settings icon
share icon
Swali

Je, tuna malaika walinzi?

Jibu


Mathayo 18:10 inasema, "Angaliamsidharau mmojwawapo wadogo hawa, kwa maan nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazam uso wa Baba yangu aliye mbinguni." Katika mkudhata, "hawa wadogo" inaweza aidha ashiria wale ambao wamemuamini (mstari 6) au inaweza rejelea watoto wadogo 3-5). Hiki ni kifungu muhimu kuhusu malaika mlezi. Hakuna shaka kuwa malaika wazuri husaidia kulinda (Danieli 6:20-23; 2 Wafalme 6:13-17), kutoa taarifa (Matendo 7:52-53; Luka 1:11-20), mwongozo (Mathayo 1:20 -21; Matendo 8:26), kutoa kwa (Mwanzo 21:17-20; 1 Wafalme 19:5-7), na kuhudumia waumini kwa ujumla (Waebrania 1:14).

Swali ni kama kila mtu au kila muumini - ana malaika ambaye ametengewa. Katika Agano la Kale, taifa la Israeli lilikuwa malaika mkuu (Mikaeli) kwa ajili ya hilo (Danieli 10:21; 12:1), lakini hamna mahali maandiko inasema kwamba malaika ametengwa "kwa ajili ya" mtu binafsi (Malaika wakati mwingine walimtumwa kwa watu, lakini haitaji kazi ya kudumu). Wayahudi wakawa na imani kikamilifu katika malaika walinzi wakati wa kipindi cha kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Baadhi ya babawa mapema wa kanisa waliamini kuwa sio eti kila mtu alikuwa malaika mzuri pekee kwa ajili ya yake, hata pepo pia. Imani katika malaika walinzi imekuwa karibu kwa muda mrefu, lakini hakuna maandiko ya msingi kwa ajili yake.

Tukirudi kwa Mathayo 18:10, neno "yao" ni kiwakilishi cha pamoja katika Kigiriki na kina rejelea ukweli kwamba waumini ni wanahudumiwa na malaika kwa ujumla. Malaika hawa wanaonekana kuwa "daima" hutizama uso wa Mungu, ili kusikia amri yake kuwasaidia waumini wakati inahitajika. Malaika katika kifungu hiki hawaonekani kumlinda mtu sana kama vile kuwa makini kwa Baba mbinguni. Wajibu wa kazi au usimamizi unaonekana, basi, kuja zaidi kutoka kwa Mungu kuliko kwa malaika, ambao huwa na maana kamilifu kwa sababu Mungu peke nidye Mwenye ujuzi. Anaona kila muumini kila dakika, na Yeye peke yake anajua wakati mmoja wetu anahitaji malaika kuingilia kati. Kwa sababu wao daima wanaendelea kuona uso wake, malaika wako tu kusaidia mojawapo wa "wadogo" wake.

Kwa msisitizo haiwezi jibiwa kutoka kwenye maandiko kama au si kila muumini ana malaika mlinzi kwa ajili yake. Lakini, kama nilivyosema awali, Mungu huwa anatumia malaika katika kutuhudumia. Ni kimaandiko kusema kwamba Yeye anatumia wao jinsi anatutumia sisi, yaani, Yeye kwa njia yoyote hatuhitaji sisi wala wao ili kutimiza malengo yake, lakini anaamua kutumia sisi na wao lakini (Ayubu 4:18; 15:15). Katika mwisho, hata kama tuko na au hatuna malaika kwa ajili ya kutulinda sisi, tuna uhakika zaidi kutoka kwa Mungu: kama sisi ni watoto wake kwa njia ya imani katika Kristo, Yeye hufanya mambo yote pamoja kwa ajili ya mema (Warumi 8:28-30), na Yesu Kristo kamwe hatuachi au kututenga (Waebrania 13:5-6). Kama tuna anayejua yote, Mwenye nguvu, Mungu wa umpendo kwetu, je, inajalisha kweli kama kuna au hakuna milele malaika mlinzi wa kutulinda sisi?

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tuna malaika walinzi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries