settings icon
share icon
Swali

Maombezi ni nini?

Jibu


Kwa ufupi kabisa, maombezi ni kitendo cha kuomba kwa niaba ya wengine. jukumu la upatanishi katika sala lilikuwa wazi katika Agano la Kale, katika kesi ya Ibrahimu, Musa, Daudi, Samweli, Hezekia, Elia, Yeremia, Ezekieli, na Danieli. Kristo aneonekana katika Agano Jipya kama mwombezi mkuu, na kwa sababu hiyo, sala yote ya Kikristo inakuwa maombezi kwa vile inqtolewa kwa Mungu kwa njia njia ya Kristo. Yesu alisiba mwanya kati yetu na Mungu wakati alikufa juu ya msalaba. Kwa sababu ya upatanishi wa Yesu, tunaweza sasa omba kwa niaba ya Wakristo wengine au kwa ajili ya waliopotea, kuuliza Mungu kujibu maombi yao kulingana na mapenzi yake. "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati yetu ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu" (1 Timotheo 2:5). "Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na Zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu naye yuko mkono wa kuume wa Mungu tena ndiye anayetuombea"(Warumi 8:34).

Mfano wa ajabu wa maombi ya kuombea hupatikana katika Danieli 9 Una mambo yote ya sala ya kweli ya kuombea. Ni katika kukabiliana na neno la Mungu (mstari wa 2); sifa ya kuwa na bidii (mstari 3) na kujinyima (kifungu cha 4); kujitambulisha bila ubinafsi na watu wa Mungu (mstari wa 5); nguvu na kukiri (v. 5-15); tegemea maadili ya Mungu (vv. 4, 7, 9, 15); na ina utukufu kwa Mungu kama lengo lake (vv. 16-19). Kama Danieli, Wakristo wanafaa kuja kwa Mungu kwa niaba ya wengine kwa uliobondeka na nia toba, wakitambua kwamba hawafai wao wenyewe na kwa nia ya kujinyima. Danieli hasemi, "Nina haki ya kudai hili kwako Wewe Mungu, kwa sababu mimi ni mmoja wale wako wa kipekee, waombezi waliochaguliwa." Anasema, "mimi nina dhambi," na katika athari, "Mimi kwa hakika sina haki ya kudai kitu chochote." Maombezi ya kweli hayatafuti kujua mapenzi ya Mungu pekee na kuona yakitimia, lakini kuyaona yakitimia kama inatufaidi au haitufiadi bila kujali ni nini gharama yetu. Kweli maombezi inataka utukufu wa Mungu, si wetu wenyewe.

zifuatazo ni baadhi ya sehemu ya orodha ya wale ambao tunapaswa kuwaombea: wote walio mamlakani (1 Timotheo 2:2); mawaziri (Wafilipi 1:19); kanisa (Zaburi 122:6); marafiki (Ayubu 42:8); wananchi wenzatu (Warumi 10:1); wagonjwa (Yakobo 5:14); adui (Yeremia 29:7); wale wanaotutesa (Mathayo 5:44); wale ambao hutukana (2 Timotheo 4:16); na watu wote (1 Timotheo 2:1).

Kuna dhana potofu katika Ukristo wa kisasa kwamba wale ambao huomba maombi ya kuombea ni kikundi maalum cha "Wakristo supafu," walioitwa na Mungu kwa huduma maalum ya maombezi. Biblia ii wazi kwamba Wakristo wote wameitwa kuwa waombezi. Wakristo wote wana Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yao na, kama vile Anavyotuombea kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu (Warumi 8:26-27), pia sisi tunapaswa kuombeana. Hii si bahati ambayo ni iko Wakristo wasomi pekee; hii ni amri ya wote. Kwa kweli, kukosa kuombea wengine ni dhambi. "Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema; na kuyoka " (1 Samweli 12:23).

Hakika Petro na Paulo, wakati waliuliza wengine waombea, je, hawakuweka ombi lao kwa wale walio na wito maalum wa maombezi. "Basi, Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likwamoba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake" (Matendo 12:5). kumbuka ni kanisa lote liliomba kwa ajili yake, si tu walio na kipaji cha maombezi. Katika Waefeso 6:16-18, Paulo anawasihi waumini wote wa Efeso - kwa misingi ya maisha ya kikristo, ambayo ni pamoja na maombezi "katika nyakati zote na kila aina ya sala na maombi." Ni wazi, maombezi ni sehemu ya maisha ya Kikristo kwa waamini wote.

Zaidi ya hayo, Paulo alitaka sala kwa niaba yake kutoka kwa waumini wa Kirumi wote katika Warumi 15:30. Pia aliwaimiza Wakolosai kumwombea katika Wakolosai 4:2-3. Hakuna mahali popote katika ombi lolote la Kibiblia kwa maombezi kuna dalili kwamba ni kikundi fulani cha watu wataomba. Kinyume chake, wale ambao wanataka wengine kufanya maombezi kwa ajili yao wanaweza kutumia msaada wote wanaweza kupata! wazo kwamba maombezi ni upendeleo na wito wa baadhi ya Wakristo halina misingi wa kibiblia. Mbaya zaidi, ni wazo haribifu ambalo mara nyingi hupelekea kiburi na hisia ya ubora.

Mungu anawaita wakristo wote kuwa waombezi. Ni mapenzi ya Mungu kwamba kila muumini kuwa hai katika maombi ya kuombea. Ni nafasi ilioje ya kusifiwa kwamba tuna uwezo wa kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha Mwenyezi Mungu na sala zetu na maombi!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maombezi ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries