Warumi 8:29-30 na Waefeso 1:5-10 kikamilifu vinafundisha kwamba Mungu huwajalia baadhi ya watu kwa wokovu. Mungu akiamua ni nani atakayeokolewa inategemea utawala wake, tabia yake isiyo na mabadiliko (Malaki 3:6), ujuzi wa mapema (Warumi 8:29, 11:2), upendo (Waefeso 1:4-5), na mpango na furaha yake (Waefeso 1:5). Haja ya Mungu ni kwamba wote waokolewe na wafikie toba (1 Timotheo 2:4, 2 Petro 3:9). Anatoa wokovu kwa kila mtu (Tito 2:11), lakini tunajua kwamba si kila mtu ataokolewa. Jinsi haya yote yanavyofanya kwa pamoja yanaweza kujadiliwa, lakini kujaliwa kwenyewe ni fundisho la Kibiblia. Vifungu vingine vingi vya agano jipya vinarejelea kujaaliwa kwa waumini au kuteuliwa kupata wokovu (Mathayo 24:22,31; Marko 13:20,27; Warumi 8:33; 9:11; 11:5-7,28; Waefeso 1:11; Wakolosai 3:12; 1 Wathesalonike 1:4; 1 Timotheo 5:21; 2 Timotheo 2:10; Tito 1:1; 1 Petro 1:1-2; 2 Petro 1:10).

Hata hivyo, Biblia pia inafundisha kwamba watu wanawajibika kwa uamuzi wao (Yoshua 24:14-15, Luka 10:42, Waebrania 11:24-25). Je, hii inafanya kazi vipi na hiari ‘uhuru’? Swali tunalopaswa kujiuliza ni nini maana ya kuwa na hiari uhuru (uhuru wa kuchagua)? Changamoto moja katika mjadala wa kuhusu uteuzi wa kabla dhidi ya uhuru wa kuchagua ni ufahamu wa kawaida wa uhuru wa kuchagua kuwa uhuru wa kufanya chochote tunachochagua. Hii sio jinsi Biblia inavyowasilisha hiari uhuru, wala haiendani na ukweli. Uhuru wetu daima unapunguzwa na mazingira yetu na asili yetu: kwa mfano, tuna kikwazo katika ‘‘uhuru’’ wetu wa kupaa kwa sababu hatuna asili ya ndege mnyama, na tunategemea sheria za kimwili kama vile mvuto na mzunguko wa hewa (elimu mwendo). Biblia inafundisha kwamba bila Kristo sisi ni “wafu sababu ya makosa na dhambi zetu” (Waefeso 2:1). Ikiwa tumekufa kiroho, bila shaka hilo huathiri maamuzi yetu. Yohana 6:44 inasema kwamba, “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.”. Ikiwa uamuzi wa kuamini katika Kristo hauwezekani bila Mungu “kuingilia kati,” basi hiari yetu si “huru” kabisa. Hata hivyo, Mungu anatoa wokovu kwa kila mtu (Tito 2:11) na amejiweka wazi kwa kila mtu ili kila mtu asiwe na udhuru (Warumi 1:19-20).

Tuko na hiari huru kiwango kwamba tunaweza kufanya maamuzi ya kimaadili. Walakini,maamuzi yetu yanakumbwa na sababu nyingi, kama vile, asili yetu ya dhambi, malezi yetu, akili yetu, mafunzo/elimu yetu, biolojia yetu, saikolojia yetu n.k. Kwa hivyo, binadamu hawana hiari huru, jinsi inavyofafanuliwa na watu wengi. Tunayo hiari. Tunaweza kufanya maamuzi. Kwa mtazamo wa Kibiblia, tuna jukumu la kujibu kile ambacho Mungu amefunua kwetu, ikiwa ni pamoja na mwito wake wa kuiamini Injili (Yohana 1:12; 3:16; Matendo ya Mitume 16:31; Warumi 10:9-10; Ufunuo 22:17). Lakini, tena hiari yetu kwa kweli si “huru” kwa sababu tunakabiliwa na vikwazo vinavyoathiri maamuzi yetu.

Majaaliwa (uteuzi wa mapema) ni mafundisho wazi kabisa ya kibiblia. Hakika Mungu ni mwenye enzi juu ya kila kitu, ikiwa ni pamoja na nani atakayepata wokovu. Vile vile, tunawajibika kikweli kwa maamuzi yetu yanayohusiana na wokovu. Haya si kweli ambazo ni tofauti kabisa au zisizoweza kupatana. Katika Biblia, Mungu mara kwa mara anatuita kufanya uamuzi na kuamini kwa Kristo ili kupata wokovu, na tunapaswa kutafuta utii kwa amri hizo bila kujali tunavyoelewa uamuzi wa kabla (mbeleni).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu majaaliwa dhidi ya hiari uhuru?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries