settings icon
share icon
Swali

Je, maombi ya imani ni nini?

Jibu


Kifungu “maombi ya imani” kinatoka katika Yakobo 5, ambacho kinasema “Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa” (Yakobo 5:15).

Wakristo wengi wanaamini mstari huu unamaanisha kwamba, ikiwa mtu ataomba kwa imani ya kutosha, uponyaji kwa mgonjwa umehakikishwa. Wengine wanaamini kwamba “maombi ya imani” hasa inarejelea maombi yaliyotolewa na wazee wa kanisa, na neno kuokoa wakati mwingine hurejelea faraja na hisia ya kiroho ya Mungu, badala ya uponyaji wa kimwili (soma 2 Wakorintho 1:3-5).

Huu ndio muktadha wa aya hii: “Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa. Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:14-16).

“Maombi ya imani” hufanywa na wazee wa kanisa wanaomtembelea mgonjwa chini ya uangalizi wao wa kiroho. Sala, ikiambatana na upako wa mafuta inatolewa “kwa jina la Bwana”; yaani, katika mamlaka ya Bwana na kutii mapenzi yake. Sala hufanywa kwa uhakika kamili wa nguvu za Mungu za kuponya. Ikiwa ugonjwa fulani ni matokeo ya dhambi ya kibinafsi, basi kuungama na kutubu dhambi hiyo pia kunahitajika.

“Kuinuliwa” kwa Yakobo 5:15 sio kwa kimwili-ingalikuwa hivyo, basi hakuna muumini yeyote anafaa kufa! Wakristo wengi hufa kutokana na magonjwa au majeraha kila mwaka, lakini hii haimanishi kwamba hawana imani au kwamba wale wanaowaombea hawana imani. Inamaanisha tu kwamba haikuwa mapenzi ya Bwana kuponya katika tukio hilo maalum (angalia 1 Yohana 5:14). Sala ya imani hutolewa kwa imani, na sehemu ya imani ni kuamini kwamba Mungu anajua zaidi. Wale wanaosali hawapaswi kuyumbayumba katika uhakika wao kwamba Mungu atafanya yaliyo sawa sikuzote. Baada ya kuomba ombi la imani, kwa furaha tunaweza kuyakabidhi maisha yetu mikononi mwa Mungu. Urejesho wa mgonjwa ambayo Yakobo 5:15 anahakikisha ni kwa mjibu wa maombi ya imani yanayojumuisha hisia, urejesho wa kiroho ambao huja kwa namna ya faraja na imani ya Mungu.

Yesu alizungumza na wanafunzi wake mara kwa mara kuhusu maombi. Aliwaambia waombe uflame wa Mungu uwakilishwe duniani na mapenzi Yake yatimizwe; Aliwaambia waombe riziki yao ya kila siku, msamaha, na nguvu dhidi ya majaribu (Mathayo 6:9-13). Pia aliwaambia kwamba chochote walichoomba kwa jina Lake, kwa ajili ya utukufu wa Mungu, kingefanyika kwa ajili yao (Yahona 14:13-14), na Aliwahakikishia kwamba Mungu anajua jinsi ya kuwapa watoto Wake zawadi nzuri (Mathayo 7:11). Vifungu hivi vyote vinasisitiza wema wa Mungu na kutujali sisi, lakini hakuna hata kimoja kati yao kinachohakikisha uponyaji wa kimwili. Tunaomba mapenzi ya Mungu, tunasihi kwa ajili ya kile tunachotamani, na tunaomba kwa jina Lake, lakini wakati mwingine uponyaji wa kimwili sio mpango Wake kwa ajili yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, maombi ya imani ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries