settings icon
share icon
Swali

Je, kuna umuhimu na thamani gani ya maombi ya kikundi?

Jibu


Maombi ya kikundi miongoni mwa Wakristo ni muhimu na yenye thawabu. Imekuwa hivi tangu mwanzo wa kanisa. Katika Matendo 2, wakati wanafunzi kwa uwezo wa Roho walikuwa wanahubiri na maelfu wakaokolewa, kanisa lilikuwa na mpango, nao waliutekeleza katika jamii. “Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali” (Matendo 2:42). Maombi ya kikundi yalikuwa muhimu katika kanisa la kwanza kama kitu kilichowaunganisha walipokuwa wakitekeleza Agizo kuu.

Katika Matendo 4:31 maombi ya kikundi yametajwa tena, “Walipokwisha kuomba, mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.” Mungu aliwapa ujasiri kundi lote katika kushuhudia kwao kwa kujibu maombi yao. Walihitaji nguvu hii, kwa kuwa walikuwa wanakabiliwa na mateso.

Katika Matendo 6:3-4, “Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, nasi tutatumia muda wetu kuomba na huduma ya neno.” Maombi yalikuwa moja ya vipaumbele vya juu vya uongozi wa kanisa.

Roho Mtakatifu daima anaomba ndani yetu na kupitia kwetu “kwa uchungu usioweza kutamkwa” (Warumi 8:26), na Yesu alifundisha umuhimu wa maombi ya kibinafsi kwa siri katika chumba cha ndani (Mathayo 6). Lakini maombi ya kikundi au ya ushirika yana umuhimu pia. Maombi ya kikundi huwaunganisha waumini na kuwatia moyo waliolemewa na mizigo. Kundi la waumini linapoomba pamoja, matokeo yake ni umoja, unyenyekevu, shukrani, kukiri dhambi, maombezi, na uvumbuzi wa mapenzi ya Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna umuhimu na thamani gani ya maombi ya kikundi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries